Hongera Mbowe umeshinda mchezo wa kisiasa

Very well
 
Watu hatumkosoi kuhusu maridhiano. Tunamkosoa kwa kuwachinjia baharini viongozi wenzake. Alizungumzia zaidi yeye kuambiwa amelamba asali kuliko mafanikio ya maridhiano. Hapo ndipo alipotukwaza wengine.

Amandla...
 
Kumbe hadi CDM kuna chawa? Yericko Nyerere .

Mengine muwe mnaiacha tu yanapita. Ni ngumu sana Mbowe kuendelea kuaminiwa Tena. Nami nahisi Mbowe amechoka na sio yule nilio mzoea. Sasa anatafuta ugali wa wanae kwa njia nyingine anaona njia ya Ikulu ngumu.
 
Uhalisia unakataa. Maridhiano hayo yataidhoofisha CDM na sio kinyume chake.
Kwani wewe Tindo unataka M/Kiti na CHADEMA wafanye nini ili u - appreciate kuwa they are doing fine?

Uko against kila kitu kinachofanywa na CHADEMA chini ya Freeman Mbowe Kwa Sasa Kwa hoja ambazo Mimi hata sioni uzito wake..

Na mara nyingi huwa nafuatilia mtazamo na maoni yako juu ya mwenendo wa CHADEMA chini ya Freeman Mbowe Kwa muda mrefu. You don't appreciate anything bro, why.?

Yaani kuna wakati unatamani viongozi wa chama chini ya M/Kiti Freeman Mbowe na CHADEMA Kwa ujumla siku Moja usikie wakitangaza kutumia njia ya mapambano ya kimwili (physical confrontation) dhidi ya CCM na serikali badala ya hii ya kukaa mezani kuzungumza ili kupata wakitakacho--

Mimi nasema HAPANA!!... Njia hiyo uwazayo wewe haikubaliki kwa Sasa na mpaka kesho.!!

Na ikitokea ikatumika njia hiyo uitakayo, basi tambua kuwa hata wewe hutabaki salama kiasi cha kukaa kwenye Kiti chako ukiposti haya unayoposti Kwa sababu vita au aggressiveness au physical confrontation haijawahi kuwa njia fanisi na salama kupata chochote toka Kwa mpinzani wako zaidi ya hasara na maumivu...!

Kubali kuwa, Freeman Mbowe ni miongoni mwa viongozi bora sana wa vyama vya siasa vilivyo nje ya serikali a.k.a vyama upinzani Tanzania, Afrika na duniani wa miongo hii.

CHADEMA wako vizuri na Wana akili sana na wako kwenye njia sahihi na nakuhakikishia jambo Moja, hiki chama KITAICHUKUA NCHI SIKU MOJA ISIYO MBALI NA KUONGOZA SERIKALI..!!
 
Bt usisahau maridhiano yamesababisha manufaa makubwa Kwa wananchi.

Mauaji ya kutisha hayakuripotiwa.
 
Watu tuna vilema hapa vya kuingia barabarani, labda useme kingine. Kuna watu tulijitoa kuwapigania wakaishia kuunga juhudi, kisha wakahongwa vyeo hivyo hivyo kwa mlango wa uani. Sasa sijui unaongea nini boss.
So sorry.

Bt pasi maridhiano ya Mandela na makaburu, Hadi Leo wangekuwa wanauana.

Wakat mwingine viongozi wajishushe Ili raia wapate manufaa.

The End justifies the means.
 
Mbowe ameshakuwa 'compromised'.
Kama Mbowe ana compromise na mwisho TUNAPATA KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA,

Aendelee na njia hiyo, bt kama wanamuingiza kingi, tumekwisha.

Maana deni la Taifa linazidi kupaa, na pesa wanazoziiba what if wakirudi nazo kuwanunua wapiga kura!!!
 
Hoja zitoke wapi CHADEMA ? Usijitekenye.
 
CHADEMA imesonga mbele ? Kweli wewe hujui kitu kabisa.
 
Kumbe umeshamsoma [emoji1319][emoji1319][emoji1319][emoji1317][emoji1317][emoji1756][emoji1756]

Now ni kujiita kilema, kutafuta huruma, bila ushahidi ili ku- justify kile anachopigania kionekane sahihi[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kwa hiyo maridhiano ya CCM na Chadema na hizo siasa wanazoita za kistaarabu ndio zitawapeleka Chadema ikulu?
Hata kama hawataenda ikulu zitawaondoa kwenye taharuki ya kuwindwa kama sungura.
 
Ila kwenye hiyo clip nilichoona ni kimoja tuu kwamba Mbowe saa uzee unamkaba koo kwa kasi.
Nimeona na yeye anaonge huku una mung'unya mung'unya midomo kama wale wazee vibogoyo..

Ila jamaa kama ni kazi kwa taifa hili lililojaa wapumbavu basi kafanya kazi kubwa sna..Namuheshim na namuombea kwa Mungu kuhusu hilo.

Lastly i love Change but i dnt believe in change through CDM wamepoa sana kwasasa nadhan ile misuko suko haijatuacha salamaa kabisaaa na ccm wanajua fika kwamba wametumaliza
 
Kumbe umeshamsoma [emoji1319][emoji1319][emoji1319][emoji1317][emoji1317][emoji1756][emoji1756]

Now ni kujiita kilema, kutafuta huruma, bila ushahidi ili ku- justify kile anachopigania kionekane sahihi[emoji3][emoji3][emoji3]
TINDO yupo sawa.

Wasiwasi ndio AKILI.

Chama Cha Mapinduzi Si Rahisi kuachia bila KUPINDULIWA,

Tujifunze Zanzibar, Maalim alitumia njia zote za nguvu na ustaarabu bt nn yalikuwa matokeo yake???
 

Kwanza nashukuru kwa kunifuatilia, na kizuri zaidi kutokukubaliana na mtazamo wangu, hasa kuhusu huyo Freeman Mbowe. Napenda kusema naheshimu mtazamo wako kwani hiyo ndiyo afya ya mjadala, na zaidi hiyo ndio demokrasia.

Sasa tuje huko kwa Freeman Mbowe, nasema hivi, mimi ni muumini wa nafasi ya kiongozi wa kuchaguliwa kutokuzidi miaka 10, sasa hili ni kosa langu sio lako. Lakini ni ukweli usioacha shaka kuwa kiongozi akikaa madarakani zaidi ya miaka 10, ubora wake hupungua, na huanza kutawala kwa mizengwe, Mbowe anaangukia kwenye kundi hili. Ukitazama CDM ilipotoka na ilipotakiwa kuwa sasa hasa upande wa miundombinu, kama ofisi hata 1 moja MKOA ni vitu tofauti! Kibaya zaidi anaanza kusema kuna mabilioni yake mengi ameyatumia kwa ajili ya CDM, yaani anaonyesha CDM ni mali yake na wala sio kiongozi.


Kwa kiongozi muwajibikaji, baada ya blunder ya kumpokea Lowassa kushindwa kupata urais, Mbowe alipaswa Kujiuzulu. Ama kama aliona sio sawa, kujiuzulu baada ya kosa lile, basi hakupaswa kugombea uenyekiti tena msimu uliopita. Jambo hili halinipi ruhusa dhamira yangu kukubaliana na mwenendo huo. Hii ni haki yangu ya kidemokrasia, je nakosea kutumia haki yangu ya kidemokrasia kumkataa kiongozi ambaye nina sababu za msingi za kumkataa? Sababu hizi sio lazima ziwe za msingi kwako, lakini kwangu zina msingi, na nitazishikilia.

Huko kwenye maridhiano, kwanza mimi sio muumini wa maridhiano na hao ccm, hilo moja, lakini sipingi wenye kuamini hayo maridhiano. Japo kwa mtazamo wangu, si sahihi Mbowe kwenda mwenyewe kwenye jambo hilo. Naijua tabia ya CCM kwenye maridhiano, na mifano hai ninayo. Hapa ni mjadala mpana.

Nahitimisha kwa kusema, ni sahihi sana Mbowe kukaa pembeni, kwani ameshakaa muda wa kutosha, na sasa anaelekea kushuka chini, ni vyema akakaa pembeni akapisha wengine, labda uniambie kuwa huko CDM hakuna mwingine zaidi yake kwa nafasi ya uenyekiti.
 
Naunga mkono HOJA,

Mbowe anatakiwa apumzike,

Point ya mwisho ndo yenye UKWELI,

Ukimuondoa Mbowe sasa CDM hayupo wa kuvaa VIATU vyake,

Mfumo wa CDM haukuwahi kuwaandaa vijana wake Kwa majukumu ya mkt.

Mbowe aendelee kuwapo, bt awe chini ya UANGALIZI mkali. Naamini JASUSI YERIKO nyererere ananielewa.
 
Upuuzi mtupu,maridhiano kati ya pande 2 hasimu za kisiasa huwa yanatikana na reactions za wanachama husika na sio vinginevyo.

Speech ya Mbowe ukiisikiliza kiumakini umetokana na kukosa support ya Wananchi & Wanachadema katika mapigano ya democracy-hivyo anaona umri unakwenda bora ahangaikie alichokipoteza individuali na sio tena kupigania watu wasio thamini struggle za democracy.
 

Si kweli, kuwa Mbowe akiondoka CDM itakosa mtu. Je akifa ndio mwisho wa CDM?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…