Hongera Mbowe umeshinda mchezo wa kisiasa

Kujua handwriting ya mwanamke na Mwanaume Huwa unafanya utafiti?

Ndivyo ilivyo,

Mimi niliwahi kumsikia Dr Issaac wa Clouds kipindi Cha njia panda na niliweza kutengeneza image ya sura yake akilini mwangu,

Nilipokuja Kumuona live, ndivyo alivyoonekana.

Ukipenda Amini. Usipopoamini sawa pia.
Sasa utajuaje handwritting kama ni ya mwanamke au mwanaume hapa JF?

Hebu tusibishane kama watoto.
 
Hapa nafurahi umeshatambua mimi sio yule, nashukuru kwa kufahamu hilo, hivyo uache kuendeshwa kwa hisia ukiwa JF na kujibu comments za wengine kwa kutumia hisia, hapa tunahitaji facts.

Mwisho, mimi huwa natwanga kwa hoja, sikutwangi kwa mawe au ngumi, najua hii itakuwa njia yako kukimbia, nimekuelewa, kuhusu mjadala wenu nawaachia, niliingilia tu baada ya kuona umejimwambafy kwa hoja zako nyepesi zilizojaa hisia kuwa hazijibiki!

Baada ya kuona umeingia ikabidi nicheke, ndio maana nimeogopa usije ukanitwanga kwa hoja 😂😂
 
Hongera kwa kurejea. Tuanzie hapo kwa Shibuda. Sina popote ninapokataa mtu ama kiongozi yoyote kupokelewa ndani ya CDM. Ninachokataa ni mtu kupokelewa ndani ya muda mfupi na kupewa nafasi ya kugombea. Case study ikawa huyo Shibuda baada ya kuingia muda mfupi, akaendelea na tabia zake za kiccm. Hilo lilipelekea kutoshirikiana na chama. Labda useme hakunyimwa ushirikiano.
Katiba ya CHADEMA inasema mtu apokelewe kuwa mwanachama muda upi? Hebu fafanua...
Narudia tena, sina popote ninapokataa mtu kupokelewa na kupewa uanachama, ninachokataa ni mtu kupokelewa tena ndani ya muda mfupi, na kupewa nafasi ya kugombea, huku wanachama waaminifu wakiachwa. Matokeo yake hao watu wa kuokoteza wanakuwa wepesi kutokuenda na mtazamo wa chama, au kukosa uvumilivu. Kwenye hili tukubali kutokubaliana.
Tindo, ili mtu (mwanachama) apate nafasi ya kugombea uongozi wa kuchaguliwa kwa udhamini wa chama ni sharti afikie vigezo vilivyowekwa na chama.

Kama hawa walipata nafasi, obvious walikuwa na sifa kuwazidi walioachwa. Kigezo cha kuwa mwanachama tu wa muda mrefu, hakitoshi.
Nijuavyo Slaa hakuwa mwanachama wa CCM baada ya kuondoka CDM, bali alifanya majukumu ya kiserikali. Je kufanya majukumu ya kiserikali ni kufanya kazi za CCM? Unanituhumu kwa hisia, ila unataka niamini Slaa alienda kufanya kazi za CCM.
Aaah, hakuwa mwanachama wa CCM siyo?

Labda ulikuwa hujui, naomba nikujulishe kitu kimoja. Uanachama siyo 'kadi ya chama' bali ni zaidi ya hicho
Huu upotoshaji kuwa Lowassa alileta kura 6m huwa nikisikia nacheka sana. Kwahiyo kazi yote kubwa ya CDM toka 2010-2015 haikuleta hizo kura 6m, bali uwepo wa Lowassa ndio ulileta hizo kura ndani ya miezi miwili! Kama Lowassa alileta kura 6m+ akiwa na miezi miwili, alileta viti vingapi vya ubunge na udiwani akiwa na miaka miwili?
Ok. Naheshimu maoni yako...
Ni kweli mwenendo wa kufanya siasa unabadilika, na kubadilika ni lazima, ila sio kama unavyosema ww. Nimejibu haya maana nimeona wangalau yanaelekea, hayo mengine naona ni burudani kama burudani nyingine.
Vizuri Kwa kuelewa kuwa ufanyaji siasa umebadilika.

Kama unaelewa hili, basi ni vyema ukakubali kwenda sambamba na mabadiliko hayo ili kuwa relevant...
 
Katiba ya CHADEMA inasema mtu apokelewe kuwa mwanachama muda upi? Hebu fafanua...

Tindo, ili mtu (mwanachama) apate nafasi ya kugombea uongozi wa kuchaguliwa kwa udhamini wa chama ni sharti afikie vigezo vilivyowekwa na chama.

Kama hawa walipata nafasi, obvious walikuwa na sifa kuwazidi walioachwa. Kigezo cha kuwa mwanachama tu wa muda mrefu, hakitoshi.

Aaah, hakuwa mwanachama wa CCM siyo?

Labda ulikuwa hujui, naomba nikujulishe kitu kimoja. Uanachama siyo 'kadi ya chama' bali ni zaidi ya hicho

Ok. Naheshimu maoni yako...

Vizuri Kwa kuelewa kuwa ufanyaji siasa umebadilika.

Kama unaelewa hili, basi ni vyema ukakubali kwenda sambamba na mabadiliko hayo ili kuwa relevant...

Mtu anaweza kupokelewa muda wowote kuwa mwanachama wa CDM, lakini kwa taasisi makini anayepaswa kupewa nafasi ya kugombea uongozi lazima apitie michujo kadhaa na inayoaminika. Ile 2015 umakini haukuwepo. Kama waliochaguliwa huku wakiwa wamefika muda mfupi kabla ya uchaguzi, basi ujue ni hela zao. Sasa kama mtu anaweza kuja muda wowote na kupata nafasi ya kugombea, ana haja gani ya kuja kuhangaikia chama, wakati akija muda wowote tu anaweza kupata nafasi ya kugombea? Ukiona mtu anapata nafasi ya kugombea kwa fedha zake, ujue hicho sio chama boss, bali kikundi cha wajanja, na hiyo ndio taswira ya CDM.

Slaa hakuwa mwanachama wa ccm, kwani uanachama lazima uwe na kadi. Umeshasema tuache hisia, sasa hapa sijui inakuwaje tena!

Kubadilika ni sahihi, lakini kubadilika kuendana na utashi wa CCM, huko sio kubadilika, bali kubadilishwa. Ukashabadilishwa huna haki ya kutamba kuwa umebadilika.

Pamoja na maelezo yako mazuri ambayo nayaheshimu sana. Sioni ukizungumzia ni wapi fedha za ruzuku kutokana na uchaguzi wa 2015-20 zilipoingia, ili nipime vipaombele vya CDM. Maana mikutano haikuwepo. Na sidhani kama eneo hilo unalikwepa kwa bahati mbaya, bali naona unacheza na maneno tu, huku ukichombeza na vijimaneno kadhaa ya kiingereza,😂😂
 
Pamoja na maelezo yako mazuri ambayo nayaheshimu sana. Sioni ukizungumzia ni wapi fedha za ruzuku kutokana na uchaguzi wa 2015-20 zilipoingia, ili nipime vipaombele vya CDM. Maana mikutano haikuwepo. Na sidhani kama eneo hilo unalikwepa kwa bahati mbaya, bali naona unacheza na maneno tu, huku ukichombeza na vijimaneno kadhaa ya kiingereza,

1. Hayo mengine yote nilishaandika na kushea na wewe sana.

Nadhani inatosha na tukubaliane kutokukubaliana

2. Hili la pesa za ruzuku na zimefanya nini na zilikuwa ngapi, nilikuambia hayo siyajui maana mimi simo humo ndani ya CHADEMA.

Umeliibua wewe, basi liko mikononi mwako kulithibitisha maana ulishaonesha kuwa unaelewa CHADEMA hupata fedha kiasi gani na hutumikaje. Ndiyo maana unaandika Kwa ujasiri kabisa kuwa huwa zinaibiwa na Mbowe.

3. Sasa nakupa challenge kwamba, mambo ya fedha hayajadiliwi bila kuwa na data sahihi na za kutosha.

Ili ujue pesa za CHADEMA huibiwa au hutumikaje; vibaya au vizuri, basi ingalau ujue haya;

✓ Vyanzo vya mapato yao.

✓ Kiasi wanachopata kwa siku, wiki, mwezi au mwaka 1 au miaka 5.

✓ Bajeti (mpango wao wa matumizi ya fedha hizo Kwa kipindi fulani) ni upi.

✓ Nini ni vipaumbele vyao ktk matumizi Yao.

Ukielewa haya ndugu Tindo kuhusu fedha za CHADEMA utakuwa na haki ya kutuambia kuwa pesa za CHADEMA huibiwa au vinginevyo. Kinyume chake unaleta umbeya na propaganda tu!!

Asante na usiku mwema
 
Mtu anaweza kupokelewa muda wowote kuwa mwanachama wa CDM, lakini kwa taasisi makini anayepaswa kupewa nafasi ya kugombea uongozi lazima apitie michujo kadhaa na inayoaminika. Ile 2015 umakini haukuwepo. Kama waliochaguliwa huku wakiwa wamefika muda mfupi kabla ya uchaguzi, basi ujue ni hela zao. Sasa kama mtu anaweza kuja muda wowote na kupata nafasi ya kugombea, ana haja gani ya kuja kuhangaikia chama, wakati akija muda wowote tu anaweza kupata nafasi ya kugombea? Ukiona mtu anapata nafasi ya kugombea kwa fedha zake, ujue hicho sio chama boss, bali kikundi cha wajanja, na hiyo ndio taswira ya CDM.

Slaa hakuwa mwanachama wa ccm, kwani uanachama lazima uwe na kadi. Umeshasema tuache hisia, sasa hapa sijui inakuwaje tena!

Kubadilika ni sahihi, lakini kubadilika kuendana na utashi wa CCM, huko sio kubadilika, bali kubadilishwa. Ukashabadilishwa huna haki ya kutamba kuwa umebadilika.

Pamoja na maelezo yako mazuri ambayo nayaheshimu sana. Sioni ukizungumzia ni wapi fedha za ruzuku kutokana na uchaguzi wa 2015-20 zilipoingia, ili nipime vipaombele vya CDM. Maana mikutano haikuwepo. Na sidhani kama eneo hilo unalikwepa kwa bahati mbaya, bali naona unacheza na maneno tu, huku ukichombeza na vijimaneno kadhaa ya kiingereza,[emoji23][emoji23]
Usijiwekee kigezo kimoja pekee cha mtu kupokelewa chamani kwamba lazima awe amepitia mchujo, unaonesha ulivyojifunga akili, kuna njia nyingine na zenye mafanikio...

Hapa lazima tukubaliane, mtu kupokelewa chamani na kupewa nafasi ya kugombea inawezekana pia factors nyingine zikachukua nafasi, ikiwemo kukubalika kwa mgombea kwa wakati na jamii husika...

Hiki ndicho kilichochangia Lowassa kupokelewa Chadema, na kupewa nafasi, na hata yale "mafuriko" yaliyokuwepo wakati ule yalichangiwa na uwepo wake, lakini mawazo yako potofu hayawezi kuwa mipango ya taasisi makini, na kama ikiyafuata itakufa kwa kukariri mbinu outdated!.

Hapa hata kama utasema juhudi za chama kujijenga zilichangia, lakini huwezi kupuuza uwepo wa Lowassa na nguvu ya kisiasa aliyokuwa nayo kwa wakati ule, na kusema unachekeshwa kuambiwa Lowassa alichangia kura mil 6+ unaonesha ulivyo na upeo mfupi.

Naandika hivi kwa sababu, kama unaamini ni suala la juhudi za chama pekee kuchangia kura milioni 6+, mbona tuliona Dr. Slaa akiwa mgombea wa Chadema 2010, pamoja na umaarufu wote aliokuwa nao wakati ule, na jitihada za chama kujijenga, tena mbele ya JK dhaifu, lakini bado alishindwa kufikia idadi hiyo ya kura? na kupata mafuriko kama ya Lowassa?

Huo ni uthibitisho kwamba, usikariri njia moja pekee ya kupata mgombea chamani kwamba ndio italeta mafanikio kwa chama wakati wa uchaguzi, unajidanganya, nguvu ya Lowassa 2015 haiwezi kupuuzwa na yeyote anayejielewa..

Kuhusu suala la ruzuku nilishakujibu, wacha kulazimisha mawazo yako pekee ndio iwe mipango ya chama, nilishakwambia, kama unaiamini ripoti ya CAG, na kama ripoti ya CAG ilikuwa safi kwa mahesabu ya Chadema, basi huo ni uthibitisho tosha kwamba pesa zile zilitumika vizuri.

Lakini kulazimisha kile unachotaka wewe ndio kiwe mipango ya chama, huo kwangu ni udikteta tu, na usijifiche kwenye kivuli cha kuuliza watu maswali wasiyo na taarifa nayo ili ujione mjuaji, unajidanganya, naona unatafuta tu uchochoro wa kutokea, simply visit website yao, piga simu, au nenda Ufipa kawaulize...
 
Baada ya kuona umeingia ikabidi nicheke, ndio maana nimeogopa usije ukanitwanga kwa hoja [emoji23][emoji23]
Cheki nilivyokutwanga hapo juu[emoji3][emoji3], tena kwa mfano halisi, dogo uwe mpole, usirudie kujimwambafai huku unachoandika hakijibiki!.
 
Mkuu sikutegemea uwe na jipya kwenye hili, na kwa kukusaidia tu unataka nikapte habari kwenye website ya CDM, hebu ingia kwenye hiyo website uone nini kinaendelea kisha uje tuendelee na mjadala. Kwenye hiyo website ndio utajua nini naongea.
 
Cheki nilivyokutwanga hapo juu[emoji3][emoji3], tena kwa mfano halisi, dogo uwe mpole, usirudie kujimwambafai huku unachoandika hakijibiki!.

Mkuu kweli ww unajua kutwanga tena ni kwa hoja tu!🤣🤣
 
1. Hayo mengine yote nilishaandika na kushea na wewe sana.

Nadhani inatosha na tukubaliane kutokukubaliana

2. Hili la pesa za ruzuku na zimefanya nini na zilikuwa ngapi, nilikuambia hayo siyajui maana mimi simo humo ndani ya CHADEMA.

Umeliibua wewe, basi liko mikononi mwako kulithibitisha maana ulishaonesha kuwa unaelewa CHADEMA hupata fedha kiasi gani na hutumikaje. Ndiyo maana unaandika Kwa ujasiri kabisa kuwa huwa zinaibiwa na Mbowe.

3. Sasa nakupa challenge kwamba, mambo ya fedha hayajadiliwi bila kuwa na data sahihi na za kutosha.

Ili ujue pesa za CHADEMA huibiwa au hutumikaje; vibaya au vizuri, basi ingalau ujue haya;

✓ Vyanzo vya mapato yao.

✓ Kiasi wanachopata kwa siku, wiki, mwezi au mwaka 1 au miaka 5.

✓ Bajeti (mpango wao wa matumizi ya fedha hizo Kwa kipindi fulani) ni upi.

✓ Nini ni vipaumbele vyao ktk matumizi Yao.

Ukielewa haya ndugu Tindo kuhusu fedha za CHADEMA utakuwa na haki ya kutuambia kuwa pesa za CHADEMA huibiwa au vinginevyo. Kinyume chake unaleta umbeya na propaganda tu!!

Asante na usiku mwema

Mkuu nilitegemea lazima kwenye maelezo yako uanze kupindisha maelezo ile yabebe utetezi wako. Unasema nimeandika kuwa pesa zinaibiwa na Mbowe, unaweza kuonyesha ni post ipi? Nimesema Mbowe hastahili tena kuwa mwenyekiti wa CDM, na sababu nimezitoa bila kujali unakubaliana nazo ama la. Pia nikasema ni wapo fedha za ruzuku ziliingia baada ya uchaguzi wa 2015-20. Hiyo kusema Mbowe kaziiba naona unajishuku.

Narudia tena sema fedha zilifanya nini, usitumie jazba kwenye kujibu mambo ya fedha, na ukiona kuna majibu ya jazba, ujue hapo ndio tatizo lilipo.
 
Back
Top Bottom