#COVID19 Hoja za Askofu Gwajima wameshindwa kuzijibu

a

Acha kuita mazezeta watu wenye akili timamu...kama vipi ww kachanje na muda ndio hakimu wa kweli...tutakuja kujua nani kati yetu atakuwa zombie 5years down the line!
Mkuu Kuna aliyewaita waumini wa Askofu Gwajima mazezeta ndio ironically nikamwambia na hao ni "waumini mazezeta" wa Askofu Gwajima.
 
Lakini dogo, inamaana hairuhusiwi kuipinga chanjo? Kama ni hivyo, kwanini Serikali Yetu Pendwa inasisitiza chanjo ni hiari!? Unafikiri haijui kuwa wengine kama mimi hawapo tayari kuchanjwa? Kama vipi wewe kachanje utukomoe sie tusiotaka kuchanjwa!!
 
Kamsikilizeni NA huyu youtube jamani sio gwajima tu
 
Uyu anatafuta sifa tu, izo hoja zake ni nyepesi mno, alafu si anasemaga anamakanisa nje ya nchi tutaona Kama atakuja kwenda kwenye nchi yao Kama hajapata chanjo, Gwajima atachanja kimia kimia ,nchi jirani nawambieni Kama kweli hajachanja kimia kimia,

GWAJIMA najua anasafili kwenda nje je chanjo ya hepatitis B,c hakuwai pata? Màana zipo chanjo upende usipende utachanja kambla ya kuingia kwenye mataifa ya watu, na Kama ndivyo , kachanja Iyo chanjo alitengeneza kanisani kwake,

Mtu mzima ,tena kiongozi mkubwa wa dini anakua muongo mpaka wajukuu zake wanamshangaa,
 
Kwani chanjo ya hepatitis B ni mRNA?
 
Sehemu ya Taarifa ya Wataalamu iliyochapishwa kwenye tovuti ya Center for Disease Contro and Prevenvion inasema:-
Full report, inapatikana hapa!!

Haya, weka hapa credible source ya hayo uliyosema! Na iwe ni source yenye maelezo ya watalaamu na sio consipiracy theorists ambao hawajafanya utafiti wowote wa kitabibu!!
 
Tangu lini ZWAZWA akawa na hoja? Mbona kachanja chanjo nyingi tu maishani mwake zikiwemo za polio, kifua kikuu, polio etc na hayo maswali yake ya kipuuzi hakuyauliza!??
 
Za kuambiwa changanya na zako
 
Tangu lini ZWAZWA akawa na hoja? Mbona kachanja chanjo nyingi tu maishani mwake zikiwemo za polio, kifua kikuu, polio etc na hayo maswali yake ya kipuuzi hakuyauliza!??
Mzee nenda kachanje Mimi nipo upande wa Gwajima
 
Rev. Bishop Josephat Gwajima anajua haya kuliko wewe na wenzako huko mnavyojua...!!

Ukiachilia mbali molecular biology science ya hizo DNA na RNA na kirusi wa CORONA anavyozaliana na kuushambulia mwili wa host, mwenzako ana elimu ya sayansi bora zaidi [spiritual science] ambayo wenye maarifa ya kidunia pekee kama wewe hawana na hawajui lolote...!!

Kwa sababu hii, ni wazi kuwa ni ngumu kumwelewa Rev. Bishop Josephat Gwajima kwa sababu mnasafiri kwa kutumia masafa [frequency] tofauti...

Mwenzenu anatumia masafa marefu [high frequency] ktk kujenga hoja zake na ninyi mnatumia masafa mafupi [low frequency]....

Kwa hiyo, if this is the case, there's no way tunaweza kukutana wala kupatana. Lazima tu upande mmoja ushindwe spectacularly...!

Na upande huo obviously ni ule unaotegemea akili za kibinadamu ktk ku - argue na kuamua juu ya mambo haya. Upande huo ni huo wenu ninyi mnaomshambulia mtu huyu just for the sake ya kumshambulia tu...
 
Hapo kwenye frequency ndipo anapo wateka akili za mazezeta.

Gwajima awe na frquency kwa theology gani aliyosoma na kwa chuo gani cha theology?

Mtu aliyejitngaza mwenyewe kuwa askofu na kujifanyia mwenyewe mambontofuti na makasisi unasema !!!! Frequently

Maaskofu walio undergo hutua zote za kusimikwa uaskofu baada y kusoma vyuo vyenye ithibati na mitaala ya makasisi akina shoo, mwalasua, rwaichi wamekubali chanjo halafu unaniambia habari ya frquency za gambosh zinazodanganya watu zinafufua watu na misukule wakati hajawahi kufufua hata Panya? Huyu Mungu amekaa kimya watu wanamchezea saana
 
Hoja ya kwanza.

Fomu ya kujaza kukubali kupewa uduma ya afya ni jambo la kawaida sana kwani chochote kinaweza kutokea. Chanjo zote lazima ujaze consent form.

Hoja ya pili: Nani kalazimishwa?

Hoja ya tatu: soma hio link


Hoja ya nne:

Chanjo ni nini? Ukishapata jibu ndio utajua kwanini mda mwingine mtu anahitaji booster shot.
 
Mzee wewe ni mtanzania au mkenya!?
Tumechanjwa chanjo kibao, lini tumejaza fomu!? Usitupotoshe.
 
Hapo kwenye frequency ndipo anapo wateka akili za mazezeta.
Kama hujui na huelewi utajiona umetekwa. Tunaoifahamu lugha hiyo hatuna shida...
Gwajima awe na frquency kwa theology gani aliyosoma na kwa chuo gani cha theology?
Theology halisi na yenye manufaa kwa binadamu haisomewi chuo chochote hapa duniani. Chuo cha Theology yetu ni NENO LA MUNGU na ROHO MTAKATIFU...

Inayosomewa ni ile ya kutafutia heshima na vyeo vya kidini hapa duniani...

Niambie Yesu Kristo alisoma chuo gani cha theology? Sisi tunafuata njia yake, mafundisho take na mfano wa maisha yake...
Mtu aliyejitngaza mwenyewe kuwa askofu na kujifanyia mwenyewe mambontofuti na makasisi unasema !!!! Frequently
Unajua utaratibu wa kanisa lake? Mbona kama umekariri? Utaratibu wa kanisa/dhehebu lako la kumpata Askofu siyo lazima utumiwe na kanisa/dhehebu jingine. Muhimu ni kibali toka kwa Mungu na watu. Anacho kibali hicho...!!
Nisome ktk hoja ya hapo juu na jinsi ya kumpata Askofu wa dhehebu/kanisa fulani.

More over, nasikitika ni kama vile hujui lolote kuhusu nguvu ya Mungu na Neno lake (Biblia). Katika hili ngumu tukaongea na kuelewana kwa sababu kama nilivyosema tunafikiri kwa kutumiwa masafa (frequency) tofauti...!
Huyu Mungu amekaa kimya watu wanamchezea saana
Isije ikawa wewe ndiye unayemchezea na ameamua kukustahi na kukuvumilia ili labda you will sooner or later come into your sense...

Tubu na mwamini Yesu Kristo ili awe Bwana na mwokozi wako. Hii ndiyo njia salama ya kujiokoa na ghadhabu ya Mungu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…