Uchaguzi 2020 Hoja tatu ni kwanini wapinzani hawatoshi kwenye Uchaguzi huu

Hesabu hiyo rahis sana, moja tutazarisha Ajira kwenye tren ya mwendo kazi, titazalisha viwandani baada ya kupata umeme wa uhakika kule rufiji, kwenye meri kubwa ya mizigo ziwa Victoria, na kadhalika
 
Tumeshamalizana na mkuu Ben. Tumeelewana
 
Hoja pumba kabisa. Asilimia kubwa ya majibu yanapatikana katika mahojiano ya TL na ITV jana. Kaisikilize.
Mkuu, zile dakika 45 za Mh. T.A. Lissu katika kipindi cha Dakika 45 cha ITV,unaweza kuombea mkopo JPMorgan Chase & Co au Wells Fargo & Co na ukapewa bila masharti.
Pia unaweza kuandikia thesis na kupatia PhD chini ya muda uliopangwa katika vyuo vikuu vinavyotoa elimu bora,sio vinavyotoa vyeti.
 
Residenturaaaaaaaaaaa
 
Ukiona mtu hamweliewi lisu au Chadema maana kuna ccm b,c,d n.k ujue huyo mtu bongo yake kuna sehemu ipo na shida
 
Upumbavu ni kipaji.
Na CCM ya sasa upumbavu ni mtaji.
Wewe ni nani wa kuwasemea Watanzania kuwa mgombea wa Rebeca 83 sio chaguo sahihi la Watanzania?
Residentura ndugu yangu. Zibeni kwanza hilo tundu lenu kwa kuweka mlango imara dhidi ya hasira, wivu, visasi na jazba. Sisi tutawasaidia kuwapa "Makufuli" imara kabisa.
 
Kwakifupi kuungana wapinzani kuna mitego ambayo CCM wameiweka hawatakiwi watumie akili za kuvukia barabara kama wewe unavyo lazimisha
 
Safi kijana, upo vizuri kwenye kudadavua hoja sio hao wengine wapo tu kwenye mkumbo.
 
Naona umeanza kuongea kitu nilichokuwa nasema ila hujajielewa tu!
Msemo huo Roma ulipaswa umgeukie JPM mwenyewe!Kuendea miradi inayochukua fedha nyingi kwa pupa ndio kunafanya sekta kama ya kilimo inayobeba maisha ya watanzania wengi kuzorota!
Mkuu sekta ya kilimo ilikuwa na madudu mengi na pesa ilikuwa inapelekwa nyingi tu. Mambo yananyooka taratibu lakini itafika siku tutakuwa katika njia sahihi.
 

Fikiria. Unaishi Ubungo; unafanya kazi Posta mjini. Unahitaji USAFIRI kwenda/kurudi kazini kila siku. Mshahara wako ni shilingi laki 2-5. Utanunua gari au kutenga bajeti ya mwendo kasi/daladala kwa mwezi? Ndio maamuzi ya kisera yanavyofikiwa.

Watu wenye akili hatuwezi kujadili umuhimu wa ndege kama vile ambavyo hatuwezi kujadili umuhimu wa gari. Suala ni USAFIRI. Sasa kwa kipato kisichozidi shilingi milioni moja, sitakuwa sahihi kununua gari ili kunipeleka kazini kwa hoja kwamba gari ni kitu muhimu! Gharama za ununuzi, mafuta, matengenezo na maegesho, nk haviwiani na uwezo wangu. Naweza kupanda Uber/taxi mara moja moja ikitokea ulazima sana kama Lissu anavyopanda ndege ASIYOIMILIKI kwenye hiyo picha. Ikitokea CHADEMA wakanunua ndege eti kwa sababu ni muhimu nitawatambua rasmi kama wehu.

Shirika la ndege halifufuliwi kwa serikali kununua ndege kwa pesa (cash) za walipa kodi. Hayo si matumizi sahihi ya pesa za umma. Hii ni biashara inayobidi kufanywa na wawekezaji binafsi. Ikibidi serikali inaweza kuwa m’bia muhimu kwa kuweka hisa zake na usimamizi makini. Halafu, sijawahi kusikia ndege za biashara zikinunuliwa kwa cash. Inaelekea hilo shirika litaendeshewa kwa ruzuku ya serikali maisha yake yote na gharama zake zikiwekwa wazi kutakuwa na mtafutano mkubwa. Brace yourselves.
 
Kwanini mgombea wa ccm hastahili kupewa tena kura zetu?

Sababu za kutompa kura zetu mgombea wa ccm ni hizi zifuatazo.

1. Mauaji ya raia wasio Na hatia,

2. Umeendesha nchi kikabila na kikanda,

3. Umeshiriki katika ufisadi wa kununua ndege nk kama sio kweli tupe mikataba ya ununuzi.

4. Umewatesa sana waliokukosoa mfano hai TUNDU LISU na MDUDE CHADEMA.

5. Kutoa ajira kwa kupendelea wanaccm wenzake.

6. Kuwavunjia nyumba wakazi wa mbezi kinyume na sheria za nchi.

7. Kuuza nyumba za serikali kiholela tena kwa watu ambao hawakuwa watumishi wa serikali wakati zinauzwa.
 
Mkuu sekta ya kilimo ilikuwa na madudu mengi na pesa ilikuwa inapelekwa nyingi tu. Mambo yananyooka taratibu lakini itafika siku tutakuwa katika njia sahihi.
Miaka mitano mmeshindwa kushughulikia hayo unayoita madudu,tuwaeleweje?Sasa unasema bado mnashughulikia madudu,mpaka lini?Shame!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…