Hofu hii inasababishwa na nini na kwanini haikuwapo wakati wa kupigania uhuru?

Hofu hii inasababishwa na nini na kwanini haikuwapo wakati wa kupigania uhuru?

ungeanzisha hii mada nyumbani kwako uwe mwenyekiti wa kikao, wewe unataka kujibiwa yako ya wenzio unaruka ruka tu.. umeulizwa swali rahisi mtu anataka kufahamu MOHAMED SAID ni jina la Kiislam au Kiarabu... kama hujui sema hujui na wewe ufahamishwe ila sio kukimbia swali kwa kujifanya et umedharauliwa... dharau ipo wapi hapo? eti sio mtu wa hivyo, una mapembe??? Status zako kama zinakuingizia kipato post whatsapp.! usituletee hapa.
Asante mkuu kwa ufafanuzi muruwa, swali bado limesimama palepale inabidi jamii ipate elimu kuhusu majina, je ni majina ya kidini au ya jamii za eneo fulani?
 
Wewe una ushahidi upi kwamba Mkwawa alikuwa na dini kabla hajawa muislamu?

..kwangu mimi mambo ya kiasili ya wahehe, ikiwemo matambiko, ni imani / dini. Ndio maana nasema Mkwawa alikuwa na dini yake ya asili kabla hajasilimu.
 
Inaonekana purpose ya maisha yako ni kutaka kuaminisha uma kwamba TANU ni chama cha waislamu. Na wapigania uhuru wote walikuwa ni waislamu. Lakini yanakufaidisha nini haya?

Tukiwatambua tu kama Watanzania bila kuangalia dini zao kuna shida?
Soma asili ya Tanu iliasisiwa na waislamu kwanza kama movement kilipokuwa ndo wakaanza ingiza wasomi wengine mfano Mwalimu Nyerere, waislamu wa pwani ndio walioleta UHURU wa nchi hii wao waliamua kumpa Mwalimu Nyerere ikiwa na maana ni msomi Ili aweze kuwaongoza wakiwa na lengo la kumdhibiti Mwalimu ambapo ikawa kinyume chake maana Mwalimu akaamua kuviunganisha vyama vyote maana vilikuwa na lengo moja la kudai UHURU ndipo ikazaliwa Tanu.
 
Vito...
Wapo Mkwawa ambao si Waislam hili linafahamika lakini uchifu umebakia kwa ukoo wa Mtwa Abdallah Mkwawa.

Ingia Google utaisoma historia hiyo tena kutoka vyanzo vya kuaminika.

Fika Kalenga Mkwawa Museum utajifunza mengi.
Hivi mzee Adam Sapi Mkwawa alikuwa ni Muislamu au Mkristo.
Kama alikuwa Muislamu nini ajabu kwa baba yake kuwa Muislamu.
 
Kuandika hati ya Kiarabu haimfanyi mtu kuwa Muislam, maana hiyo ni lugha tu ya mawasiliano wala haina attachment na dini yoyote. Ndiyo maana hata magazeti ya Michezo na Biashara huandikwa kwa lugha hiyo pia ili kuifikia hadhira iliyokusudiwa kupashwa habari. Hata Biblia pia yaweza kuandikwa kwa kutumia lugha hiyo ya Kiarabu. Kwahiyo ni hoja dhaifu kusema kwakuwa Mkwawa aliweza kuandika lugha hiyo basi yeye pia alikuwa Muislam.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Mini...
Kuwa Mtwa Mkwawa alikuwa Muislam utaelezwa hapo Mkwawa Museum na utafahamishwa pia ilikuwaje na utapewa jina la aliyemsilimisha.

Aliyemsilimisha ni Abushiri bin Salim Al Harith.
 
ungeanzisha hii mada nyumbani kwako uwe mwenyekiti wa kikao, wewe unataka kujibiwa yako ya wenzio unaruka ruka tu.. umeulizwa swali rahisi mtu anataka kufahamu MOHAMED SAID ni jina la Kiislam au Kiarabu... kama hujui sema hujui na wewe ufahamishwe ila sio kukimbia swali kwa kujifanya et umedharauliwa... dharau ipo wapi hapo? eti sio mtu wa hivyo, una mapembe??? Status zako kama zinakuingizia kipato post whatsapp.! usituletee hapa.
Invisible...
Umeghadhibika.

Lugha yako imekuwa kama pana ugomvi baina yetu ilhali ni mjadala.

Huwa mtu akifika hali hii mimi humwepuka.
 
Hivi mzee Adam Sapi Mkwawa alikuwa ni Muislamu au Mkristo.
Kama alikuwa Muislamu nini ajabu kwa baba yake kuwa Muislamu.
Kalunya,
Mkwawa Museum kuna picha ya kaburi la Mkwawa sehemu iitwayo Mlambalasi alikozikiwa.

Picha ya kaburi lake ukiangalia ni kaburi la Kiislam.

Makaburi mwanae Mkwawa Sapi na kaburi la mkewe Sapi Bi. Johari yapo Kalenga ndani ya Mkwawa Museum yote ni makaburi ya Kiislam.

Angalia picha hapo chini:

Kulia ni kaburi la Mkwawa na chini ni picha ya kaburi la mkewe Sapi Mkwawa Bi. Johari.

1656841655036.png
1656841747665.png
 
mbona kama mnajipa tabu sana! chain ya chifu Mkwawa si bado ipo(wajukuu zake) kwanini msiwaulize wao ndio watakuwa wanajua zaidi kuhusu imani ya babu yao...mwandishi yeye kafanya hivyo kwa kufika eneo husika la historia ya chifu na kutuletea historia hiyo kwanini kabla ya kumbishia mwandishi nanyi mnaobisha msifanye utafiti na kutuletea majibu kama alivyofanya mwandishi
Mawazo mazuri, ubishi usokuwa na jibu kiutafiti unasumbua sana.
 
Mzee kilizi..aliyefungwa kwa tabia zake za hovyo...amejaa udini na chuki zidi ya wakristo..wakati elimu na ufahamu kapewa na shule za kanisa..mjinga huyu..wakupuuzwa hafai hata kusikilizwa.

Anataka kupotosha historia ya nchi na kuondoa umoja wa watanzania kutoka na illusion zake.

Mpotoshaji na mzushi.

#MaendeleoHayanaChama
Jenga hoja zako kitaalamu siyo blaa blaa tu.

Lete ushahidi kama alivyoleta yeye kuwa Mkwawa alikuwa hana dini au ni wa dini nyingine yo yote ile.
 
..Kama Mtwa Mkwawa alikuwa akiandika kwa herufi za Kiarabu hudhani kwamba kuna uwezekano mkubwa alifundishwa dini ya Kiislamu?

..Unaweza ukadai kwamba, kwa nafasi yake ya Mtwa wa Wahehe, huenda Mkwawa alikuwa akiendeleza mambo ya KIMILA, lakini sidhani kama suala hilo lina-disprove the fact kuwa alisilimu.
Umeshawahi kuona au kusikia kuhusu msikiti aliokuwa anaswali mkwawa?
Ni upi au ulikua wapi?
 
Kalunya,
Mkwawa Museum kuna picha ya kaburi la Mkwawa sehemu iitwayo Mlambalasi alikozikiwa.

Picha ya kaburi lake ukiangalia ni kaburi la Kiislam.

Makaburi mwanae Mkwawa Sapi na kaburi la mkewe Sapi Bi. Johari yapo Kalenga ndani ya Mkwawa Museum yote ni makaburi ya Kiislam.

Angalia picha hapo chini:

Kulia ni kaburi la Mkwawa na chini ni picha ya kaburi la mkewe Sapi Mkwawa Bi. Johari.

View attachment 2279830View attachment 2279832
Case closed
 
HOFU HII INASABABISHWA NA NINI KWANINI HAIKUWAPO WAKATI WA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA?

KUSUPA HAPENDEZEWI NA KUSEMA KUWA CHIEF MKWAWA ALIKUWA MUISLAM ANASEMA:

‘’MOHAMED SAID USICHEZE NA HISTORIA YA WAHEHE, WAPO WANAOIJUA VILIVYO!
ETI MKWAWA AJIITE ABDALLAH? HIVI KWELI WEWE UNAMJUA MKWAVINYIKA?

Mohamed Said naandika haya baada ya kuisoma post yako kuhusu Abdallah Mkwawa, nami nina machache ya kukwambia;
1. Tumekunyamazia unapotoa maandishi yako juu ya historia ya TANU na mwelekeo wako wa kutaka kuwaaminisha (wanaokuamini) kwamba TANU kilikuwa chama cha Waislamu, kilianzishwa na Waislamu, kiliiamarishwa na Waislamu…’’

Jibu langu kwake Bwana Kusupa:
''Ndugu yangu Kusupa umehamaki sana.

Najua kwa nini umehamaki na kwa mbali katikati ya mistari unajaribu kunitisha.

Hayo yote niliyoandika nimeyapata Mkwawa Museum Kalenga.
Si kama mie naandika bila ushahidi.

Yuko mtaalamu wa historia ya Mkwawa hapo makumbusho unaweza ukamuuliza.

Nilimuuliza kuhusu Mkwawa kuwa Muislam.

Akaniambia ni kweli.
Nikamuuliza aliupataje?

Akamtaja Abushiri bin Salim Suriyama kutoka Pangani.

Nikamuuliza jina lake la Kiislam.

Akaniambia ni Abdul.
Nikamsahihisha nikamwambia ni Abdallah.

Sithubutu hata kidogo kucheza na historia ya Wahehe wala na ya yeyote awaye yule.

Ikiwa kuandika yale yaliyoandikwa Mkwawa Museum ni "kucheza," basi wanaochezea historia hiyo si mie bali ni wenyewe wenye dhamana ya kuhifadhi historia hii.

Angalia hapo chini imeandikwa Abushiri asili yake ni Tanga.

Ukweli ni kuwa Abushiri ni Mzanzibari na ndiye aliyemfunza Mkwawa kuandika na kusoma kwa hati za Kiarabu.

Barua hii aliyoandika Mtwa Abdallah Mkwawa kwa mkono wake ipo Mkwawa Museum.

Hapo chini inaonyeshwa barua aliyoandikwa na Mtwa Abdallah Mkwawa.

Ndugu zangu haya ndiyo niiyoyakuta Mkwawa Museum Kalenga nikayaandika na haya ndugu zangu ndiyo yaliyomghadhibisha

Bwana Kusupa na kunionya mimi nisicheze na historia ya Wahehe kama ilivyo huko juu.

Huu uoga wa majina ya Kiislam nini maana yake?

Huyo hapo juu chini jina wanalolipenda wanahistoria wetu ni Songea Mbano ingawa ukweli jina lake ni Abdulrauf Songea Mbano.

Ukieleza kuwa hilo jina mnalomwita la Songea Mbano mnalikatiza jina lake ni Abdulrauf Songea Mbano kuna watu wanaghadhibika hawalitaki jina hilo.

Halikadhalika Mkomanile jina lake ni Khadija Mkomanile lakini jina la Khadija hawalipendi.

Kote katika historia ya Vita Vya Maji Maji mashujaa hawa hawatambulishwi kwa majina yao kamili ya Kiislam.

Hii nini maana yake?

View attachment 2277103View attachment 2277106View attachment 2277105View attachment 2277108View attachment 2277107
Hivi kwani Kuna tija gani ku "islamize" harakati za uhuru?
Kama mwanamuziki tajiri bongo ni Nasibu Abdul, Diamond, siku ikiandikwa historia, kwanini isitoshe kuandika tu jina lake, kwanini, iongezwe, alikuwa muislam? kwani huo uislam utakuwa umechangia nini kwenye muziki wake?
Huo uislam wa Mkwawa, uoisaidia vipi harakati za kudai uhuru?
Mandela alikuwa mkristo,lakini kwenye historia hatuandiki mpigania haki na baba wa Taifa, SA Mandela aliyekuwa mkristo pia!! huo ukristo, had nothing to do with fight against apartheid.
Hebu weka mchango wa uislam kama dini, au taasisi kwenye kudai uhuru.
Siku ikiandikwa historia ya huduma za jamii bongo,afya na Elimu, ukristo umechangia sana, sio kwa kuwa na waalimu wenye majina ya kikristo! la hasha kwa kujenga miundo mbinu, shule, hospitari, nk,
Je uislam ndio ulitengeneza mikuki, bunduki wakati wa vita ya majimaji?
 
Kwahili Mzee wangu hapa umepotoka, mimi kijijini kwetu kwa wazee wangu kuna makaburi kama haya na hawaujui uislamu hata chembe.

Makaburi mengi ni ya hivi makaburi yenye misalaba ni ya miaka baada ya uhuru watu walipoanza kupokea dini ya wamisionari.

Kama haya makaburi ndio ushahidi wa Mkwawa alikuwa dini gani basi nenda Musoma utasema wote ni waislamu utayakuta makaburi kama haya na ukifanya utafiti utagunduwa hata baba yake Nyerere au babu yake kaburi lake ni kama hilo la Mkwawa.
 
..kwangu mimi mambo ya kiasili ya wahehe, ikiwemo matambiko, ni imani / dini. Ndio maana nasema Mkwawa alikuwa na dini yake ya asili kabla hajasilimu.
Hawa watu wa dini za Abraham Waislamu na Wakristo hawaamini kama kuna dini nje ya hizo, nje ya Abraham religion wanakuita mpagani, sasa hakuna kusilimu kwa mpagani.
 
Umeshawahi kuona au kusikia kuhusu msikiti aliokuwa anaswali mkwawa?
Ni upi au ulikua wapi?
Daudi...
Nimefika Kalenga njiani nikaonyeshwa kichuguu ambacho Mtwa Mkwawa alikuwa akisimama kuhutubia watu wake.

Miaka ile kilikuwa kirefu hivi sasa kimeliwa na mvua nk. ni kifupi.

Hapo Museum nikaelezwa kuwa ndipo ilipokuwa nyumba yake lakini haikuweza kuhifadhiwa kwa kuwa ujenzi wa nyumba ile ulikuwa nyasi udongo na miti.

Nje uwanjani nyumbani palipokuwa kwa Mkwawa nilionyeshwa mabaki ya ngome iliyokuwa inapita ukuta wa urefu mita 12 na upana mita tatu.

Ngome hii ndiyo inayotenganisha Kalenga na Tosamaganga.

Wajerumani walishambulia ngome hii kutokea hapo.

Leo hiyo sehemu limejengwa kanisa kubwa.

Huu ukuta ulipigwa mabomu na kubomolewa kabisa na Wajerumani katika mapambano ya mwisho na Mkwawa.

Katika hali kama hii nyumba zote zilitekeketea.

Kama kulikuwapo na msikiti usingeweza kubakia.

Lakini hapo Kalenga nimesikia adhana kujulisha kuwa kuna msikiti.

Picha ya kwanza hapo chini ni kichuguu ambacho Mtwa Mkwawa akitoa hutuba zake.

Picha ya pili ni mabaki ya ukuta wa mita 12 urefu na mita tatu upana.
Screenshot_20220703-142847_Photos.jpg

Screenshot_20220703-143231_Photos.jpg
 
Daudi...
Nimefika Kalenga njiani nikaonyeshwa kichuguu ambacho alikuwa akisimama kuhutubia watu wake.

Miaka ile kilikuwa kirefu hivi sasa kimeliwa na mvua nk. ni kifupi.

Hapo Museum nikaaelezwa kuwa ndipo ilipokuwa nyumba yake lakini haikuweza kuhifadhiwa kwa kuwa ujenzi wa nyumba ile ulikuwa nyasi udongo na miti.

Nje uwanjani nyumbani kwa Mkwawa nilionyeshwa mabaki ya ngome iliyokuwa inapita ukuta wa useful futi 12 na upana futi tatu.

Huu ukuta ulipigwa mabomu na.kubomolewa kabisa na Wajerumani katika mapambano ya mwisho na Mkwawa.

Katika hali kama hii nyumba zote zilitekeketea.

Kama kulikuwapo na msikiti usingeweza kubakia.

Lakini hapo Kalenga nimesikia adhana kujulisha kuwa kuna msikiti.
Mzee wangu hapa umetowa tu maelezo ya safari yako ya Kalenga lakini haujajibu swali.

Sasa hivi ukienda Butiama ambako ni ardhi ya Zanaki kuna msikiti mkubwa tu na adhana utaisikia.

Ziko taasisi za kutoka nje za kiislamu zimejitolea ujenzi wa misikiti sehemu yoyote ili mradi uwaoneshe kiwanja tu.
 
Mzee wangu hapa umetowa tu maelezo ya safari yako ya Kalenga lakini haujajibu swali.

Sasa hivi ukienda Butiama ambako ni ardhi ya Zanaki kuna msikiti mkubwa tu na adhana utaisikia.

Ziko taasisi za kutoka nje za kiislamu zimejitolea ujenzi wa misikiti sehemu yoyote ili mradi uwaoneshe kiwanja tu.
Matola,
Umeniuliza kama nimeona msikiti aliokuwa anasali Mkwawa na jibu langu ndilo hilo kuwa hapo Kalenga hakuna chochote kilichobaki si nyumba ya Mkwawa wala ngome yake.
 
Back
Top Bottom