Uchaguzi 2020 Hoja tatu ni kwanini wapinzani hawatoshi kwenye Uchaguzi huu

Lissu is strong candidate ana fit kila mahali ndugu,sasa hivi mmebanwa pabaya..no Policcm no what..Lissu hamumuibiii kura...very interesting Election..cant wait.
 
Watoto wa hao wa Nanyamba na Kyabakari wanasoma bure ili siku moja wapate elimu kubwa ya kuweza kuzipanda mara kwa mara hizo ndege wakienda Ulaya kwa ajili ya kufanya biashara kubwa.

Akili zinazoangalia mbali huwa zinahoja masuala kwa kina.
Elimu ipi bure unayoizungumzia?Magufuli ndiye kasoma bure,sio hii geresha la mpaka kidato cha nne!
Nyerere alisomesha kuanzia msingi mpaka chuo kikuu bure na JPM ni mnufaika wa hilo!
Badala ya kuwekeza kwenye kilimo na Elimu ya juu,mnawekeza pesa nyingi kwenye vitu vya kuonekana kama ndege!Mbaya zaidi hamtaki hata kukaguliwa mnapofanya hayo manunuzi!Kuna jambo hapo!

Ethiopia wamewekeza sana kwenye ndege,ila wananchi wao kutwa kujipakia kwenye makontena kwenda kufia mbele ya safari kutafuta unafuu wa maisha!Huko ndiko tunataka kwenda!
 
Ethiopia na Tanzania zina historia tofauti kabisa, hazifanani na hazitakuja kufanana.

Faida ya ndege wenye kuzijua ni wenye biashara za kimataifa wewe kama unafanya biashara za kutumia guta na mikokoteni endelea kujadili mambo ya ndani ya uwezo wako.

Kilimo na elimu ya juu ni sekta zinazofanyiwa kazi na pesa za kuzishughulikia sekta hizo zipo.
 
Ningefurahi kujifunza kutoka kwake na kwa wengine. Mfano, katika hayo niliyoyataja, Kuna jambo lolote la uongo?
Kama hakuna wahusika wajirekebishe. Tunataka Upinzani wenye afya
Wewe una afya?
 
Pesa ziko wapi wakati bajeti hata 40 % haikufika huku wizara ya ujenzi ikipata 228% ya bajeti iliyoombwa na bunge?
Wafanyabiashara hawakuwahi kukwama kwa sababu ya ndege kwani kuna mashirika mengi tu yana operate,usafiri wa anga haukuwa changamoto kwa wafanyabiashara!Watu tumesafiri sana tu na mashirika ya ndege ya kimataifa!
Tunaweka vipaumbele kwenye vitu ambavyo havigusi maisha ya watanzania wengi!Basi tungebalance,ndio maana watu wanalalamika mzunguko wa fedha nchini kushuka,hii ni kutokana na fedha nyingi kwenda kwenye makampuni ya nje kwa ajili ya ndege,SGR,Flyovers na Stiglers!Yaani hakuna uwiano mzuri wa miradi ya maendeleo na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja kwa kuweka mzunguko mzuri wa fedha!
Tatizo lenu mnajitia upofu na hamtaki kusikia huu ukweli!
 
Inachekesha kuona unabeza kila jema. Kipindi cha Nyerere tulikuwa wangapi halafu Sasa hivi tuko wangapi?
Bilioni 23 y mwei kwaajili ya elimu bila malipo sio dogo. Idadi kubwa ya wanafunzi Sasa wako shuleni. Mikopo ya elimu ya juu imeongezwa.

Watanzania wanajua
 
Lissu is strong candidate ana fit kila mahali ndugu,sasa hivi mmebanwa pabaya..no Policcm no what..Lissu hamumuibiii kura...very interesting Election..cant wait.
Rebeca, what a beautiful name. It's sad ur candidate is not a right choice kwa watanzania.
 
Mkuu ni wabunge wa upinzani waliokuwa wakiikejeli serikali ya Kikwete kwa kutokuwa na shirika la ndege la taifa leo watu wamegeuka!!.

Miradi mikubwa unaweza kuahirisha kuifanya leo lakini sio milele yote. Ipo siku utakuja kuiona umuhimu wake.

Huwezi kukwepa umeme wa uhakika,huwezi kuikwepa treni ya kisasa.

Hakuna namna ya uwepo wa serikali yenye kuweza kumfurahisha kila mtu kila wakati.
 
Hiyo bil 23 mara miezi 12 haijafika hela ya kununua boeing dreamliner moja!So bado ni ndogo sana!
Watu wanaingia darasa la kwanza milion na ushee,wanufaika wa mkopo ni chini ya laki na nusu,watu wangapi wanaishia hapo katikati?
Elimu,kilimo sio kipaumbele cha serikali ya CCM!
Ni wakati muafaka wapumzishwe tuweke damu mpya!
 
Umekataa kuelewa. Utasubiri Sana
 
Tunasema kila kitu kifanywe kwa wakati na kwa kiasi ili kubalance!Hata wewe nyumbani kwako huwezi walisha watoto wako ugali maharage kila siku ili ununue gari,ujenge nyumba nzuri!Lazima utapangilia uanze kujenga au ununue gari lakini wakati huo huo familia isitaabike,wale vizuri!
Ndio hivyo hivyo,pesa unapeleka kwenye miradi kubwa bila uwiano sahihi!Mbaya zaidi makampuni yanakula hizi pesa ni ya nje!Mzunguko wa ndani wa fedha unaathirika pakubwa!Hata Kikwete alijenga barabara na madaraja!Lakini aliweza kubalance walau mzunguko wa ndani ulikuwa wa kuridhisha!Sio kwamba alishindwa kukopa na kufanya yote kwa pamoja,ila kila kitu kwa hatua!
Huyu JPM wala hajali,ni yeye na miundombinu!Ndio maana nasema hata Ethiopia kuna miundombinu bora sana kuliko hapa kwetu,ila wananchi wake wengi ni mafukara!Kupanga ni kuchagua!
Binafsi yangu naona JPM apumzishwe kwa sasa!Ameshafikia kilele cha uwezo wake na tumeuona!
 
Mkuu pole sana kwa maumivu ya ndani ya nafsi.

Ipo siku yanayofanywa sasa hivi yataonekana faida zake. Subira huvuta heri.
 
Mkuu pole sana kwa maumivu ya ndani ya nafsi.

Ipo siku yanayofanywa sasa hivi yataonekana faida zake. Subira huvuta heri.
Mkiishiwa hoja ndio huwa mnakuwa hivi!Nafsi yangu haina hayo maumivu unayoyadhania!Huenda nikawa na maisha mazuri kuliko hata wewe lakini hilo halinifanyi niwe kondoo wa nyama!
Tujikite kwenye hoja badala ya personal attacks!
 
Mkiishiwa hoja ndio huwa mnakuwa hivi!Nafsi yangu haina hayo maumivu unayoyadhania!Huenda nikawa na maisha mazuri kuliko hata wewe lakini hilo halinifanyi niwe kondoo wa nyama!
Tujikite kwenye hoja badala ya personal attacks!
Ndege zinanunuliwa Madawa yapo mahospitalini na nchi inakwenda vyema kabisa.

Hakuna anayeishiwa hoja mkuu. Kazi inaendelea.

Kikwete alikopa sana na pakawa na deni kubwa la ndani na wasio na shukrani wala heshima kina Mnyika wakamuita dhaifu.

Raid hawezi wala hapaswi kumridhisha kila mtu yeye anabaki kutimiza yote anayoagizwa na ilani kuyatimiza.
 
Ndege zinanunuliwa Madawa yapo mahospitalini na nchi inakwenda vyema kabisa.

Hakuna anayeishiwa hoja mkuu. Kazi inaendelea.
Sio mbaya maana uelewa wako uko limited,binafsi watu kama wewe huwa siwakatii tamaa!Tutaendelea kuelimishana kidogo kidogo juu ya masuala haya kadri muda utakavyoruhusu!
Swali dogo tu,taarifa ya 2019 ya mabank Tz ilionesha kuwa uwezo wa watu kukopa na kurejesha mikopo umeshuka sana!Kwa akili yako unadhani ni kwa nini?
 
Tumia lugha za kistaarabu pia dhibiti hasira yako unapokuwa kwenye mijadala ya JF.

Uwezo wa kukopa na kurejesha ni masuala ya muda tu.

Nchi inafunguka kwa ujumla wake na kadri miundo mbinu inavyosambaa ndivyo fursa
zinavyofunguka.

Ukitazama shida za maisha ya mijini unaweza kudhani maisha ni ya humu mijini tu kumbe Tanzania ni mpaka huko vijijini.
 
Delete ccm Oct 28
 
Rebeca, what a beautiful name. It's sad ur candidate is not a right choice kwa watanzania.

He is, Kilimo,Afya,Elimu...kasome tena ilani yao...he has got vision, has got pragmatic approach to our problems,Magufuli hana vision,na matatizo yetu watanzania yale common hayajui, A+B might be C but how do you derive C??,one will use this approach and other will use another method,which is more quick and efficient. Mimi sio kwamba simpendi Magu ila hizo ndege zinatosha yaani alivyosema ataongeza mi ndege yake ambayo hamna tija zaidi ya pride yake,ndio nikaona huyu si mwenzetu.....yaani watanzania wateseke tena miaka mitano TENA,kisa mkuu wa CHATO ananunua ndege nyingine...Kwa kweli hapana!!!...na aache kuita wenzake mafisadi...wakati yeye hatuelewi ile Trillion 1.5 sijui kaiminyia wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…