Hofu ya Corona: Rais Magufuli asitisha mbio za Mwenge 2020. Fedha kupelekwa ktk maandalizi ya kupambana na Corona

Hofu ya Corona: Rais Magufuli asitisha mbio za Mwenge 2020. Fedha kupelekwa ktk maandalizi ya kupambana na Corona

Nilikuwa kwenye kijiwe cha magazeti, mzee mmoja akasema wakimbize tu mwenge, corona itatupita..
Mwenge ni kitu muhimu na kinaleta mwanga kwenye "Giza" kama kuna mshauri amfikishie ujumbe
sikumuelewa,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye mazindiko na makafara kuna roho huwa zinaumbwa na kumbuka roho hazifi
Sasa kama masharti alipewa marehemu na alishakufa tunaendelea kukimbiza mwenge wa nini? Kama adhabu ya kukiuka hilo iko tied na marehemu sidhani kama kuna lolote baya litatokea endapo mbio zake zikisitishwa.

Jr[emoji769]
 
Nilikuwa kwenye kijiwe cha magazeti, mzee mmoja akasema wakimbize tu mwenge, corona itatupita..
Mwenge ni kitu muhimu na kinaleta mwanga kwenye "Giza" kama kuna mshauri amfikishie ujumbe
sikumuelewa,

Sent using Jamii Forums mobile app
Forojo Ganze ambaye alikuwa ni mmoja kati ya wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya uhuru mjini Bagamoyo mkoani Pwani.

Forojo Ganze aliyezaliwa mwaka 1902 alifuatana na wazee wengine kwenda kwenye zindiko Bagamoyo ili Mwalimu Julius Nyerere aweze kutawala vema.

Wazee hao na miaka yao ya kuzaliwa kwenye mabano ni Mzee Ramadhan (1920), Ally Tarazo (1929), Komwe wa Komwe (1918) na Shehe Yahya Hussein (1925).

Wazee hao walipewa kazi hiyo na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam enzi hizo kuhakikisha rais aliye madarakani hapingwi na mtu yeyote, zindiko hilo lilifanyika Bagamoyo katika moja ya mashimo yanayopatikana wilayani hapo na baadaye Mwalimu Nyerere alipelekwa Bagamoyo, akachinjwa mbuzi na Nyerere akaambiwa atambuke (aruke damu) baada ya kutokula kutwa nzima, jambo ambalo aliwahi kukiri hadharani katika moja ya hotuba zake.

Jr[emoji769]
 
Mshana ,sio wote tunamfahamu Forojo...namna ulivoandika Ni Kama vile wote tunamjua...hebu tudondlee. Huyu Ni Nani,kulikuwa na Nini Hadi akatoa utabiri huu
Ipo siri kubwa kuhusu Mwenge wa Uhuru ambao hukimbizwa nchi nzima. Wapo wanaodhani kwamba aliyeleta mabadiliko katika nchi kwa kuanzishwa kwa mwenge huo ni Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere lakini kumbe siyo kwa mujibu wa taarifa hii.

Mnajimu maarufu ambaye sasa ni marehemu, Sheikh Yahya Hussein aliwahi kusema na ikaandikwa kwamba mvumbuzi wa wazo la kuwa na Mwenge wa Uhuru ni Forojo Ganze ambaye alikuwa ni mmoja kati ya wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya uhuru mjini Bagamoyo mkoani Pwani.

Forojo Ganze aliyezaliwa mwaka 1902 alifuatana na wazee wengine kwenda kwenye zindiko Bagamoyo ili Mwalimu Julius Nyerere aweze kutawala vema.

Wazee hao na miaka yao ya kuzaliwa kwenye mabano ni Mzee Ramadhan (1920), Ally Tarazo (1929), Komwe wa Komwe (1918) na Shehe Yahya Hussein (1925).

Wazee hao walipewa kazi hiyo na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam enzi hizo kuhakikisha rais aliye madarakani hapingwi na mtu yeyote, zindiko hilo lilifanyika Bagamoyo katika moja ya mashimo yanayopatikana wilayani hapo na baadaye Mwalimu Nyerere alipelekwa Bagamoyo, akachinjwa mbuzi na Nyerere akaambiwa atambuke (aruke damu) baada ya kutokula kutwa nzima, jambo ambalo aliwahi kukiri hadharani katika moja ya hotuba zake.

Sheikh Yahya Hussein alisema hata hivyo, katika mashimo yale Forojo Ganze ndiye mtu pekee aliyeingia katika moja ya shimo kwa ajili ya kuuliza mizimu na aliwaacha wenzake nje wakimngoja ili kujua atakuja na jibu gani ili wakampatie rais na wazee wa Dar es Salaam.
Kilichoshangaza, alisema ni mtu huyo kuingia shimoni na kukaa siku kadhaa na alipotoka alikuwa hoi hajiwezi akiwa kama mtu aliyepigwa.

“Tulimchukua akiwa hoi hadi Ikulu Dar es Salaam na tulimfikisha mbele ya Mwalimu Nyerere na akatamka maneno yanayotumika au yanayohusu Mwenge wa Uhuru kwa Kiswahili kisha akanyoosha juu mkono wake wa kulia ambao tayari ulikuwa umeandikwa namba hii 115, kisha akakata roho,” alisema Sheikh Yahya.

Akinukuu maneno hayo Sheikh Yahya alisema Forojo alimwambia Nyerere:
“Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau.

“Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwalimu Nyerere, Ganze alikata roho na siku chache baadaye Mwalimu Nyerere akayafanyia kazi maneno yake na kuanzisha Mwenge wa Uhuru ambao ulipandishwa Mlima Kilimanjaro na Kapteni Alexander Nyirenda aliyekuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),” alisema Sheikh Yahya.

Hata hivyo, mtaalam huyo wa unajimu alisema kilichowashangaza wengi ni maneno yaliyoongozwa yasemayo “UMULIKE NJE YA MIPAKA YETU ULETE TUMAINI” akahoji ina maana ndani ya nchi tubaki gizani? Sheikh Yahya Hussein alisema anashangazwa kwa nini Forojo Ganze hakutangazwa kama mwanzilishi wa Mwenge wa Uhuru kwani baada ya mazishi ya Forojo, ulianzishwa ambao ulikimbizwa nchi nzima mara tu baada ya uhuru mwaka 1961 na unaendelea kukimbizwa hadi sasa.

Jr[emoji769]
 
Laana isiyo na sababu haimpati mtu, watu waendelee kuombea nchi, ikiwa ni wakati ambao Mungu ameruhusu CCM ipatwe na mabaya basi itapatwa, ikiwa yeye hajaruhusu basi haitatokea.

Kikubwa uovu wa nchi umeondolewa kwa sasa, ashukuriwe Mungu aliyeumba mbingu na nchi, tuzidi kuombea Taifa letu.

Kwahiyo CCM kuondoshwa madarakani ni kupatwa na mabaya..?
 
Back
Top Bottom