Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Infact,
Mnafanya kazi nzuri sana na inaonekana dunia nzima. Kamwe msikubali kuyumbishwa wala kuzingatia matakwa ya wenye nia binafsi, bali zingatieni misingi ya taaluma yenu. Fanyeni majukumu na kazi zenu kwa uhuru, haki na usawa bila mbambamba za mzee au kijana yeyote. Mmefanya vizuri sana kukataa kuburuzwa.
Tunapoelekea maandamano ya Chadema yaliyopigwa marufuku. Tafadhaliini sana, ni muhimu kuripoti na kuuhabarisha umma kila mipango na njama za kila muhusika wa maandamano hayo, ili waTanzania waweze kujua dhima iliyojificha nyuma ya maandamano haya haramu.
Kwa wale wanaochukulia maandamano haya kama fursa ya kupata kibali cha kwenda kuishi uhamishoni ughaibuni, tafadhali sana waripotini ili waTanzania wawajue vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi na wasaliti wa Taifa letu.
Kwa wale waliokusudia kuleta fujo, kupora mali katika maduka na ofisi za watu, na kwa wale waliokusudia kufanya uharibifu wa miundombinu na ofisini za umma nao pia waripotini na kuwaweka wazi, ili wajulikane vyema kwa waTanzania.
Uchu na tamaa ya madaraka kwa ufadhili au usaidizi wa mataifa ya nje, hauwezi kamwe kutugawa na kuvuruga umoja, uhuru, amani na utulivu wa waTanzania. Tutailinda amani na Taifa letu kwa gharama yoyote.
Mungu awabariki sana waandishi wa habari na vyombo vya habari nchini, kusimama Imara kwenye nisingi ya taaluma ya kazi zenu, na kulipambania Taifa, kwa nguvu zenu zote.
Mungu Ibariki Tanzania