Hongera sana mchungaji Dkt. Kimaro kwa kufahamu ukweli

Hongera sana mchungaji Dkt. Kimaro kwa kufahamu ukweli

Ukifika Kanisani homiliya yako ilenge kwenye liturijia ya siku na sio kuanza blaa blaaa za mtaani.

Ndio maana amefukuzwa.
 
ASKOFU MWAMAKULA AZUNGUMZIA SUALA LA KUSIMAMISHWA KWA MCH. DKT. KIMARO

Taarifa za kupewa likizo na kusimamishwa kwa muda kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Kijitonyama Mch. Dkt. Eliona Kimaro zimeanza kuenea katika mitandao ya kijamii na kuzua hisia nzito miongoni mwa waumini na wasio waumini wa KKKT. Kimaro ni miongoni mwa watu maarufu, hivyo suala hili haliwezi kuchukuliwa wepesi.

Hapa tumeweka tazamo wetu wa kitheologia ili kutoa mchango wetu katika hoja hii. Ni dhahiri kuwa misimamo binafsi ya Mch. Dkt. Kimaro imemtia katika misuguano mingi na uongozi wa KKKT kwa kipindi kirefu. Lakini, misimamo hiyo iliweza kuvumiliwa ndani ya KKKT na ndio maana alipewa kuongoza Usharika mkubwa katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Tumefuatilia kutoka kwa baadhi ya viongozi ndani ya Dayosisi ya Mashariki na kuelezwa kuwa matamshi ya Mch. Dkt. Kimaro aliyoyatoa hivi karibuni baada ya kutoka Marekani ndiyo yaliyopelekea uongozi wa Dayosisi kumuita na kumpa likizo ambayo imeibua hisia na mjadala mzito baada ya yeye Mch. Dkt. Kimaro kutoa hadharani jambo ambalo lilikuwa ni karipio la Kichungaji.

Kwa mujibu wa video iliyosambaa, Mch. Dkt. Kimaro amesikika akisema kuwa vijana wa Kikristo sio waaminifu bali vijana wa Kiislamu ndio waaminifu kuliko vijana wa Kikristo. Mch. Dkt. Kimaro amesikika pia akisema kuwa watu wote wanaosimama madhabahuni [Wainjilisti, Wachungaji na Maaskofu] ni matapeli na watu wote waliokaa kwenye viti [vya ibadani - Wazee wa Kanisa na waumini] ni matapeli pia. Mch. Dkt. Kimaro amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa takwimu [hajataja ni takwimu gani na taasisi iliyotoa takwimu hizo] zinaeleza hayo aliyosema.

Kitheologia tunapata tafsiri kuwa Mch. Dkt. Kimaro hana imani na maadili ya Kikristo, hana imani na mafundisho ya Kikristo na pia hana imani hata na watumishi wenzake wote wa Kikristo kutoka madhehebu yote nchini Tanzania. Tafsiri hapa ni kuwa Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa ana imani na maadili ya Kiislamu, mafundisho ya Kiislamu na hata Mashehe wa Kiislamu. Pia, Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa hana imani pia na hata vijana wake wa Kikristo ndani ya KKKT na nje ya KKKT ambao siku zote yeye mwenyewe amekuwa akiwafundisha katika ibada, mikesha, semina, morning glory, bali ana imani kubwa na vijana wa Kiislamu ndio maana akawaajiri hao katika miradi yake.

Mtumishi ye yote (Mwinjilisti, Mchungaji/Padre au Askofu) kutoka katika madhehebu yetu ya Katholiko (RC, Moravian, Lutheran, Anglikana na Orthodox) akitoa kauli kama hizo, ni lazima aitwe na uongozi wake, ahojiwe na hata ikibidi achunguzwe. Hicho ndicho kilichotokea kwake Mch. Dkt. Kimaro kuitwa na uongozi wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, kuhojiwa na kuchunguzwa. Kauli zake alizotoa zimepingana na imani, mafundisho na maadili ya Kikristo! Kauli ya Mch. Dkt. Kimaro hayakushambulia Ulutheri tu, bali kwa kujua au hata kutokujua, kauli yake ilishambuliwa Ukristo wote kwa ujumla katika nchi hii.

Kwa sababu hiyo, sisi Askofu tunatoa wito kwa waumini wote wa Kikristo nchini kuwa watulivu wakati KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani inashughulikia jambo la Mch. Dkt. Kimaro. Sisi tumelazimika kuandika baada ya kuona kuwa jambo hili limeanza kusambaa mitandaoni na kubeba hisia zaidi kuliko uhalisia na pengine kubeba upotofu mwingi zaidi kuliko ukweli.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.
 
Pamoja na hoja zako nzuri sana, ukweli sisi wakristo sio waaminifu, kimavazi, kimaongezi, kiimani..amenena vizuri. Sisi sio waaminifu.

Unaelewa maana ya mkristo?. Au wewe una deal na majina ya watu. Ukristo ni kuwa mwanafunzi na mfuasi wa Yesu Kristo sio jina la mtu.
 
Unaelewa maana ya mkristo?. Au wewe una deal na majina ya watu. Ukristo ni kuwa mwanafunzi na mfuasi wa Yesu Kristo sio jina la mtu.
Mimi ni mkiristo pia ila sio mwaminifu waislamu wanajitahidi sana kwenye uaminifu
 
Nakubalianq na wewe namba tatu tu,Mengine ni mtazamo tu,ukosefu wa uaminifu hauna mahusiano na dini ya mtu moja kwa moja,yapo Mengi ysnayokatazwa na msaafu lakini waislam wanayafanya,kama kujishughurisha na mziki.
Ukitaja kijana mmoja wa kikristo asiye muaminifu,nitakuonyesha mmoja wa kiislam,
Kijana wa kiislam wa Zanzibar sio Sawa na kijana wa Kiislam wa Dar au Arusha,hapo ishu sio dini,ni muingiliano wa secural life na maisha ya kila siku,
Zenj uislam umekolea sana,na hakuna muingiliano wa ubepari sana.
Ila ndani ya serikali wafanyakazi wapo Wala Rushwa,na wabadhirifu,na Zenj,99%ni Islam!

Tunaangalia msimamo wa Waislam katika kile kilichoandikwa na kinafanyika nyumba za ibada?
Je viongozi wao wanasemaje kuhusu hayo yaliyokatazwa?

Tukirudi kwenye Ubaya, ni kweli kila dini inawatu wabaya lakini tunaangalia uwiano na kiwango cha uovu.

Nimekupa mfano, ukikuta kijana mlarushwa wa Kikristo mlinganishe na kijana mlarushwa wa kiislam, alafu wapime utakuja nipa majibu.

Tuje kwenye uongozi WA juu kabisa.
Fanya Makosa, mfano tukana uongozi mtandaoni kwenye kipindi anaongoza mkristo alafu tukana tena Wakati WA UTAWALA anaoongoza Muislam. Alafu linganisha Response ya Watawala.
Ni vipimo tuu vidogo tunaweza kuvitumia vikatufanya tubadilike tuwe Watu Bora.
 
Unaelewa maana ya mkristo?. Au wewe una deal na majina ya watu. Ukristo ni kuwa mwanafunzi na mfuasi wa Yesu Kristo sio jina la mtu.
Naelewa sana maana ya kuwa mkristo, sasa kama ukristo haufuati tabia za kristo tunasemaje..
 
Uaminifu ndio hoja.
Kama tunashindwa kuwa waaminifu Kwa kufuata yaliyomo kwenye Misahafu yetu mpaka inafikia kipindi MTU anaanzisha na dhehebu linalopingana na Aya za Biblia huoni mpaka hapo tunashida?

Wewe ndio mwenye shida, unachukua imani potofu unalazimisha iwe Ukristo. Mtu anajiita mungu au nabii mkuu, bado mnamuita mkristo. Ukristo Ni kuwa mfuasi na mwanafunzi wa Kristo. Kama mtu hafuati hayo huyo sio mkristo. Narudia Tena, uaminifu Ni suala la mtu binafis sio dini.
 
Mimi ni mkiristo pia ila sio mwaminifu waislamu wanajitahidi sana kwenye uaminifu

Mwambie Aende Kariakoo apime ni Vijana wapi baina ya waislama Vs Sisi Wakristo wanaheshimu Ibada.
Wakati Sisi Wakristo Vijana wengi tukiwaachia Wanawake waende ibada huku Sisi tukitafuta sababu, vipi upande wa Vijana WA kiislam?

Ingawaje sio kama nawatetea Ila tunajaribu kuangalia uaminifu baina Yao na yetu
 
4. Kuheshimu jina la Mungu na manabii wake
Waislam wanaweza kuwa na mapungufu mengi lakini linapokuja suala la Jina la Mungu wao ALLAH na Mtume wao Muhammad kwa kweli hapo wanaonyesha uaminifu mkubwa.
Kupitia taarifa iliyitolewa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Gerald Kusaya leo Jumanne Novemba 15, 2022 amesema kuwa Mamlaka hiyo iliendesha Operesheni katika maeneo mbali mbali ya nchini na kukamata Jumla ya Kilo 34.89 za dawa za kulevya aina heroin.

Katika watuhumiwa hao 11 waliokamatwa yumo Mfanyabishara na Mmiliki wa Kituo cha Michezo cha Cambiasso Sports Academy, Kambi Zubeir Seif.

Amesema watuhumiwa wengine ni Seleman Matola (24) mkulima na mtoto wa dada yake na mtuhumiwa Seif, Said Matwiko (41) fundi seremala, Maulid Mzungu (54) ambaye anaundugu wa mtuhumiwa Sultan ambaye ni kocha wa Simba.

โ€œWengine waliokamatwa ni John Andrew (40) mkazi wa Magore Kitunda, huyu ni mfanyabiashara pia ana jukumu la kutafuta vijana wenye vipaji na kuwapeleka kituo cha Cambiasso Sports Academy, Rajabu Dhahabu (32) mfanyabiashara na mkazi wa Tabata Segerea, Hussein Pazi (41) pamoja na Ramadhan Chalamila (27)โ€ alisema Kusaya

Kusaya alisema katika tukio jingine mamlaka hiyo ilimkamata mtuhumiwa Abdulnasir Kombo (30) ambaye ni mkazi wa Kaloleni jijini Arusha akiwa na biskuti 50 zilizotengenezwa kwa kutumia dawa ya kulevya aina ya bangi kama moja ya malighafi aliyokuwa akiiuza katika eneo la Jiji hilo.
 
Embu linganisha uaminifu baina yetu Sisi Vijana Wakristo Vs Waislam Kwa Hoja. Ili tupime je ELIONA KIMARO kakosea au yupo sahihi

Unalinganisha kwa angle ipi au kupitia wapi?. Na ni utafiti upi ulifanya ukafikia hapo?
 
Wewe ndio mwenye shida, unachukua imani potofu unalazimisha iwe Ukristo. Mtu anajiita mungu au nabii mkuu, bado mnamuita mkristo. Ukristo Ni kuwa mfuasi na mwanafunzi wa Kristo. Kama mtu hafuati hayo huyo sio mkristo. Narudia Tena, uaminifu Ni suala la mtu binafis sio dini.

Mkristo kitabu chake ni Biblia, wanatumia Biblia.
Mkristo siku ya ibada ni jumamosi au jumapili, wanaabudu siku hiyo ya jumapili,
Mkristo anaamini ufufuo na Ujio WA Kristo mara ya pili, nao wanaamini.
Ukristo ni kumkubali Yesu kama BWANA na mwokozi wa Maisha yetu,nao wanaamini hivyo.

Sasa kipi kinakufanya usiwaite kuwa ni Wakristo?
 
Mkuu ukweli hata uwe mchungu vp we upokee

Kwa hivyo siku hizi uaminifu ni suala la dini sio mtu binafsi. Juzi hapa Kuna mwislamu kakimbiwa na mke wake Dubai, hapo utasema dini inahusika. Naona siku hizi jf imekuwa platform ya kushambulia ukristo.
 
Back
Top Bottom