Mtu anaweza kupokelewa muda wowote kuwa mwanachama wa CDM, lakini kwa taasisi makini anayepaswa kupewa nafasi ya kugombea uongozi lazima apitie michujo kadhaa na inayoaminika. Ile 2015 umakini haukuwepo. Kama waliochaguliwa huku wakiwa wamefika muda mfupi kabla ya uchaguzi, basi ujue ni hela zao. Sasa kama mtu anaweza kuja muda wowote na kupata nafasi ya kugombea, ana haja gani ya kuja kuhangaikia chama, wakati akija muda wowote tu anaweza kupata nafasi ya kugombea? Ukiona mtu anapata nafasi ya kugombea kwa fedha zake, ujue hicho sio chama boss, bali kikundi cha wajanja, na hiyo ndio taswira ya CDM.
Slaa hakuwa mwanachama wa ccm, kwani uanachama lazima uwe na kadi. Umeshasema tuache hisia, sasa hapa sijui inakuwaje tena!
Kubadilika ni sahihi, lakini kubadilika kuendana na utashi wa CCM, huko sio kubadilika, bali kubadilishwa. Ukashabadilishwa huna haki ya kutamba kuwa umebadilika.
Pamoja na maelezo yako mazuri ambayo nayaheshimu sana. Sioni ukizungumzia ni wapi fedha za ruzuku kutokana na uchaguzi wa 2015-20 zilipoingia, ili nipime vipaombele vya CDM. Maana mikutano haikuwepo. Na sidhani kama eneo hilo unalikwepa kwa bahati mbaya, bali naona unacheza na maneno tu, huku ukichombeza na vijimaneno kadhaa ya kiingereza,[emoji23][emoji23]
Usijiwekee kigezo kimoja pekee cha mtu kupokelewa chamani kwamba lazima awe amepitia mchujo, unaonesha ulivyojifunga akili, kuna njia nyingine na zenye mafanikio...
Hapa lazima tukubaliane, mtu kupokelewa chamani na kupewa nafasi ya kugombea inawezekana pia factors nyingine zikachukua nafasi, ikiwemo kukubalika kwa mgombea kwa wakati na jamii husika...
Hiki ndicho kilichochangia Lowassa kupokelewa Chadema, na kupewa nafasi, na hata yale "mafuriko" yaliyokuwepo wakati ule yalichangiwa na uwepo wake, lakini mawazo yako potofu hayawezi kuwa mipango ya taasisi makini, na kama ikiyafuata itakufa kwa kukariri mbinu outdated!.
Hapa hata kama utasema juhudi za chama kujijenga zilichangia, lakini huwezi kupuuza uwepo wa Lowassa na nguvu ya kisiasa aliyokuwa nayo kwa wakati ule, na kusema unachekeshwa kuambiwa Lowassa alichangia kura mil 6+ unaonesha ulivyo na upeo mfupi.
Naandika hivi kwa sababu, kama unaamini ni suala la juhudi za chama pekee kuchangia kura milioni 6+, mbona tuliona Dr. Slaa akiwa mgombea wa Chadema 2010, pamoja na umaarufu wote aliokuwa nao wakati ule, na jitihada za chama kujijenga, tena mbele ya JK dhaifu, lakini bado alishindwa kufikia idadi hiyo ya kura? na kupata mafuriko kama ya Lowassa?
Huo ni uthibitisho kwamba, usikariri njia moja pekee ya kupata mgombea chamani kwamba ndio italeta mafanikio kwa chama wakati wa uchaguzi, unajidanganya, nguvu ya Lowassa 2015 haiwezi kupuuzwa na yeyote anayejielewa..
Kuhusu suala la ruzuku nilishakujibu, wacha kulazimisha mawazo yako pekee ndio iwe mipango ya chama, nilishakwambia, kama unaiamini ripoti ya CAG, na kama ripoti ya CAG ilikuwa safi kwa mahesabu ya Chadema, basi huo ni uthibitisho tosha kwamba pesa zile zilitumika vizuri.
Lakini kulazimisha kile unachotaka wewe ndio kiwe mipango ya chama, huo kwangu ni udikteta tu, na usijifiche kwenye kivuli cha kuuliza watu maswali wasiyo na taarifa nayo ili ujione mjuaji, unajidanganya, naona unatafuta tu uchochoro wa kutokea, simply visit website yao, piga simu, au nenda Ufipa kawaulize...