Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Paschal Mayala ametutendea haki watanzania.
Lakini Rais ameshindwa kujibu kuhusu katazo la shughuli za kisiasa na hata jibu lake kuhusu uhuru wa mihimili mitatu lilikuwa ni dhaifu sana.
 
Pascal Mayalla big up sana,umeuliza maswali bora ila najua hujaridhika na jibu la swali moja na la pili kutokujibiwa.Nimeamini waandishi wa habari ni waoga sana otherwise wewe uko tayari kujua ukweli kwa kila linalokutesa/linalokuumiza akili.HONGERA SANA
 
mimi binafsi simpongezi kwa pasco kwa swali bali kwa kuwakilisha vizuri jukwaa hili la jamii forum ametutendea haki ,siku zote hoja za jamii forum hoja ni nzito zinahitaji upekee kukabiliana nazo .pongezi kwa uwakilishi mzuri hukuficha uhalisia wako na umejitambua ulikotoka ,hii inaonyesha ya kuwa michango yetu inakubalika katika jamii husika .
 
Inasikitisha sana kuona swali zuri kama hilo linakosa jibu kutoka kwa mtu mwenye mamlaka ya kufanya hivyo,kibaya zaidi anaweza kujibu maswali yasiyo na mwelekeo tena kwa tabasamu kubwa na bashasha isiyo na kifani,apo inatupa ishara ni mambo gani serikali inayotaka tuyajue kifupi hawa jamaa wanatutembeza gizani wakiwa wametufunga vitambaa vyeusi machoni huku wakitudanganya kua tupo katika nuru.
 
KUDOS Paschal Mayalla umeitendea HAKI taaluma yako, lakini kubwa zaidi umewatendea haki Watanzania wote!

Waandishi wengine wote waliouliza maswali ni MAKANJANJA!
 
Back
Top Bottom