Hongereni sana Yanga SC kwa Ushindi na Kuingia Makundi CAFCC

Hongereni sana Yanga SC kwa Ushindi na Kuingia Makundi CAFCC

Amemzidi aliyekuzaa hilo Tatizo au?
Ndo wewe kabisa, niliwahi ambiwa unacheti cha milembe. Nafaham watu hawakuelewi lakini siyo makosa yako. Unalotatizo la muda mrefu sana. Najua ipo siku tutafahamiana tu kwa hizi id fake za jf
 
Mmecheza mpira mwingi na mkubwa mno huku wachezaji wote wakiwa na ari, nia na uthubutu wa kufanya vyema, na hakika mmekifanya na mmestahili pia.

Hata hivyo mwenyewe tu kimoyo moyo nilikuwa bado natafuta kiini cha ajali ya ndege ya watu majuzi na waliosababisha, kwani kwa ndege kama ile, tena iliyokuwa na marubani wazoefu isingeanguka vile.

Ila leo saa 4 kamili usiku huu nimeshapata msababishi/kisababishi, kwani kwa matukio ya kimaamuzi makafara mazito mazito huwa yanahitajika ili kuleta ufanisi kwa kile unachokidhamiria kusudi usije ukaumbuka.
Hongera ya kinafiki hii! Hatuna shida nayo.
 
1. Acheni kabisa kujidanganya kuwa kwa kuwa Kipanga FC ya Zanzibar alitoka nao suluhu (sare isiyo na magoli) basi hawa wapinzani wenu Club Africaine ya nchini Tunisia mnawaweza na mtawafunga.

2. Dhambi ile ile mliyoifanya kwa Al Hilal FC kwa kuwadharau na kujiona ni wakubwa kuwa mngewafunga ndiyo hiyo hiyo mnairudia tena leo.

3. Kumbukeni hawa Club Africaine hawatokei katika Madafu Premier League yetu Tanzania yenye farasi wakubwa wanne au watano, huku wao na nchi yao wakiwa miongoni mwa nchi kubwa na iliyoendelea sana kimataifa hasa katika mchezo wa mpira wa miguu.

4. Kwa ubovu wa timu ya Kipanga FC ilikuwa ni lazima tu Club Africaine ya nchini Tunisia wabovu kama wao (kipanga) na hivyo watashinda kiuwepesi na hatimaye kuingia makundi ya CAFCL.

5. Mnaoidharau Club Africaine ya nchini Tunisia (kutokana na ujuha wenu) kumbukeni kuwa hawa wenzenu walishafika hadi fainali ya CAFCC je, nyie (Yanga SC) mmeshafika huko walikofika au hata tu kupasogelea?

6. Ninavyowajua Waarabu walivyo makini katika michuano hii ya Afrika watakuwa tayari wameshabeba video za mechi za Yanga SC na timu zingine ili kujipanga zaidi kuwakabili kimchezo na kiufundi. Ila kwa niwajuavyo Yanga SC kwa sasa kipaumbele chao ni udhamini wa UNICEF na kuchanja UVIKO - 19, kuiroga kuifunga Simba SC Jumapili ijayo, kujisahau na ushindi wa ligi nyepesi ya NBC Premier League na ikifika tarehe 30 December 2022 siku tatu kabla ya kukutana na hawa Club Africaine ndiyo Watazinduka na kuanza kujiandaa na wakitolewa kama kawaida, mbuzi wao wa kafara na kichaka chao cha kujitetea kitakuwa ni kumlaumu mwamuzi (refa) kuwa amewaonea.

7. Tayari waandishi wa habari, watangazaji na wachambuzi wa michezo wameshaanza kujipendekeza kwa Yanga SC na kuwa waongo dhidi yao huku wakiwadanganya kuwa Club Africaine ya nchini Tunisia ni nyepesi mno na Yanga SC atashinda tu kote kote, wakati kiuhalisia wana Yanga SC wachache wenye akili wameshakubali kuwa kwa kimataifa Yanga SC anakufa na michuano hii haiwezi.

Endeleeni tu kujidanganya sawa?
Hivi ukirudia kusoma hiki ulichokiandika hapa si utajiona ni mjinga sana!!
 
Hivi ukirudia kusoma hiki ulichokiandika hapa si utajiona ni mjinga sana!!
Nami bado nauliza je, baada ya Yanga SC Kufuzu Makundi ya CAFCC tuendelee kuliita hili ni Kombe la Walioshindwa ( Losers ) au?
 
Ndo wewe kabisa, niliwahi ambiwa unacheti cha milembe. Nafaham watu hawakuelewi lakini siyo makosa yako. Unalotatizo la muda mrefu sana. Najua ipo siku tutafahamiana tu kwa hizi id fake za jf
Nami bado nauliza je, baada ya Yanga SC Kufuzu Makundi ya CAFCC tuendelee kuliita hili ni Kombe la Walioshindwa ( Losers ) au?
 
Hatuna haja na hongera za Makolo,pambaneni na hali zenu[emoji1745]
 
Yani uwakere watu then uje uwasifie ushaona wapiii?? Wapiiii? Ndo maana wengine tunakaza fuvu tuu.
 
Tuache unazi yanga kweny game ya taifa na hii ya Tunisa alionesha kabisa ameanza kupata uzoefu na amebadilika nazan Ile game na Al hilal iliwapa Somo namna gani ya kucheza mechi za CAF na hivi kaingia makundi ya shirikisho Atapata zaidi uzoefu utakao msaidia kweny Champions leauge ni suala la muda tu yanga naye atakua anacheza group stage za ligi ya mabigwa
 
Tuna wapongeza yanga
Ila Wakikuambia Yanga imeweka historia na haijawahi tokea.
Waambie Je wanakumbuka ile historia ambayo haijawahi vunjwa ya simba kupigwa 4-0 ikapindua ugenini kwa 0-5 au wamesahau
 
Back
Top Bottom