Hongera Mbowe umeshinda mchezo wa kisiasa

Si kweli, kuwa Mbowe akiondoka CDM itakosa mtu. Je akifa ndio mwisho wa CDM?
Kufa ni jambo lingine,

Pale CDM ya sasa mtu wa kuvaa nafasi ya mkt bila kukiua chama hayupo.

Labda Si CCM hii nayoijua mm.
 
Uko sahihi kabisa!
Hata Zimbabwe pia Morgan Tsvangirai (R.I.P).alipoteza mvuto,baada tu ya kufanya maridhiano na Serikali ya Robert Mugabe (R.I.P).
 
TINDO yupo sawa.

Wasiwasi ndio AKILI.

Chama Cha Mapinduzi Si Rahisi kuachia bila KUPINDULIWA,

Tujifunze Zanzibar, Maalim alitumia njia zote za nguvu na ustaarabu bt nn yalikuwa matokeo yake???
Wasiwasi sio akili pekee, wakati mwingine ni uoga usio na maana..

Mbaya zaidi unapokomalia jambo mpaka kwa kutafuta sababu za kutengeneza [fabricated] ili kuhalalisha unachopigania, wakati uhalisia field ni tofauti.
 
Wasiwasi sio akili pekee, wakati mwingine ni uoga usio na maana..

Mbaya zaidi unapokomalia jambo mpaka kwa kutafuta sababu za kutengeneza [fabricated] ili kuhalalisha unachopigania, wakati uhalisia field ni tofauti.
Kwamba unaamini CCM wanaweza wakakubali kuachia madaraka ya nchi nafasi ya Urais Kwa maridhiano?

Zanzibar hapo Jirani hapakupi tu kujifunza?
 
Ni wazi mwenyekiti kalamba asali na kwakua alijua akiwa sober hawezi ongea vile akaona atupie vitu kwanza ndio apande kwa stage
 
The fact kuwa wana CHADEMA waliokuwa magerezani na mahakamani kwenye makesi uchwara ya yule dhalimu mwendawazimu wako huru sasa hilo ni jambo la msingi sana..

JPM alikuwa na uchungu na maendeleo ya nchi ila ukatili wake dhidi ya binadamu wengine utabaki kwenye historia.
 
Komredi Mbowe umeacha alama kubwa sana ktk siasa za upinzani Tz.
Umejaa karama na kipawa cha uongozi ambacho wengine hawana!
Songa mbele usirudi nyuma lkn nakuhakikishia hata ndani ya CDM ya sasa kuna mapandikizi!
 
Kwamba unaamini CCM wanaweza wakakubali kuachia madaraka ya nchi nafasi ya Urais Kwa maridhiano?

Zanzibar hapo Jirani hapakupi tu kujifunza?
Suala la kuachia madaraka hiyo ni next stage, kwa sasa tukubaliane maridhiano yameleta mikutano ya siasa, na kama maridhiano yameleta mikutano ya siasa, basi pia, muamini yataleta Katiba Mpya na mengineyo ikiwemo Tume Huru.

Mbowe na Chadema wanaipigania, Samia nae kaonesha ushirikiano kwa upande wao, sasa kwanini muendelee kuishi kwa wasiwasi na mashaka kama sio ujinga tu wa kiharakati uliojaa kwenye vichwa vyenu? tena wakati mwingine mpaka kujitungia vijisababu vya vilema!.

Mkiambiwa siasa ni sayansi muelewe, msishupaze shingo na mbinu moja tu ya kukariri ya harakati.
 
Kwanza nashukuru kwa kunifuatilia, na kizuri zaidi kutokukubaliana na mtazamo wangu, hasa kuhusu huyo Freeman Mbowe. Napenda kusema naheshimu mtazamo wako kwani hiyo ndiyo afya ya mjadala, na zaidi hiyo ndio demokrasia.
Ok.

It's true and thanx for that at least
1. Kuhusu mtazamo wako wa kiongozi kukaa muda mrefu madarakani, hilo halina shida kwangu. Ni maoni yako and I respect that kwa sababu kwa hilo hata Mimi naweza kuwa na maoni tofauti na ndivyo ilivyo. Na kuhusu hilo, mimi nadhani hata Freeman Mbowe na CHADEMA wenyewe nina hakika wanajua umuhimu wa kubadili uongozi baada ya muda fulani..

Lakini kwa mazingira ya siasa za Kitanzania na Afrika au ktk nchi za dunia ya tatu, ziko factors mbalimbali za kuangalia Kila kunapotaka kufanyika inner political party power transition na moja kubwa ni uwezo wa kiongozi huyo kuunganisha makundi mbalimbali ndani ya chama cha siasa bila kuwa compromised. Freeman Mbowe ktk mazingira ya siasa hizi anastahili na ameweza kuilinda CHADEMA na ndiyo maana Iko hai leo na inaendelea kukua kwenda mbele..

Hii yote inatokana na uongozi thabiti wa huyu ndugu.

Hata hivyo hayupo binadamu aliye perfect 100% . Hata Mbowe ana mapungufu yake. Lakini it's a fact that mapungufu kiuongozi ya Mbowe yanafunikwa na mazuri ya uongozi wake kwa muda wote alioshika madaraka ya uenyekiti

Kwa kiongozi muwajibikaji, baada ya blunder ya kumpokea Lowassa kushindwa kupata urais, Mbowe alipaswa Kujiuzulu.
Hapa una maanisha nini?

Je, una maana Kila mwanachama aliyekaribishwa CHADEMA akitokea CCM na kisha baadae kuondoka zake basi viongozi waliojadili uanachama wake na kuchukua uamuzi wa kukaribisha wanachama haa wanapaswa kijiuzuru.?

Je, hukumbuki kuwa chini ya Mbowe huyuhuyu walikaribisha wana-CCM kibao mwaka kati ya mwaka 2010 na 2015 wakiwemo kina Shibuda kisha wakagombea ubunge na kushinda? Kwanini hutoi credits kwa hilo? Huyu Edward Lowassa ana u - speciality gani hata umtumie kama kigezo cha kum-discredit huyu Mbowe na kutaka ajiuzuru.?
Ama kama aliona sio sawa, kujiuzulu baada ya kosa lile, basi hakupaswa kugombea uenyekiti tena msimu uliopita.
Soma maelezo hapo juu
Jambo hili halinipi ruhusa dhamira yangu kukubaliana na mwenendo huo. Hii ni haki yangu ya kidemokrasia, je nakosea kutumia haki yangu ya kidemokrasia kumkataa kiongozi ambaye nina sababu za msingi za kumkataa?
Hukosei hata kidogo. Ni maoni yako na ni haki yako ya kabisa. Lakini wapo ambao hawatakubaliana na maoni yako. Muhimu ni kuheshimiana you..!!
Sababu hizi sio lazima ziwe za msingi kwako, lakini kwangu zina msingi, na nitazishikilia.
Yes. You are absolutely right..

Ndio maana nasema, NAHESHIMU MAONI YAKO..
Kama wewe si muumini wa ku - resolve conflicts kwa njia za amani (mazungumzo), then there's something wrong in you.

Huwaamini CCM, it's ok.

Lakini utawakwepaje hawa maana ndiyo walio madarakani, wanaongoza serikali? Ulitaka akaridhiane na nani labda? ACT WAZALENDO? CUF? NCCR MAGEUZI?
Nahitimisha kwa kusema, ni sahihi sana Mbowe kukaa pembeni, kwani ameshakaa muda wa kutosha, na sasa anaelekea kushuka chini, ni vyema akakaa pembeni akapisha wengine, labda uniambie kuwa huko CDM hakuna mwingine zaidi yake kwa nafasi ya uenyekiti.
Hopefully, kwa wakati wake hilo litafanyika. CHADEMA walio wengi wanajua na Freeman Mbowe mwenyewe anajua..
 
Tusubiri.
 

Nakushukuru kwa maoni yako yenye wingi wa busara. Tuje hapo kwa Lowassa. Nitaanzia hapo hapo kwa Shibuda. Ifahamike Shibuda alikuwa bungeni kama mbunge wa CDM, lakini aliyekuwa hashirikiani na cdm tena kiutendaji. Ilifika mahali tukawa tunajiapiza kuwa tusirudie tena kuokota wañaccm tena kwa njia ya voda Fasta. Mbona 2015 ndio tukafanya kosa kubwa kuliko la huyo Shibuda?

Ifahamike baada ya uchaguzi wa 2010 kuelekea 2015, CDM ndio chama kilichofanya mikutano mingi kuliko vyama vyote ikiwemo CCM? Unajua ndio chama kilichotoa elimu ya uraia, na kupandisha hamasa ya kisiasa katika wakati huo kuliko chama chochote? Wakati yote hayo yakifanyika Lowassa alikuwepo? Je wafuasi wa CDM na wananchi walimchukulia vipi Lowassa? Unafahamu vitambulisho vya kupigia kura viliitwa vichinjio kwa ajili ya kumchinja Lowassa, kwani ilionekana ndio atakuwa mgombea wa CCM? Inawezekana vipi chama makini kumchukua mtu iliyemtumuhumu muda wote huo, na kumpa nafasi adhimu kama kugombea urais? Ina maana hatukujifunza kwa kosa la Shibuda, huoni hoja yangu ilipo? Haya haidhuru tumechukua Lowassa, chama kimeonekana hakina msimamo, tena kwa jambo lililopaswa kupimwa madhara yake, lakini bado mtu huyo huyo akaondoka mbali ya madhara aliyokifanyia chama. Niliache hili maana nina shaka kama utakuwa na majibu ya uhakika.

Tuje kwenye ofisi za chama. Baada ya uchaguzi wa 2015-2020 CDM ilipata wabunge wengi, hii maana yake ruzuku kubwa zaidi. Ifahamike kipindi chote hicho ni kama shughuli za kisiasa zilipigwa marufuku. Ina maana pesa zilizokuwa zikiingia hapo awali kwenye mikutano, hazikuenda tena. Je ni kwanini ruzuku hiyo haikutumika kujenga ofisi angalau 1 kila mkoa ya 50m? Ukiachia ruzuku, sigusii Kiwango ambacho kila mbunge alikuwa anatoa kwa mujibu wa makubaliano yao. Hapo achia mbali pesa zilizotolewa kwa uwazi na kificho kuoa support CDM.

Je katika mazingira hayo, unawezaje kusema mwenyekiti huyo ni bora, na anastahili kufumbiwa macho hata baada ya kukaa muda mrefu?

Pamoja na maelezo hayo, sikatai kwamba mchango wake wa hali na mali umeifikisha CDM mahali pazuri. Na ninaheshimu ukweli huo. Lakini nitakuwa najiongopea mwenyewe kuendelea kuwa na mwenyekiti wa aina hiyo, eti tu kisa wakati fulani huko nyuma alifanya vyema. Ni hatari kubwa kwa taasisi kama hiyo kuwa na mtazamo wa kiongozi wa muda mrefu, kwa kichaka cha siasa za Afrika. Je akifariki hiyo taasisi itakuwa mwisho wake, maana hiyo taasisi haitahamia ulaya? Kama tunaimani hiyo kuhusu Mbowe, ni kwanini tunataka kuitoa CCM, na tunashangaa inaposema haimini kama chama kingine kitaweza kuongoza nchi?
 

Boss sijakuona tena ukija kujibu post yangu namba 92, huenda utakuwa unakusanya nondo za uhakika. Tena uzuri id yako ni mpya, huenda ndio Mbowe mwenyewe. Nakukaribisha siku ukipata nafasi, bado huu mjadala haujafungwa unaweza kutoa ufafanuzi hasa ni wapi fedha za 2015-2020 zilipoishia.
 
Kuweni makini, Bi Mkubwa is a very smart politician, kwenye miaka yenu 30 ya mapambano hamjawahi kukutana na mwanasiasa smart kama huyu
 
Kuweni makini, Bi Mkubwa is a very smart politician, kwenye miaka yenu 30 ya mapambano hamjawahi kukutana na mwanasiasa smart kama huyu

Mmhhh, hizi sifa mbona naona kila rais hupewa? Au hizi sifa ni auto, hivyo ni maneno yanayotokea kila rais anayekuwa madarakani kwa tiketi ya ccm?
 
Analysis yako imeshiba na nimeieelewa. Maridhiano ni give and take, hakuna winner takes all approach.

Ninaamini huko mbele kuna vitu vingi vya msingi ambavyo ni muhimu kuliko Siasa ngumu. Àthari za Siasa ngumu tumeziona kwa Magufuli, hazina tija na ni hatari kwa utaifa wetu.

Ni matatajio yangu kuwa huko mbele kwenye maridhiano kuna takwa la kufanya uchunguzi wa mauaji ya Ben Saanane na kushambuliwa Tundu Lissu ambayo ndiyo kiu ya Watanzania wengi.

Subira yavuta heri
 
Umepiga ngumi ya Sogunyo kama ya Mandonga. Wakikujibu niko pale niite mbwa
 
Ukiambiwa uandamane unajificha ndani kwenu, Mange Kimambi anawajuwa vizuri unafki wenu.
 
Hongera kwa uchambuzi mzuri na uliojaa logic kaka.naunga mkono hoja one tanzania one nation
 
Umepiga ngumi ya Sogunyo kama ya Mandonga. Wakikujibu niko pale niite mbwa
Hawa jamaa wamejaa hoja nyepesi sana, mwishowe wanajiegemeza kwenye vivuli vya vilema, mara haki yao kidemokrasia kutoa maoni yao...

Hawajui haki ya kidemokrasia haiwezi ku extend mpaka mawazo ya mjinga yakubaliwe, kama mawazo yako ni ya kijinga, yatabaki ujinga tu, bila kujali kama kuyatoa ilikuwa haki ya kidemokrasia au kidikteta!.
 
Sheria ya vyama vya siasa inamruhusu mtu yeyote, bila kujali rangi, jinsia, na vinginevyo, kujiunga na chama chochote apendacho, ilimradi akidhi vigezo vilivyopo kwenye chama husika atakapokwenda.

Hii ndio sababu ya Chadema kuwapokea wote, Lowassa na Shibuda, utambue Chadema sio chama cha mtu binafsi, au mali ya familia fulani, au kikundi fulani cha watu kama unavyodhani, mpaka unakuwa na mawazo ya kuwatenga wengine, Chadema ni Public Political Party.

Hapa suala la Shibuda kutoungana na wenzake kwenye shughuli za chama, au Lowassa kuitwa fisadi muda wote wa mikutano ya siasa waliyofanya Chadema miaka iliyopita, hayawezi kuwa na uzito wa kuvunja sheria kumkataa mwanachama anayetaka kujiunga nao, mawazo yoyote ya kutompokea mtanzania yeyote kwenye chama, yalikuwa ni potofu yaliyojaa uvunjifu wa sheria, ajabu huu upotofu umekaa nao kichwani mpaka leo, tena ndio unauita nondo zisizojibika!

Suala la ruzuku baada ya uchaguzi wa 2015 - 2020 kwamba kwanini hiyo pesa ya ruzuku haikujenga ofisi za chama..

Tabia za Magufuli baada ya kuingia madarakani hakuna asiyezijua, alianza kubana kila kona, sio tu kuwapora watu fedha zao, lakini alifikia mpaka kuzuia ruzuku kwa Chadema, na kama alikuwa akiitoa, hakuitoa kwa wakati, na kwa kiwango kile kilichotakiwa, sasa unapomlaumu Mbowe kutokujenga ofisi, ulitaka atoe pesa zake mfukoni?

Na kama angezitoa si ndio ungeanza kulalamika kwamba chama kinaendeshwa kwa fedha za Mbowe?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…