Hofu hii inasababishwa na nini na kwanini haikuwapo wakati wa kupigania uhuru?

Kuna mtu anaitwa juma na mwingine maulid lakin ni wakristo unavyosema huwez ni sheria ipi inazuia mtu kuitwa abdalah na hawez kuwa mkristo acha upotoshaji

..ukiona hivyo ujue mhusika anatokea ktk jamii ambayo ilifikiwa na dini ya Kiislamu kabla ya dini ya Kikristo.
 
Kuna mtu anaitwa juma na mwingine maulid lakin ni wakristo unavyosema huwez ni sheria ipi inazuia mtu kuitwa abdalah na hawez kuwa mkristo acha upotoshaji
Juma si neno tu la kiarabu, wapo pia watu wanaitwa jumanne waisilamu na Wakristo, kuna majina ya kiisilamu na Kiarabu Juma ni la kiarabu.

Mfano nakupa majina wa Waarabu Wakristo, Feirouz (feruzi), Salim, warda, walid etc haya ni majina ambayo kwetu mtu akiitwa Utasema ni muisilamu ila uhalisia ni majina ya kiarabu.

Ila Ukiona neno Abdul then linafuatiwa na jina La mwenyezi Mungu hilo ni jina la kiisilamu, hutakuta mkristo Muarabu anaitwa hivyo. Iwe Abdul Rahman, Abdullah, Abdul Malik, Abdul Salam, AbdulAziz etc.

SSababu kwenye uisilamu Tunaamini ukishakua muisilamu una Submit to Allah na neno Abd linamaanisha Mja hivyo tunaanza na hilo neno kisha tunaweka Moja wapo ya majina 99 ya mungu.

Kama vile ambavyo jina Baptista ama Bautista ni exclusive la kikristo, wapo waisilamu wanaitwa Daniel, Moses etc ila Baptista ni exclusive la Kikristo MAANA linaongelea dini ubatizaji.
 
Thanks for this useful post.
 
..ukiona hivyo ujue mhusika anatokea ktk jamii ambayo ilifikiwa na dini ya Kiislamu kabla ya dini ya Kikristo.
Si kweli, Musoma jamii za kiislamu au uislamu uliingia lini?

Nenda kule utakuta kina Juma wengi tu, Abdala, Musa wanaita Msa.

Kuna jamii ilipendaga tu majina kama kizazi chetu cha sasa kinavyopenda kuiga majina ya uzungu uzungu.

Siku hizi watoto wa kiislamu wengi tu wanapewa majina ya Dayana, Sasha, Natasha ili mradi kutaka uzungu uzungu tu na majina haya so ya kiislamu wala si ya kikristo, ila wenye hayo majina wana dini zao.

Mimi napenda Sana na najisikia fahari kumuita na kumtamka Sheikh Mazinge, Sheikh Ponda, Sheikh Mataka, Sheikh Gologosi, hivi hapo hao masheikh wetu kwa kuitwa hivyo kwa majina yao ya asili, je wamepotezs Usheikh wao na uislamu wao?

Lakini hali ni tofauti kwa Mzee wetu Mohamed Said hata majina yake ya asili hayataki ila majina yakiarabu yeye ndio yanampa fahari.

Licha ya heshima kubwa aliyonayo Mzee wetu haya nayo ni mapungufu yake makubwa na mbaya zaidi huwa hawezi kukuelewa kwa lolote juu ya kile anachokiamini lakini wakati huohuo akitaka wengine nao wasiamini wanachokiamini na ndio mwisho wa siku Mzee wetu huishia kwenye muslim movement Propagandist au kama Modern Mujahedeen fulani tu hivi mwenye cover ya mwanahistoria.
 
Matola,
Nazungumza kuhusu historia iliyopotoshwa na mimi nikaja kuiweka sawa.

Huu ndiyo mjadala wetu hapa.
Je nimesema kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…