Hongera Spika Dkt. Tulia Ackson. Kuna haja MaSpika wetu iwe lazima kuwa Wanasheria?

Nakuombe kauteuzi hivi karibuni
Ni mawazo finyu kudhani kila mtu anayeisifia serikali ni anatafuta uteuzi!. Mimi nimeisha hudumu kwenye media kwa zaidi ya miaka 30 hivyo kama ni kuisaidia nchi, nimeisha sana bila hata ya uteuzi.

Mama akirudisha mazingira ya kabla 2015, https://www.jamiiforums.com/threads...ika-sasa-ni-zamu-ya-media-ina-suffer.1518514/ watu kama sisi hatuhitaji uteuzi wowote na tutamsaidia Mama kuwalipa mishahara ma DC wake 3, RC 2 na Mkurugenzi mmoja.
Na Ile laana ya JPM iishe
It's true kuna kauli zina powers hivyo zinaumba!, ukiitwa njaa, njaa inakutembelea kweli!, ila pia kuna watu sio mchezo!, ukiwatibua tuu... https://www.jamiiforums.com/threads...nani-kati-yake-na-aliyetoa-kauli-hii.1328562/

Hivyo mimi nami ... https://www.jamiiforums.com/threads...na-kauli-umba-ambazo-huumba-shuhudia.2013308/

Mwisho wa siku, he laughs last, laughs most!.
P
 
Umejitahidi sana, inabidi akuone!! ulijitahidi sana pia kwa top wa awamu ya tano lakini bahati mbaya kabla hajakuona akawa amemaliza kazi na kupimzika!!
 
Masikitiko makubwa sana kwa wakazi wa Liwale kuwa na Mbunge mjinga kama huyu.
 
Nikikumbuka hila Na ghilib za watu wengine jinsi wanavyoupata ubunge huwa nawakinahi watu hao Na kuwakifu hata wafanye jema kiasi gani!

I am sorry to say that!

Sijui sababu ni mwana wa Mungu?!

Yaani huwa napendezwa na haki mno kuliko udhalimu , uzandiki, hila , udanganyifu, ghilib na vya kufanana na hayo!
 



Shukrani hiyo vipi?

Kwani ni hisani au yupo pale kuwajibika na kulipwa kodi ?
 
Leo tena Spika Dr. Tulia Akson, ameonyesha tena ubobevu wa sheria Bungeni, mbunge mmoja wa viti maalum Hanang, amelalamikia mkataba wa mkopo wa matrekta ya Asus katika mkataba na NDC uliohisisha wakulima kukopeshwa matrekta na vipuri

Wakulima wamekopeshwa matrekta lakini hayana vipuri hivyo matrekta yameharibika yako grounded na kushindwa kulipa deni, wanakuwa harassed sana.

Spika akautisha mkataba hapo hapo akaufafanua kisheria, kisha akamuuliza Waziri wa Ulinzi, Innocent Bashungwa atoe maelezo kwasababu matrekta ya Asus yanakopeshwa na Kampuni ya Suma JKT.

Ndipo Waziri Bashungwa akakiri kampuni Mama ya matrekta ya Asus ni muflis hivyo hakuna vipuri. Hivyo Spika akauliza umkopeshe mtu matrekta bila vipuri, trekta limeharibika huyo mkulima atalipa vipi mkopo huo?.

Akamshauri mbunge alipeleke jambo hilo kwenye kamati ili kamati imletee rasmi atoe maelekezo serikalini.

Hili sasa ndio Bunge linaloisimamia serikali,
Hongera sana Spika Madam Dr. Tulia Akson.
P
 
Asanteee
 
Pascal Mayalla , je haudhani kwamba Ili tuwe na maspika wa vigezo hivyo tunahitaji kufanya mabadiliko Ili spika asiwe lazma mbunge. Mfano pale mbeya spika akishindwa kutetea nafasi yake atashindwa kuwa spika. Kuna watu wazuri sana wenye vigezo ulivyotaja ambao wanaoweza kuwa viongozi Bora na wanaoweza KUONGOZA taasis na mihimili vizuri tu, lakini watu hao sio wanasiasa. It's high time tukubali mabadiliko, maspika na mawaziri sio lazma wawe wabunge, wagombee hizo nafasi
 
Spika Tulia amtuliza Dr. Dorothy Gwajima na kumshushua kiungwana na kistaarabu baada ya Waziri Gwajima kuomba muongozo wa Spika na kuruhusiwa akamtaka Mbunge kuondoa maneno ya KE na ME ni maneno ya udhalilishaji wa kijinsia, Spika akaingilia kati kuwa hakuna udhalilishaji wowote na hakutumia kifungu sahihi cha kuomba muongozo wa kumtaja mbunge afute kauli na kumtaka mbunge aendelee kuchangia.

Ukimuondoa Spika Sitta ambaye ni mwanasheria, Spika Tulia ndie Spika wa pili kumkalisha chini Waziri, Spika Tulia pia ni mwanasheria.
P.
 
Naunga mkono hoja kwa asilimia 100% chini ya 100% na niliwahi kushauri https://www.jamiiforums.com/threads...u-kuna-haja-spika-asitokane-na-vyama.1560625/
P
 
Huo ni uchawa tu by any other name!!
 
Wanabodi,

Niko mahali nafuatilia Bunge Live, kiukweli kabisa nimekuwa very impressed na jinsi Madam Spika Dr. Tulia Akson anavyoliongoza Bunge.
Paskali
Nina imani sana na Spika, Dr. Tulia Akson, leo huyu Dada, ataonyesha uwezo mkubwa alionao katika kuongoza mjadala muhimu sana wa Bunge letu kujadili mkataba wa HGA kati ya serikali yetu na kampuni ya DP World ya Mwarabu wa Dubai.

Mijadala kama hii ndio itatufungua macho Watanzania, kwanini Spika Sitta alikuwa Spika bora, na sasa Spika Tulia Akson ni Spika bora!.

Kwa maneno ya rafiki William Malecela (RIP), huwezi kuacha hoja nzito kama za mkataba wa kimataifa wa rasilimali zetu, ukaongozwa na mbululaz!.

Wish all the best Madam Spika, ni maslahi ya taifa mbele!.
P
 
Tatizo lako P unajifanya huwajui wabunge wa CCM na speaker wao hasa kweny masuala ya kupitisha miswada bungeni!! Utasubir san kama unategemea kwenda kinyume pasi kupitisha azimio husika!
 
Nakumbuka uliwahi kumsifia Ndugai kuwa ni spika bora kuwahi kutokea.

Sasa naona umemruka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…