Hoja: Utaratibu wa Mahari unatakiwa ufutwe, jamii ibadilike...!!

Hoja: Utaratibu wa Mahari unatakiwa ufutwe, jamii ibadilike...!!

Zamani pia vijana wanaume hawakuwa wanashinda vijiweni na mitandaoni kukodolea macho makalio ya wanawake, ku comment na ku like clips na picha zao na kuwafuata DM.
Hivyo ulivyo vitaja vinaondoa usichana wa binti? Kwani mwanaume akilike na kucomment kunaondoa usichana ya binti?

Kuna wengine riziki zao zipo vijiweni mfano dalali, mitandao wengine wanashinda ila wanalipwa ni contents creator.
 
Heri ya Sabato, poleni na mfungo ndugu zetu waislam na wakristo mnaotimiza agizo hili la kiimani.

Nimeamua kudandia treni ya wanaokataa mambo ya mahari kwa dunia ya sasa, hasa barani Afrika ambapo kwa asilimia kubwa ndipo haya mambo hufanyika

Dunia ambayo mwanamke amekuwa huru sana, anaweza kuamua namna anavyotaka maisha yake yawe bila upande wowote kujali/kuingilia.
●Sio dunia ya kulipana pesa/mali kwa ajili ya kumuoa na kuishi nae tena.
●Sio dunia ya kuamuliwa nani utamuoa au utaolewa nae.
● Sio dunia ya kuambiwa ukajenge nje ya boma la wazazi tena, SIO.
● Ni dunia ya kukutana wawili na kuamua hatma ya maisha yenu bila kuingiliwa na mtu yoyote.

Dunia ya namna hii inatakiwa impunguzie mwanaume mzigo, hasa kwenye mambo ya lobola, mahari, dowry.
●Uhuru uliopitiliza kwa mwanamke umekuja na athari hasi, anaweza kuwa na msururu wa wanaume na hakuna anayehoji.
●Anaweza kuamua nani wa kumuoa na hakuna mtu wa kupinga.
●Kwa nini ulipe gharama kubwa kwa kitu ambacho kiimani wewe sio mmliki? Mtu alishamalizana na wanaume kumi+, mmekutana tu for the sake of establishing a society, kwa nini uwe obliged kutoa mapesa ili tu uishi nae?

Wanawake wa sasa wengi ni viwembe, haya mambo tuliyazoea miaka hiyo kwa vijana wa kiume, ila kwa sasa mdada anaweza kuwa na wanaume hata watano kwa wakati mmoja na wala hajali. Mtu wa namna hiyo akikutana na mwanaume kwa ajili ya kutulia(settling) kuna haja gani ya kulipa dowry kama sio kumdhulumu huyo kijana.

Jamii inatakiwa kufikiri mara mbili, tumeamua kuiga tamaduni za wazungu huko, basi na hii iingizwe taratibu kwenye jamii zetu.

Tuachane na hizi mambo.
Happy day y'all!!
Kimsingi tulipokea sera ya usawa wa kijinsia bila kuifanyia maandalizi. Mwanzoni haikuonekana shida lakini kwa sababu hapakua na maandalizi na mbaya zaidi wanawake waliielewa vibaya hii sera, ndio tunaanza kuona nyufa kwenye ustawi wa jamii.

Sio suala la mahari tu, hata sheria ya ndoa inabidi ifumuliwe na kusukwa upya ili kuendana na zama hizi za usawa wa kijinsia.
 
Wanaolipa mahari wanashangaza kweli, hasa mahari kubwa. Mahari iwe ndogo tu kama elfu tano, kumi, elfu hamsini mwisho. Unatoa milioni moja, mbili, tatu, tano za nini? Ni hasara na ni matumizi mabaya ya fedha na rasilimali/mifugo. Mke ni wa kujitwalia bure, hizo mbwembwe za mahari ziwe ni zawadi tu kwa wazazi na isiwe lazima
Mambo ya kushangaza haya, mahari milioni tano. Asante gani hiyo ya kuumiza vijana wetu! Kwa wanawake ambao hata hawakujitunza, sio sawa.

"Helping a boy child"
 
Hakuna tofauti yoyote katika mapenzi kwa mwanaume kati ya mwanamke ambaye hajawahi kabisa kufanya mpenzia na aliyefanya mapenzi na mtu mmoja, wawili, watano au kumi. Tuache ujinga, ni psychology yako tu iliyotokana na utamaduni na dini pamoja na inferiority complex hasa ukiwa masikini kapuku.
Unapotosha
 
Tena hao kuliwa na wachafu ni kugusa tu! Huo upwiru unavyokaba ukaanze kumtafutia mtanashati sio leo..
Wewe na huyo mwenzako uliem-quote hamjaelewa mada. Mtoa mada hajapinga sexual freedom.

Anachotaka kusema utoaji wa mahari ulikua na vigezo vyake ambapo kigezo kimoja wapo ni mwanamke awe bikira, kwa sababu sasa wanawake wana uhuru wa kingono basi utoaji mahari hauna mantiki tena.

Kwahiyo haujakatazwa kuishi promiscous life, isipokua ukichagua maisha hayo maana yake hauna tena uhalali wa kutolewa mahari kulingana na ile maana halisi ya utoaji mahari.
 
Mambo ya kushangaza haya, mahari milioni tano. Asante gani hiyo ya kuumiza vijana wetu! Kwa wanawake ambao hata hawakujitunza, sio sawa.

"Helping a boy child"
Mimi rafiki au ndugu akiniomba niwepo kwenye msafara wa kwenda kulipa mahari kitu cha kwanza nitauliza kama alikutana na huyo mwanamke akiwa bikora. Kama jibu ni hapana, siendi. Maana naona hiyo ni fedhea
 
Mimi rafiki au ndugu akiniomba niwepo kwenye msafara wa kwenda kulipa mahari kitu cha kwanza nitauliza kama alikutana na huyo mwanamke akiwa bikora. Kama jibu ni hapana, siendi. Maana naona hiyo ni fedhea
Ni kama mnaenda kuchumbia mwanamke asiye wake, I get your concern mkuu!!
 
Mind set plus utumwa wa kurithi!

Hisia ya sijaolewa kisa mahari bado wakati anaiishi ndoa na watoto kazaa kabisa!!bahati mbaya mzuka wa kuitoa mahari wakati ushamjua binti ni tatizo sana coz unatoa bila hamu yoyote zaidi ya kuridhisha upande wa ukweni!!

Mahari zilitolewa Kwa wanawali enzi zile na sio Kwa wake za watu ambao tayari upya wao ushabebwa na walaji!!!!
 
Ile walikuwa wanatoa kumchukua binti kutoka kwenye himaya ya baba yake, ambapo anakuwa ameishi maisha yake yote akiwa amejitunza!

Sasa hivi unakuta binti anaishi magetoni kibachela, anvusha na kuvushwa, hana ushamba wowote dunia yote kashaiona.

Kwahiyo mahari inakosa umuhimu.

Mi ni wazamani kidogo pia. Wazamani hawakuwa pure kiasi hicho. Yes, walikua wana aibu kidogo na hawakuwa na exposure na baadhi ya uchafu wa kingono wa sasa uliozagaa mitandaoni na vijana wana u practice. But hata hao wazamani wengi wao waliolewa na ng'ombe nyingi walitolewa wakiwa hawana hizo bikra. In short naunnga mkono hoja kwamba mahari haina maana yeyote ila sioni uhusiano kati ya mahali na usafi wa kimaadili wa binti.
 
Ningeandika mimi huu uzi sipati picha vile ungekusanya kundi lako na kunivalia madela kuja kunishambulia
Tatizo huwa unakosa reasoning ukija na zile red pill content zako.

Hebu jaribu kuandika kwa hoja na na bila ku-generalize kama huyu mzee hapa uone kama hatujachangia bila kukushambulia.
 
Taifa linazalisha vijana wa hovyo wasiopenda kujishughulisha na chochote kutwa kubeti,pombe,dubu na wanawake,matokeo yake hawa kutoa mahari suala la kiutamaduni kabisa wanaona ni mzigo. Vijana tutafute hela ukishapata hela kutoa mahari utaona ni baraka na si mzigo.
Hiv lile suala la kiutamaduni la kuhakikisha mwanamke ni bikira liliishia wapi? Mahari inapaswa kulipwa kwa mwanamke bikira TU.
 
SWALI: Je ulipwaji wa Mahari ina ulazima wowote?..je ni Agizo la kibiblia? Na kama ni hivyo Je! Adamu alitoa mahari kwa nani ili ampate Hawa?


JIBU: Ndoa ya kwanza ilifungishwa na Mungu mwenyewe…Na hakukuhusika mahari wala viapo…Hiyo yote ni kwasababu Hawa hakuwa na Baba wala Mama…

Lakini sasa wake zetu wanao wazazi wao..hatuwatoi ubavuni mwetu kama Adamu alivyompata Hawa..

Hatuna budi kuwatoa kutoka kwa wazazi wao… Na wazazi wao waliwalea na kuwatunza kwa gharama zao.

Hivyo sio vyema kuwaiba kutoka kwa wazazi wao na kuwafanya wetu…Hatuna budi kufuata taratibu za kuwatoa kutoka kwao na kuwaleta kwetu…Na taratibu hizo zinahusisha ulipwaji wa mahari. Ulipwaji wa mahari hakumaanishi kumnunua huyo mwanamke…hapana! Bali kumthaminisha Yule binti kwamba hajaokotwa tu.

Laiti kama tungekuwa tunawapata wake zetu kama Adamu kwamba Mungu anatuletea usingizi na kuwatoa kutoka ubavuni mwetu..hapo kungekuwa hakuna haja ya mahari wala ndoa kanisani..**hapo mahari ina ulazima wowote?..haina ulazima kwasababu wametoka kwetu(kwenye miili yetu kama Adamu)…lakini tulio nao hawajatoka kwetu wametoka kwa wengine… Hivyo ni lazima mtu upitie hatua **za kuposa, na kuposa kuna taratibu zake ikiwemo mahari,

Luka 2:4 “Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;

5 ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba”.

Hivyo hatua hiyo ikishavukwa kinachofuata sasa ni kwenda kanisani…Tulipowatoa! tumewatoa katika jamii..watu wote walikuwa wanajua binti Yule hajaolewa..hivyo binti kwa idhini yake sasa hana budi kwenda kukiri mbele ya umati wa jamii ya watu wake na mbele ya kanisa la Kristo na mbele ya Mungu kwamba amekubali kwa idhini yake mwenyewe kuolewa na kijana huyo..Na kijana naye vivyo hivyo anatamka kwa kukiri..kuwa ushuhuda..Na hapo ndipo Mungu anapoiridhia kuwa ni ndoa takatifu ya kikristo.

Hivyo ndoa na mahari ni mambo ya kimaandiko kabisa hata Bwana wetu Yesu Kristo aliingia gharama ili kututoa katika ulimwengu…Ilimgharimu uhai wake ili tu atupate sisi bibi-arusi wake..

Bwana akubariki.

Je umeithamini gharama Kristo aliyoingia ili akupate wewe?..Damu yake ilimwagika pale msalabani kwaajili yako na yangu..ili sisi tuwe mali yake yeye…tuondoke katika ulimwengu tukaishi naye..Kama hujaokoka unasubiri nini?..siku ile utakuwa mgeni wa nani kule au utakuwa mfano wa wale wanawali wapumbavu tunaowasoma katika kitabu cha Mathayo 25?..Uchaguzi ni wako, mlango wa rehema bado upo wazi.
 
JIFUNZE KUELEWA MAANA YA KUOA/KUOLEWA KABLA YA KUINGIA HUKO.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.

Kama wengi wetu tujuavyo, Ndoa ya kwanza ilifungishwa pale Edeni na Mungu mwenyewe. Na ilikuwa ndoa takatifu, iliyobeba msingi na dira ya ndoa nyingine zote zitakazofuata jinsi zinavyopaswa ziwe.

Katika ndoa ile ilihusisha Mtu mume mmoja (Adamu) na mtu mke mmoja (Hawa)..Kwa kupitia wazazi wetu hawa wawili ndio sisi sote tumetokea…ikiwa na maana kuwa ndoa kamili na takatifu inahusisha mume mmoja na mke mmoja…na si Zaidi. Hicho ni kigezo cha kwanza na cha muhimu.

Pia kabla ya ndoa ile kufungishwa, Maisha yalianza na Adamu kwanza, Mungu alimpa Adamu mimea, mashamba ya kulima, makazi na kila kitu, hapo kabla Hawa hajatokea…na Adamu akaanza majukumu yake ya shughuli pale Edeni kabla ya Hawa kutokea…Na Hawa alipotokea alikuwa kama msaidizi tu wa kazi ambayo tayari ilikuwa imeshaanza. Ikiwa na maana kuwa Mwanamume yoyote kabla hajadhamiria kuoa ni lazima angalau awe na mahali pa kujishikiza ili aweze kumhudumia huyo mkewe anayekuja kumwoa…

Na kumbuka Mungu hakumleta Hawa kwaajili ya tamaa za mwili za Adamu, hapana bali alimleta ili awe msaidizi kwake, kwa namna zote, kifikra, na hata katika kazi zake za kimaendeleo Adamu alizokuwa anazifanya…Ikiwa na maana kuwa lengo la kwanza la ndoa sio kukutana kimwili kama inavyochukuliwa sasa na wachache wasio na maarifa ya kutosha.

Hivyo mwanamke jukumu lake kubwa katika ndoa ni kushirikiana na mume wake, na kuyafanya majukumu yote ambayo mume wake angepaswa ayafanye, ikiwemo ya kihuduma na ya kiuchumi, Hawa hakupelekwa kwa Adamu kumtoa Adamu pesa!..bali awe msaidizi….Maana yake kitu ambacho hakijakaa sawa au hakijakamilika mikononi mwa mwanaume, mwanamke anakiweka sawa na kukimalizia.

Na jukumu kubwa Zaidi mwanamume na mwanamke walilopewa ni kujiepusha na Uovu…Na shetani huwa anawatumia wanawake wengi kuharibu ndoa kuliko wanaume..Kama Hawa mzazi wetu wa kwanza angekaa katika nafasi yake na kujiepusha na uovu, leo hii duniani kungekuwa ni paradiso, lakini kwa kuacha majukumu yake ya USAIDIZI na kwenda kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambayo Mungu hakumwagiza matokeo yake ndio yakawa yale…Na hata sasa mwanamke akiacha majukumu yake na kujikita katika ulimwengu huu, katika usengenyaji, umbea, katika kutoa siri za mume wake nje, katika kutomheshimu mume wake, kumdharau, kumdhalilisha, kumwaibisha, kuvaa kikahaba, kuwa mhuni, mlevi,mtu mwenye mizaha na kila aina ya udunia, anajiharibia mwenyewe na anaibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe..

Na Ndoa takatifu ni lazima ihusishe watu wawili wenye Imani moja..Ni kinyume na maandiko kuoa/kuolewa na mtu asiyeamini baada ya wewe kuamini, Kama umeshamwamini Yesu Kristo na uweza wake hupaswi hata kidogo kutafuta kuoa/kuolewa na mtu asiye mkristo. Na ndoa yoyote ya kikristo lazima iwasilishwe na kubarikiwa mbele ya kanisa la Kristo. Sio sahihi kabisa kufunga ndoa za kimila wala za kiserikali baada ya kumwamini Yesu Kristo.

Na ni lazima kulipa mahari kwa ndugu wa mwanamke kabla ya kumwoa, kama huo ndio utaratibu wa familia ya mwanamke, Adamu hakulipa mahari kwasababu mkewe Hawa ,chimbuko lake lilikuwa ubavuni mwake, hakuwa na wazazi wala ndugu…lakini sasa kila mwanamke anao wazazi/ndugu/walezi…Huko ndiko alikolelewa, hakulelewa ubavuni mwako,…kwahiyo ni wajibu kumtoa kwa wazazi wake kwa utaratibu huo maalumu wa kulipa mahari…

Hata Hawa alipotolewa ubavuni mwa Adamu, Bwana Mungu aliparudishia nyama pale palipotolewa ili Maisha ya Adamu yaweze kuendelea, hakuacha shimo pale wala kidonda!…Na hali kadhalika unapomtoa mwanamke kwa wazazi wake ni lazima uzibe pengo uliloliacha pale, na hilo unaliziba angalau kwa mahari, sio unamwiba na kuacha huzuni kule na malalamiko na laana na maumivu.

kama utashindwa kulipa mahari ya kiasi hicho kidogo cha fedha utawezaje kuitunza na kuihudumia familia yako inayokuja huko mbele, ambayo pengine itahitaji matunzo ya gharama nyingi kuliko hizo za mahari??…kama hutaki kutoa mahari, maana yake bado hujaelewa maana ya kuoa, hivyo unapaswa ungoje mpaka utakapoelewa vyema maana ya ndoa ndipo uoe.

Na mwisho biblia inatuambia kuwa wakati tuliobakiwa nao ni mchache sana…wale ambao wameoa na wawe kama hawajaoa…ili muda mwingi tuutumie katika kuutafuta Zaidi ufalme wake na haki yake kwasababu unyakuo upo karibuni, na mbinguni tuendako hakutakuwa na kuoa wala kuolewa, yatakuwa ni mambo mapya huko ambayo ni ya muhimu Zaidi kuliko haya.
 
NIMEASOMA HEADING TU.
Naunga mkono..

KUTOKULIPA MAHARI NI DHAMBI.

USIPOLIPA MAHARI NI DHAMBI KABISA.

KUNA WANAUME WAPO KUZIMU WANAUNGUA NA MOTO KWA SABABU YA DHAMBI YA KUTOKUMALIZIA KULIPA MAHARI WALIYOPANGIWA UKWENI..yani unakuta KALIPA NUSU TU au robo tu akaahidi atamalizia kulipa mahari iliyobaki HALAFU KAPOTEZEA kajikausha kimya ..AU HAJALIPA KABISA...mahari anakaa na mtoto wa mtu

hata kama uliyemuoa hakuwa bikira bado ni sheria kulipa mahari,usipolipa mahari ni dhambi ambayo inaweza kukupelekea ukaishia kuchomwa moto ..motoni kabisa.

JAPO WAHUBIRI HAWAHUBURI HII SANA ILA.. NI MUHIMU KUELEWA..ILI SIKU UKIJIKUTA UKO MOTONI ..kwa dhambi ya kutokumaliza kulipa mahari au kutokulipa kabisa mahari usishangae ..useme nilikuwa sijui kama ni dhambi.

KUTOKULIPA MAHARI NI DHAMBI KABISA KAMA DHAMBI NYINGINE.
 
NIMEASOMA HEADING TU.
Naunga mkono..

KUTOKULIPA MAHARI NI DHAMBI.

USIPOLIPA MAHARI NI DHAMBI KABISA.

KUNA WANAUME WAPO KUZIMU WANAUNGUA NA MOTO KWA SABABU YA DHAMBI YA KUTOKUMALIZIA KULIPA MAHARI WALIYOPANGIWA UKWENI..yani unakuta KALIPA NUSU TU au robo tu akaahidi atamalizia kulipa mahari iliyobaki HALAFU KAPOTEZEA kajikausha kimya ..AU HAJALIPA KABISA...mahari anakaa na mtoto wa mtu

hata kama uliyemuoa hakuwa bikira bado ni sheria kulipa mahari,usipolipa mahari ni dhambi ambayo inaweza kukupelekea ukaishia kuchomwa moto ..motoni kabisa.

JAPO WAHUBIRI HAWAHUBURI HII SANA ILA.. NI MUHIMU KUELEWA..ILI SIKU UKIJIKUTA UKO MOTONI ..kwa dhambi ya kutokumaliza kulipa mahari au kutokulipa kabisa mahari usishangae ..useme nilikuwa sijui kama ni dhambi.

KUTOKULIPA MAHARI NI DHAMBI KABISA KAMA DHAMBI NYINGINE.
Kutokulipa mahari ni dhambi kwa mujibu wa kifungu kipi kwenye Bible?
 
Kutokulipa mahari ni dhambi kwa mujibu wa kifungu kipi kwenye Bible?
Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu,suala la kumchukua mwanamke kutoka kwa wazazi wake na kumfanya awe mke wako lina utaratibu wake ambao unahususha posa,mahari,ndoa makubaliano ya pande zote
Huyu binti unayemuoa humtoi hewani ,unamtoa kutoka kwa wazazi wake kwa kufuata TARATIBU ...usipofuata utaratibu..unakuwa kama UMEMUIBA kuvunja utaratibu ndipo ilipo dhambi..

DHAMBI zilivyondiwa kwenye biblia wakati mwingine inahitaji uelewa mpana zaidi
Kwa mfano usitegemee kuona kitabu cha biblia kimeendika USIVUTE SIGARA NI DHAMBI au usivute shisha au usitumie makokeni ma heroine madawa ya kulevya au usivute gundi...AU USIJIUE mwenyewe.

AU USIPIGE PUNYETO kujichua masterbation..

au usitumie madawa ya uzazi wa mpango ni dhambi..

au nikuulize DHAMBI NI NINI? wewe unaelewa dhambi ni nini?

dhambi sio hizo zilizoandikwa kwenye AMRI 10 PEKEE alizopewa Musa ...dhambi ziko zaidi ya mia 600.

na yote yangeandikwa isingetosha kwa ufafanuzi wa kimoja kimoja yasingetosha kunenea kuyaandika yote.

ILA katika hayo yaliyoandikwa yanajitosheleza yamebeba yote yanayotutosheleza kufahamu..NA TUKIWA NA ROHO MTAKATIFU atatufindisha yeye ROHO wa Mungu atatisaidia kuelewa na kutufundisha na kutuongoza.
 
Back
Top Bottom