kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,875
Kwani ina maana mtu ukimsifu inakunyima haki ya kumponda akifanya kinyume?. Kukosoa siyo kosa bali ni kuonesha una mtazamo tofauti na huyo unayemkosoa. Ukisifiwa ukafurahi pia si kosa kufurahi unapokosolewa. Huyu jamaa PASCO kwanza ana elimu nzuri ya sheria inayompa mtazamo mpana si kama hawa waandishi uchwara waliofeli shule kisha wakakimbilia DSJ, au wale waganga njaa na wenye kumtumikia matumbo yao. Swali lake nimelipenda na kunipa mtazamo chanya juu yake.ni nyie kesho mtakuja kumponda hapa akimsifia huyohuyo aliyeshindwa kujibu swali vizuri leo..
Hakika nimefurahishwa sana na Mwandishi huyu Pascal Mayalla wa kipekee aliyemuuliza swali Rais lenye msingi na hata rais kajibu kwa ubabaishaji. Natafuta clip au mwenye nayo aiweke.
Kwanza kaanza kwa kuitaji JamiiForums kwa kusema ni mwanachama mwandamizi wa JamiiForums.
...... ni kweli swali la pili halijajibiwa inawezekana walipima kiwango cha ugumu wa swali ikabidi lipotezewe ila ujumbe umefika,Kauliza vema ila swali la pili halijajibiwa.Moderator ameingilia!!!
Binafsi swali la Sammy Awamu alilomuuliza rais Magufuli limekuwa chachu na nimeliona la maana zaidi.
Ni mwandishi gani ameuliza swali lililokukonga moyo wako na lenye maslahi mapana kwa nchi yetu?
mama wee...........Amejibu kuwa uko muhimili ambao uko juu ya mingine bila kutaja ni ibara gani ya katiba inamruhusu kuvunja katiba ya nchi aliyoapa kuilinda na kuitetea
Mayala alianza hotuba,kujifagilia na kutangaza kampuni yake na kujipigia debe la kutafuta fursa ikulu .Sehemu kubwa ya aliyonngea yalikuwa hasa ya kujinadi mnadani yeye binafsi.Kwangu naona kama aligeuza Ikulu na ile press conference kama gulio la kujinadi zaidi kuliko kuuliza swali.
kisutu unapajua njia?PASCO MAYALLA HOYEEEEEE, SWALI LA PASCO MAYALLA HOYEEEEE, MAGUFULI ????? JIBU LA MAGUFULI ZIIIIIIIIIIIIIIII 😡
Ondoa kiherehere chako hapa... we mtu gani usieona na kuthamini wanaolisaidia taifa? Mods wanatakiwa wakupe BAN b'se JF ni platform ya great thinkers sio watu kama ww. Sijajua wanakuchelewesha kwa manufaa ganiMayala alianza hotuba,kujifagilia na kutangaza kampuni yake na kujipigia debe la kutafuta fursa ikulu .Sehemu kubwa ya aliyonngea yalikuwa hasa ya kujinadi mnadani yeye binafsi.Kwangu naona kama aligeuza Ikulu na ile press conference kama gulio la kujinadi zaidi kuliko kuuliza swali.