Si kweli, Musoma jamii za kiislamu au uislamu uliingia lini?
Nenda kule utakuta kina Juma wengi tu, Abdala, Musa wanaita Msa.
Kuna jamii ilipendaga tu majina kama kizazi chetu cha sasa kinavyopenda kuiga majina ya uzungu uzungu.
Siku hizi watoto wa kiislamu wengi tu wanapewa majina ya Dayana, Sasha, Natasha ili mradi kutaka uzungu uzungu tu na majina haya so ya kiislamu wala si ya kikristo, ila wenye hayo majina wana dini zao.
Mimi napenda Sana na najisikia fahari kumuita na kumtamka Sheikh Mazinge, Sheikh Ponda, Sheikh Mataka, Sheikh Gologosi, hivi hapo hao masheikh wetu kwa kuitwa hivyo kwa majina yao ya asili, je wamepotezs Usheikh wao na uislamu wao?
Lakini hali ni tofauti kwa Mzee wetu Mohamed Said hata majina yake ya asili hayataki ila majina yakiarabu yeye ndio yanampa fahari.
Licha ya heshima kubwa aliyonayo Mzee wetu haya nayo ni mapungufu yake makubwa na mbaya zaidi huwa hawezi kukuelewa kwa lolote juu ya kile anachokiamini lakini wakati huohuo akitaka wengine nao wasiamini wanachokiamini na ndio mwisho wa siku Mzee wetu huishia kwenye muslim movement Propagandist au kama Modern Mujahedeen fulani tu hivi mwenye cover ya mwanahistoria.