Natoa pongezi kwa msanii namba moja Afrika kwa sasa Diamond Platnumz kwa kununua vyombo vya anga. Biashara yake mpya anayokuja nayo ya Wasafi airlines itafungua milango ya ajira nyingi sana Tanzania na duniani kwa ujumla.
Watu tutaacha kupanda emirates na klm tutaanza kupanda ndege za kijana wa Tandale. Nitoe wito kwa vijana majobless kuanza kuandaa CV badala ya kushinda mnatukana mafanikio ya tajiri huyu mwenye umri kama wenu.
Hii biashara itaenda kuajiri marubani, hostess mpaka mainjinia mlio na madegree. Ili ni somo kwa vijana tuendelee kupambana kuzifikia ndoto zetu na tuheshimu talent. Hakuna kinachoshindikana. Hasira za kuyakosea maisha kuzishushia kwa Diamond wala sio dawa ya kutusogeza kimaisha.
Anafanya vzr,hatuna wivu nae,lakini wapo ma injinia wenye mpunga mrefu,wasafi wanasubili,
Mmiriki wa molel electrical,ndie anaemiriki majengo zilipo ofc za voda na Tigo,ndie mwenye kiwanda Cha kutengeneza nguzo za zege,
Mond utajiri wake ni bilioni 23.3!!
Molel electrical ana mara kumi ya hizo,
Je umemsikia Yule kijana wa Tanzania,asimwe kabunga aliyewekeza bilioni 90+!,kwenye kiwanda Cha madini!!?
Wasomi wapo wengi tu wenye pesa ndefu,
Avumae baharini ni papa,lakini wengine wapo,Umemsikia Fernandes wa NARA?
Je Yule kijana anayemiriki kampuni ya IT,iliyoajiri CEO kutoka Kenya?
Usisahau mmiriki wa huu mtandao,JF,ni msomi sana,Tena injinia,
Kwa kijana kutoka "tandale"kutoka kwenye maisha ni long game,acha kabisa, wako wapi Juma nature,dudu bata,tmk wanaume,Marrow,Mr nice,twenty percent,YP na Ydash,sister P,Rah P,ZeY B,
Ila kwa msomi,unakuwa umepewa ngazi ya kuanzia.