Hospitali ya Taifa Muhimbili yafafanua kuhusu video ya Joseph Haule (Profesa J) iliyosambazwa mitandaoni

Haya ni matokeo ya watanzania kupenda umbea, majungu na unafiki. Mange na upumbavu wake wote anajua hadhira yake inataka nini na anawapa wanachokitaka.

Hili limefanywa na mtu huenda kasoma miaka yote ili awe daktari au nesi, tunaamini ana utu na anajua kazi yake inataka nini, ni mpumbavu tu asiyetumia akili yake.
 
Huku ni kukosa kazi na ayo ndo matumizi mabaya ya ofsi na akili yan Watanzania wote leo habari ni pic za profesa tujifunze kufanya kaz tuache uongo
 
Anyway, mwache aendelee kuyamwaga maana si nchi imefunguliwa, mkamtumia na pasi ya kusafiri kabisa pamoja na kupiga picha na Mkulu wakati mmesahau kuwa kichwani kuna nati zake zimelegea, mpaka siku atakapoanza kuwatukana mliopiga nae picha ndio mtajua kuwa yule sista wa US akili hana
 
Tulieni...

Atatafutwa yeyote waseme kakamatwa..

Baadae yanakwisha pole pole... ..
 
Je ICU haina uangalizi kwamba watu wanajiingilia tu na kufanya yao au Madaktari ndio wanafanya haya ?
Nimewahi kufika ICU.

Unaruhusiwa kwenda kumuona mgonjwa huko.

Labda,hao waliopewa ruhusa ya kwenda kumuona ndo wamerekodi.
 
Kwanini mmekuja haraka sana na idadi ya maelfu mnaowahudumia kabla ya kuwachunguza watumishi wenu! Hatuhitaji majibu ya kisiasa kwenye hili.
 
Inasikitisha sana watu wanakosa utu kiasi hicho.
Na hilo lidada lililopost aisee lilaaniwe.
Na kuna mizombie inachekelea tu,inalipia na hela kuona mambo ya kipumbavu.
Hawa wote ilitakiwa wazolewe na kutupwa ndani jumlajumla(kwa sauti ya Mwanri)
[emoji23][emoji23][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]umeandika kwa hisia sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…