OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Utoaji wa Taarifa kwa public mmeiruka?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tupunguze kulalamika..Hii ni vita ya Mtu moja moja..
Hata tuandike magazeti Hapa JF haibadilishi kiti,
cha msingi nunua satinaiza(Sanitaizer), Barakoa wagawie wasio Nazo,
usichoke kutoa elimu ya kujikinga.
Kwamba haya ni marudio.Hivi mtu kama huna cha kuandika si unakaa kimya tu kwani lazima wote tuanzishe siredi
Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu boya ni zaidi ya hopelessNimeona wewe ni hopeless,unaleta masihara kwenye maisha ya watu,huu uzi hauna maana tena
Sent using Jamii Forums mobile app
Ila mkuu kwa covid 19 nchi zote dunia zinatoa briefing update kwa kila kile kinachojiri,ni muongozo toka WHO,inakuaje Tanzania tu ndio iwe shida kwao,covid 19 si ya kuficha.@
Sky Eclat sidhani kama unahitaji kujua idadi ya wagonjwa wa Malaria au STD, same goes to COVID19. Kuhusu oxygen ni sawa, maana huo ni mkakati.
Naunga mkono hoja!Hivi mtu kama huna cha kuandika si unakaa kimya tu kwani lazima wote tuanzishe siredi
Sent using Jamii Forums mobile app
Hiiiiii!Ndukidi hayo mambo ya kupanikishana tuachane nayo, tuweke mikakati ya mass testing ila hakuna mambo ya kutoa taarifa, kwa sababu hatuna briefing ya HIV au Kisukari so why iwe COVID19???? Kwanini tukopy kila kitu?
Je kuna umuhimu wa kutaja maambukizi ya malaria? Cancer??? Au kuna umuhimu wa kutaja vifo vya malaria??? Nadhani mikakati ya kujikinga ni bora zaidi. Tuungane kumpongeza Waziri Ummy kwa hatua aliyochukua
Halafu hawataki kuwa wawazi,wenzetu hii vita wanapambana kwa kuichangia mande,nigeria tayari ana msaada wa madr kutoka china,south africa amepewa madr na serikali ya cuba,serikali yetu inataka kupambana yenyewe kama yenyewe kitu ambacho italy walikuja kukijutia,huu ugonjwa sio kificho kwani hayo mataifa makubwa ndio yanaongoza kwa kuathirika,sie tunaficha kitu gani sijui!Kama wapo wataalamu 8 tu Tanzania nzima wenye uwezo wa kusoma Covid 19 tumekwisha
Sent using Jamii Forums mobile app
Well said mkuu 👏Naipongeza Sekta ya Afya nchini kwa jitihada kuntu inazozichukua katika kukabiliana na mlipuko wa COVID-19 tangu kuingia kwake hapa nchini. Ni wazi wataalam wa Afya wameonyesha "Commitment" itokayo mioyoni mwao huku wakiitendea haki mikataba yao ya ajira katika kipindi hiki kigumu.
Kutokana na majukumu wanayoendelea kuyatekeleza katika kipindi hiki, wataalam hawa hawana budi kujengewa uwezo zaidi ili kuyatekeleza majukumu hayo si tu kwa weledi wa hali ya juu, bali pia kwa ufanisi mkubwa.
Ni wajibu sasa wa Serikali kuchukua hatua zifuatazo;
(i). Kuhakikisha vituo vyote vya Afya nchi nzima vina vifaa/zana za kutosha katika kukabiliana na janga hili.
(ii). Kuwajenga kisaikolojia wahudumu wote wa Afya nchini ili kuwaondolea hofu pindi wanapokabiliana na wagonjwa wa COVID-19.
(iii). Kuwapa motisha ambayo ni nje ya mishahara ama marupurupu wanayoyapata kila mwezi.
Aidha, huu ndio muda muafaka wa kutumia vifungu vya tahadhali na dharura (Miscellaneous and Emergency Iterms) ili kuokoa maisha ya watanzania na si vinginevyo. Ni changamoto kubwa pale Mhudumu wa Afya anapomkimbia mgonjwa akiogopa kuambukizwa COVID-19. Hali hii itasababisha hata wagonjwa watakaougua magonjwa mengine kukimbiwa kutokana tu na hofu waliyonayo hawa wataalam. Nini hatma yake.
Nasubiri kuona Wawakilishi wetu wana sura gani wanapojadili na kuidhinisha Bajeti ya Sekta hii muhimu katika kipindi hiki kigumu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna majengo kama PTA pale saba saba na diamond jubilee,ethiopia wametenga maeneo kama hayo kwa wagonjwa wa coronaWakuu naona wengi tuna criticize badala ya kutoa maoni nini kifanyike. Imefika hatua tunashutumiana, kukashifiana na kutoka nje ya mada.
Nilitegemea tusisitize upatikanaji wa vifaa kinga na tiba (tunaambiwa hakuna tiba lakini watu wanapona). Mfano, kupata vipimo sahihi ni muhimu sana kwa sasa. Hivyo kila hospitali ya mkoa iwe na huduma hiyo. Kuwa na mashine za kusaidia kupumua za kutosha ingawa hata wenzetu walioendelea hiyo ni changamoto, kujenga wodi za dharura hata kwenye viwanja vya michezo, tumeona vilabu Fulani huko Uingereza wamejitolea viwanja vyao vitumike ktk kutoa huduma. Tunao wataalam wa majengo ya dharura au hata jeshi linaweza kutumika. Tuache siasa.
Mtego wa Noti omba msamaha haraka sana kabla sijamwaga mambo yako. Fanya fasterHuyu boya ni zaidi ya hopeless
Hii mikakati haisaidii kama mnaficha data huku mkizika wafu kimya kimya usiku wa manane kama wachawi. Serikali imefeli sana asee@
Sky Eclat sidhani kama unahitaji kujua idadi ya wagonjwa wa Malaria au STD, same goes to COVID19. Kuhusu oxygen ni sawa, maana huo ni mkakati.
Kipengele namba 6 ushauri wangu self isolation ikiambatana na "prescribed medicine" ni nzuri zaidi kuliko kuwaweka watu ambao hawako serious wodini na kutowapa huduma yoyote. Ni vizuri sasa wataalamu wa afya ambay hawajaajiriwa wakapewa mafunzo ili wawe washauri wa watu wanajitibia nyumbani hasa kuhusu dawa za kutumia na unywaji wa maji na vitaminsGreat Thinkers, ujumbe unaofuata unaonesha jinsi wizara ya afya ilivyojipanga kukabiliana na COVID19, kikao alichofanya na chama cha Madakitari (chini ya rais wao Dr Osati) kinatoa matumaini mapya kwa watanzania.
Mrejesho wa kikao cha wanataaluma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Habari za leo
Jana tarehe 27 Aprili, 2020; vyama vya kitaaluma vya afya nchini kikiwemo MAT tulikutana na timu ya Wizara ya Afya kujadiliana kuhusu mwenendo wa wa COVID-19 nchini. Kikao hiki ni matokeo ya mkutano wa vyama vyote wa tarehe 26 Aprili, 2020 kilichofanyika kupitia "zoom ". Tulijadili yafuatayo.
1. Upatikanaji wa PPEs Wizara
Mheshimiwa. Waziri Ummy Ally Mwalimu alisema tayari wameagiza mzigo wa PPEs unaotosheleza matumizi ya mwezi mzima; mzigo huo unategemewa kufika wakati wowote wiki hii. Pia wizara imepata fedha kiasi cha shilingi za kitanzania 9.6Billioni walioielekeza MSD kwa ajili ya kuagiza mzigo mwingine wa PPEs.
2. Wagonjwa kukataliwa kwenye hospitali mbalimbali
CMO na RMOs wameagizwa kushughulikia swala hili mara moja. Hii itaambatana na kuangalia upya mwongozo wa utumiaji wa PPEs bila wafanyakazi kuambukizwa. Sambamba na hilo watumishi wamehimizwa kufuata mwongozo wa IPC ili kuepuka maambukizi na hivyo wasiwakatae wagonjwa wanaopewa rufaa au kuja kwenye vituo vyao.
Kikao pia kiliridhia kwamba mafunzo ya IPC lazima yaendelee kwenye kila kituo cha kutolea huduma za afya. Pamoja na hayo tulikubaliana kuwa isolation centers ziongezeke hata kwenye hospitali za binafsi (private hospitals); kwa kuanzia hospitali hizi kupitia kwa Association of Private Health Facilities in Tanzania (APHFTA) wamekubaliana kutenga isolation za level 3 (level1, 2 and 3) katika kila wilaya ya mkoa wa Dar es Salaam na baadae mikoani, kwa ajili ya kuwaweka wagonjwa.
3. Ucheleweshwaji wa majibu ya COVID-19
Wizara imekubali kuongeza vituo vitatu kati ya tisa zenye uwezo wa kupima COVID-19. Kuanzia Jumanne ya wiki ijayo ya tarehe tarehe 5 May, 2020; maabara ya NIMR Dodoma itaanza kutoa majibu, ikifuatiwa na Mwanza na Mbeya. Changamoto imekuwa ni uwepo wa wataalam wanane tu wa maabara wanaoweza kuchakata majibu ya COVID-19. Kwa hiyo Mafunzo kwa wataalam wengine yameanza na watasambazwa kwenye vituo husika.
4. Mazishi ya waliofariki
Ikitokea mgonjwa amefariki kwenye hospitali, ndugu inabidi wahusishwe iwezekanavyo chini ya uangalizi wa wataalam wa afya kutoka manispaa husika kuhusu mazishi na eneo la kuzikia. Mganga mkuu wa wilaya (DMO) husika ataarifiwe kwa msaada zaidi ikiwa ni pamoja na magari na utaratibu wa mazishi bila kupoteza muda zaidi.
5. Contact tracing
Kwa upande wa Dar es Salaam ambapo tayari kuna maambukizi mengi kwenye jamii ni changamoto kuendelea na kuwatafuata "contacts" na pia ni vigumu kuwa weka wote ‘’isolation’’. Wizara walishauri kwa hatua tuliyo nayo sasa kwa mkoa wa Dar es Salaam kama mtu anahisi kuwa na dalili za COVID-19 aende kwenye kituo husika kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo, na kurudi nyumbani huku wakiendelea kuchukua tahadhari zote ikiwemo kuvaa Barakoa na kujitenga na wengine. Mikoa mwingine ambayo ugonjwa haujasambaa sana waendelee na utaratibu wa "contact tracing".
6. Kuweka wagonjwa wenye dalili ndogo ndogo kwenye isolations
Kuhusu hili tulijadiliana na hatukufikia muafaka. Mheshimiwa Waziri akaomba wanataaluma tujadiliane halafu tumshauri kwenye hili. Maswali yakiwa; Je ni sahihi kuwa weka wagonjwa wenye dalili ndogo ndogo kwenye isolation ambazo tayari zimejaa au tuwape ushauri halafu wajitenge nyumbani mpaka Ikitokea wana dalili za hatari?. Hii itabidi tuitolee maoni sisi kama wanataaluma
7. Upungufu wa Damu salama kipindi hiki
kumeonekana kuna upungufu mkubwa sana wa damu salama katika benki za damu hasa kwa Dar es Salaam. Wito umetolewa kwa hospitali zote kupunguza kufanya/kutoa huduma ya upasuaji usio wa dharura ili kupunguza matumizi ya damu.
8. Utafiti kwenye eneo la COVID-19
Taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) tayari inaendelea na tafiti tatu juu ya COVID-19 na pia imetoa mwongozo wa utafiti kwa wakati huu wa COVID-19. Utafiti pia unahusisha dawa za miti Shamba (tiba mbadala) ikiwa ni pamoja na kujifukiza.
9. Ufafanuzi ya juu ya kauli ya waziri kuwa hakuna watumishi walioambukizwa
Mheshimiwa Waziri alisema alichomaanisha ni kuwa hakuna mtumishi anayehudumia wagonjwa kwenye isolations aliyeambukizwa. Kwa sababu labda walipewa Mafunzo zaidi ya namna ya kujikinga. Alisema anajua kuwa kuna watumishi wameambukizwa wakiwa EMD/Mapokezi na OPDs (idara ya magonjwa ya nje). Kwahiyo ameomba Mafunzo zaidi yaelekezwa kwa watumishi wote.
NB: Tunaomba maoni yenu juu ya kipengela Namba 6 hapo juu.
Nawasilisha
Dr Elisha Osati, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).
Sasa ulidhani watamsikiliza nani huku amiri jeshi mkuu aliepaswa kuongoza mapambano amejificha kijijini. Serikali inaficha habari. Hakuna kitu kinachoendelea huku ndugu zetu wanazikwa kimya kimya usiku.Siku hizi waziri wa afya ni mange na naibu wake ni kigogo.
Hao wanasikilizwa balaa.[emoji16][emoji16].
Sent using Jamii Forums mobile app
Ndukidi hayo mambo ya kupanikishana tuachane nayo, tuweke mikakati ya mass testing ila hakuna mambo ya kutoa taarifa, kwa sababu hatuna briefing ya HIV au Kisukari so why iwe COVID19???? Kwanini tukopy kila kitu?
Je kuna umuhimu wa kutaja maambukizi ya malaria? Cancer??? Au kuna umuhimu wa kutaja vifo vya malaria??? Nadhani mikakati ya kujikinga ni bora zaidi. Tuungane kumpongeza Waziri Ummy kwa hatua aliyochukua