Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala za Kwa Maslahi ya Taifa, makala ya leo ni kuhusu umuhimu wa viongozi wetu na haswa wakuu wa Mihimili lazima sio tuu wawe wasomi, weledi na wachapakazi, bali lazima wawe Bright, brilliant na wabobezi wa fani husika.
Niko mahali nafuatilia Bunge Live, kiukweli kabisa nimekuwa very impressed na jinsi Madam Spika Dr. Tulia Akson anavyoliongoza Bunge.
Hii ndio faida ya kuwa na Spika msomi wa sheria, natumaini wengi unakumbuka uendeshaji wa Bunge enzi za Spika Sitta pia alikuwa ni msomi wa sheria.
Tanzania tunakwama baadhi ya maeneo kwasababu tuna viongozi vilaza!. We can afford kuwa na wabunge vilaza, ndani ya Bunge la JMT but we can't afford kuwa na wabunge vilaza kwenye Bunge la EALA!
Ubunge EALA, Wito Kwa CCM, Msiangalie Ukwasi, Tuteulieni, Wazalendo wa Kweli wa Taifa Hili, Wenye Uwezo na Uzoefu wa Kimataifa Kutuwakilisha Ipasavyo
Ili Tanzania tuweze kupata viongozi bora,, the best of the best, hatuwezi kuuendeleza ule ujinga uliochomekewa ndani ya katiba yetu kiubatili, kuwaachia kakikundi ka watu wachache kuamua huyu ni wenzetu mpe uongozi, hata kama ni vilaza!, na huyu sii wenzetu kata jina tupa kule, hatumuhitaji, hata kama ni the best bright and Brilliant
Hitimisho,
Nahitimisha kwa lile swali, la msingi la makala hii, kufuatia Spika Sitta na Spika Dr. Tulia Akson, ambao ni wanasheria, kuwa so good kwenye uendeshaji wa Bunge la JMT, kwasababu, they are smart, bright & brilliant! kuna haja sasa, kuanzia sasa kuhakikisha MaSpika wetu wote lazima wawe wanasheria?.
Wasalaam
Paskali