Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Kwani JPM ni msukuma? cc @Pasco .
Mkuu Mtazamo, kama iliyo dini na kabila it's just a matter of choice, mtu yuko free kujitambulisha kwa kabila la mahali alipokulia not necessarily asili yake halisi ndio maana wa kwanza alijinasibihisha na Zanaki yule wa Mkuranga akajinasibu Mzenji, Yule wa Nchumbiji akajisabu ni Chinga, Mkwere Bagamoyo ni kwa baba wa kufikia, msifuatilie sana makabila ya watu unless kama mnataka kufanya matambiko, tena hala hala msije kuibua kisa cha kijana mmoja aliye lelewa nyumbani kwa Mzee Machalila pale Karagwe na kupewa jina la Kihaya la Katto.

Paskali
 
Aisee maswali kama haya ndiyo hufanya CCM wakimbie midahalo,na si ajabu huu ndio ukawa mwanzo na mwisho kwa mh rais kuulizwa maswali live na kujibu maswali live,maana yake kigongo hiki hakikuwa cha kawaida na mh rais hakutegemea kama angeweza kuulizwa swali kama hili tena kwa ujasiri mkubwa kiasi hiki,kwa vyovyote vile mh atakuwa aliondoka huku ubongo ukiwa unatoa cheche ndani kwa ndani,kumbe mh rais anapopiga marufuku mikutano ya siasa ana fanya hivyo kwa kujihami ili asiwe ana kutana na vigongo kama hiki.
Pasco ni sehemu za sanaa za CCM, hakuja jipya.Kilichokosewa ni excecution tuu. Free style ya muulizwaji na plan mbaya ya waliyoyaengeneza na kupatitisha.
 
Thread sio ya Pasco ila yangu. Na sina uhusiano naye. Wewe mwaga tuu majamboz
Unadhani kwa bongo atume mhusika,au kibarua wake,au mpambe wake, au id ingine kunaondoa tabia za wabongo? kwa ujumla huo uzito umeondoka km ilivyo kwa documents nyingi bongo. pasco alishaingia, kilichomkimbiza ni nini?promo imebuma?Au kukosea game kumemuudhi mkaa jumba kubwa?
 
huyu ndo pekee alijua nini kimempeleka japo swali halijajibiwa ipasavyo na swali la pili ndo kabisaaa.

MUNGU AMBARIKI KWENYE KAZI YAKE
Mkuu Ichana, Amen, asante, ila kulikuwepo maswali mengine mengi tuu muhimu likiwemo lile la demokrasia, Zanzibar na Udikteta, ila kuna wengi waliokuwa na maswali ya msingi ili hawakubahatika kupata nafasi ya kuuliza.
Paskali
 
Mkuu Chakaza, asante kwa ufafanuzi huu. Watu wengine humu jf ni shida!, kwa kifupi tuna vichaa wengi kuliko tunavyojidhania, ila uzuri mmoja, kuwa kichaa, sio mpaka mtu aokote makopo.

Paskali
JF imeharibika kabisa, sio ile iliyokuwa na mijadala ya kutuelimisha yale tuliyokuwa hatujui, kutufurahisha kwa utani wa hapa na pale tukiwa tumechoka ila sasa ni ya kuudhiana na kukarahishana.
Ila nimegundua baada ya matumizi ya smartphone kuwezesha kuingia mitandaoni inekuwa shida. Vichaa na wehu ambao uwezo wa kumiliki computer binafsi au kutumia ya Ofisi sasa wanaingia tuu JF hata kwa simu ya wizi na kuharibu heshima yetu
 
Paschal Mayala ametutendea haki watanzania.
Lakini Rais ameshindwa kujibu kuhusu katazo la shughuli za kisiasa na hata jibu lake kuhusu uhuru wa mihimili mitatu lilikuwa ni dhaifu sana.
Mkuu Mzee, Thanks, I'm humbled.
Paskali
 
Mkuu Ichana, Amen, asante, ila kulikuwepo maswali mengine mengi tuu muhimu likiwemo lile la demokrasia, Zanzibar na Udikteta, ila kuna wengi waliokuwa na maswali ya msingi ili hawakubahatika kupata nafasi ya kuuliza.
Paskali
Tuliangalia na tumeona juhud zako.jitahid kutumia hekima msafara wa mamba na kenge,nguchiro na mijusi wa kichwa chekundu wapo.tunataman tena itokee na upate chance ya kuitwa tena ikulu.usibishane sana na wachache wasiotambua fani yako
 
Back
Top Bottom