Hongera Mbowe umeshinda mchezo wa kisiasa

Mimi nampongeza sana Mbowe kwa kumsifu Mama Samia kwenye mkutano wa chama chake. Jana ni kwa mara ya kwanza Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani kumsifia mwenyekiti wa chama tawala kwenye jukwaa la chama chake. Mbowe anaungana na hayati Mrema kwenye rekodi za wenyeviti wa upinzani waliowahi kumsifu mwenyekiti wa CCM hadharani. Ikumbukwe kwenye uchaguzi wa 2020, Hayati Lyatonga alimsapoti Hayati Magufuli. Tofauti ya Mbowe ni kuanza kumsapoti Mama Samia kabla ya uchaguzi 2025.
 
9
Mambo yote huwa ayapatikani kwa wakati mmoja, kama kuna juhudi hata kidogo za kutufikisha huko tusizibeze. Tuonyeshe sapoti. Sasa nyie mnaobeza mna taka nini? Njooni na suluhisho sio kubeza tu
Tatizo huwa mnatawaliwa na mihemko! Je, wakati wa JK kwanini ilikwama? Katiba Mpya huwa haitayarishwi na wawania madaraka! Maoni yangu ni kuwa Tusubiri hadi Samia wakati Anang’atuka siyo wakati akitegemea kuwania madaraka!
 
Sasa turudi katika hoja kwanini Mbowe jana kashinda mchezo wa kisiasa?

Wananchi wamejibu hoja hii nzito mjini Musoma leo na tutaendelea kufuatilia ujio huu mpya wa siasa za ushindani wa vyama vya siasa na mapokeo yake nchi nzima wakati CHADEMA ikizunguka nchi kusalimia baada ya kifungo haramu cha kufanya siasa kwa takribani miaka 7 kutenguliwa


22 January 2023
Musoma, Tanzania

LIVE: Mkutano wa CHADEMA Musoma uwanja wa Mkendo


Source : The Chanzo

N.B
TAKWIMU muhimu kuhusu mji wa Musoma mkoani Mara nchini Tanzania :
Idadi ya Watu = 134327 soma zaidi Source : Takwimu
 
Tatizo huwa mnatawaliwa na mihemko! Je, wakati wa JK kwanini ilikwama? Katiba Mpya huwa haitayarishwi na wawania madaraka! Maoni yangu ni kuwa Tusubiri hadi Samia wakati Anang’atuka siyo wakati akitegemea kuwania madaraka!
Kwahiyo ushauri wako unataka kwasasa tukae kimya tusubili mpaka Samia hatakapokuwa hana nia ya kugombea urais?
 
Umeweka vizuri mambo, hongera kwa Chadema na mwenyekiti Mbowe!
 
Mbowe amefundishwa na Magufuli kwa vitendo kuwa dunia ya leo haihitaji siasa za matusi lest utapambana na mkono halisi wa dola. Kongole kwake.
 


Nilisha sema Mbowe yuko strategic. Katiba mpya ndiyo lengo kuu hapa. Kuongelea bei ya mahindi na mchele ni kazi ya wengine.
 
Ukweli hata mimi mbowe sikumuelewa ila kupitia hili bandiko nimemuelewa[emoji120][emoji120]

Hata demu ukiwa unamtaka....... Katika hatua za mwanzo lazima uwe mpole ujifanye fala ili siku za mbele uje umpelekee moto vizuri[emoji1787][emoji1787]
 
Nenda kachukue posho yako kwa Sophia Mjema (Mbowe)
 
Mbowe amesoma hofu ya CCM juu y katiba mpya na kuielewa hofu na kujua namna ya kudeal nayo.

Viongozi wengi wa CCM wanahofia sana hatima yao na maslahi yao baada ya katiba mpya('ya warioba'),.Anachofanya Mbowe ni kutumia diplomatic plus compromised means ili mambo yafanikiwe.

Ndio maana kuna usiri maana jambo kubwa hakikisho la hatima ya viongozi wa CCM na maslahi yao binafsi.

Hili ni kama suala la Mandela na future ya weupe wachache,hawa makaburu wlipokubaliana sirini way forward ya maslahi yao hawakuona tena haja ya kuendelea kumshikiria Mandela ivyo uhuru ukapatikana na Mandela akawa Rais(ndio walichotaka blacks) na weupe wakabakia na nguvu za kiuchumi walizotaka.

Mbowe na baadhi ya viongozi wa upinzani wanaweza kufanikisha katiba mpya na uwepo wa tume huru n kuishia hapo tu,ni jukumu la kizazi kijacho kutumia uwepo wa katiba na tume huru kuiadhibu CCM na makundi maslahi yake kwa kuwaondoa madarakani na kusimamisha zama mpya.

Ikumbukwe kuwa Musa alianzisha safari ya kwenda Kaanani lakini yeye hakufika Kanaani ila Joshua mtu wake wa karibu ndie aliehitimisha safari hiyo.

Hongera CDM na viongozi wake lakini ni jukumu letu sasa kumalizia panapokwama ktk kuleta mabadiliko kmili ya kiutawala na ukombozi kamili wa wengi wasionacho dhidi na wachache walionacho.
 
Kweli !
 
Naunga mkono hoja, wengi wanaopinga maridhiano ni waoga, wanaoendekeza siasa za kuviziana, wanaishi kwa hofu, na kutojiamini,

Mbowe ameshinda mchezo, ametumia uwanja wa maridhiano kupata alichopigania, anastahili kupongezwa, ajabu wapo wahafidhina waliokariri kwao siku zote siasa ni harakati, wanamuona Mbowe amekosea..
 
Najaribu kuelewa ndugu JASUSI,

Bt ilikuwa lazima kutumia kilevi kuzisukuma kete ulizozitaja?
 
Siasa zinabadilika kulingana na mahitaji halisia, kwa kipindi kirefu siasa za kiuana harakati zimeshindikana zaidi ya watu kuumizwa kufungwa na kufilisiwa. Hata Mandela alibadili mfumo wa kukabiliana na makaburu akaanza majadiliano na kisha Nyerere akapinga akisema haamini kama makaburu watabadilika kwa majadiliaon, hakuwaamini lakini ndivyo hivyo majadiliano na diplomasia ilileta uhuru na kufunguliwa jela Mandela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…