Hotuba ya Jenista Mhagama wakati wa mkutano wa WHO Africa huko Brazaville

Hotuba ya Jenista Mhagama wakati wa mkutano wa WHO Africa huko Brazaville

Hii lugha imekuwa mwiba kwetu watanzania...yaani dah!!
Hivi sisi kama taifa, tuchague KIMAKONDE kiwe lugha ya taifa maana kiswahili hatujui na kingereza hatujui.
Mtu anasema "Alusha, arisema atakuja, etc" tupige kura tujifunze kimakonde.
 
Kila mtu ni mahiri katika lugha yake mwenyewe, mbona wamagharibi wànashindwa kuongea lugha zetu hatuwacheki? Je, Waingereza wasomi wote wanajua kuongea kifaransa kwa usahihi?

Lugha ya kiingereza tusiitumie kama kipimo cha ufahamu wa mtu
Mkuu lishauri bunge liondoe kiingereza kama lugha rasmi ya Tanzania.

Kama hujui, hadi muda huu Lugha rasmi za Tanzania ni mbili, kiswahili na kiingereza. Hivyo katika nchi ambayo zaidi ya miaka 9 mtu anajifunza kwa kutumia kiingereza, haitegemewi mtu kwa ngazi ya waziri mtu kutokuwa na ufahamu wa hiyo lugha.

Achilia mbali kuisoma kiufasaha.. Halafu mkuu, mikataba mingi na taarifa za kidiplomasia zinaandikwa kwa kiingereza je, waziri kutokuwa na ufahamu wa lugha. Huoni inaathiri
 
Hii ndo hali halisi ya wapumbavu tulionao.... hao wamekimbilia kujadili kiingereza na naamini hyo hotuba hawajaisikiliza hata!!

Hivi waziri wa Afya unaweza kutoa presentation mbovu hivi? Achilia mbali lugha mbovu hiyo content yake sasa!!

Huyo UCD ndo miongoni mwa kima walioko kwenye corridors of power... amekazania sana ooh English sio lugha yetu utafikiri mkataba wa DP world umeandikwa kiswahili. 🤣
Well said mkuu
 
Wewe siyo mzima.
Kwa hiyo Kiingereza ni utumwa ila Kirusi si utumwa?
Mimi nakakataa kusema kwamba Kiingereza ndio lugha inakufanya uonekane ni msomi na una maarifa zaidi ndio maana nikatoa mifano ya lugha mbalimbali ikiwemo Kirusi, Kichina n.k ambako wanamaendeleo na maarifa zaidi. Nasema slavery mentality kwa mtu anayefikiri Kiingereza ndio lugha inayokufanya uonekane una maarifa zaidi ukitilia maanani sisi tulitawaliwa na Waingereza. Soma bango hapa chini labda utanielewa zaidi.
IMG-20240624-WA0011.jpg
 
Nadhani huwa ina maana kuwa hiyo speech inayohusu jambo husika sio ujumbe wake mfano hapo uawakilisha nchi hivyo anazungumza kwa niaba ya nchi.
Anaingizia neno hilo kuonesha naye personally yupo pamoja naye
Hakunagaa kingereza cha namna hiyo hata kiswahili huwezi sema kwa niaba yangu mimi mwenyewe na wakati tayari upo mahali hapo...amefanya direct translation..yani kaongea kama mtoto wa darasa la tatu
 
Mimi nakakataa kusema kwamba Kiingereza ndio lugha inakufanya uonekane ni msomi na una maarifa zaidi ndio maana nikatoa mifano ya lugha mbalimbali ikiwemo Kirusi, Kichina n.k ambako wanamaendeleo na maarifa zaidi. Nasema slavery mentality kwa mtu anayefikiri Kiingereza ndio lugha inayokufanya uonekane una maarifa zaidi ukitilia maanani sisi tulitawaliwa na Waingereza. Soma bango hapa chini labda utanielewa zaidi.
View attachment 3081720
Hakuna aliyesema kwamba kujua kingereza ni usomi... Huyu waziri amesoma tangu form 1 kingereza mpaka amefikisha masters degree, na bado hawezi kusoma lugha aliyoisoma miaka yote hiyo?? maana yake ni kwamba hata huko darasani alikuwa haelewi anachosoma.. Angekuwa amesoma masters yake kwa kiswahili wala tusingelalamika hapa maana tungejuwa ni lugha ngeni...hata angekuwa ameongea kifaransa tungesema amejitahidi sio lugha anayoifahamu
 
Mkuu lishauri bunge liondoe kiingereza kama lugha rasmi ya Tanzania.

Kama hujui, hadi muda huu Lugha rasmi za Tanzania ni mbili, kiswahili na kiingereza. Hivyo katika nchi ambayo zaidi ya miaka 9 mtu anajifunza kwa kutumia kiingereza, haitegemewi mtu kwa ngazi ya waziri pasipo ufahamu wa hiyo lugha.

Achilia mbali kuisoma kiufasaha.. Halafu mkuu, mikataba mingi na taarifa za kidiplomasia zinaandikwa kwa kiingereza je, waziri kutokuwa na ufahamu wa lugha. Huoni inaathiri
Akikujibu jamaa nistue tuna watu wa ajabu mnooo
 
Hiyo ni slavery mentality tu mkuu. Tembea uone. China, Urusi, Japan, Korea Kaskazini nk. Wanamaendeleo makubwa sana wakati hawatumii Kiingereza. Na kwa taarifa yako nchi ambazo zimejitenga na kiingereza ndio zilizoendelea sana tu lakini nchi zenye kuendekeza utumwa wa akili ndio nchi zilizonyuma kimaendeleo. Mpaka tutakapojitambua ndio tutapata maendeleo ya kweli.
Kwa nini hakutumia Kiswahili??
 
Hizi ndizo tunasema akili za kitumwa. Nenda Urusi kama utafundishwa kwa Kiingereza. Madaktari wazuri hapa TZ ni wale wamesoma Udaktari wao huko Urusi na walitumia Kirusi.
Kwa nini hakutumia Kiswahili??
 
Hiyo ni slavery mentality tu mkuu. Tembea uone. China, Urusi, Japan, Korea Kaskazini nk. Wanamaendeleo makubwa sana wakati hawatumii Kiingereza. Na kwa taarifa yako nchi ambazo zimejitenga na kiingereza ndio zilizoendelea sana tu lakini nchi zenye kuendekeza utumwa wa akili ndio nchi zilizonyuma kimaendeleo. Mpaka tutakapojitambua ndio tutapata maendeleo ya kweli.
Kwa hiyo mkuu, uwajibikaji wa viongozi sio tatizo, wizi na rushwa sio tatizo, elimu na kodi sio tatizo, ukosefu wa ajira umesababishwa na kutumia Kiingereza? Umaskini na mengine yote ni kwa sababu ya Kiingereza? Je, tukitumia Kirusi au Kichina ndio tutaendelea?
 
Hiyo ni slavery mentality tu mkuu. Tembea uone. China, Urusi, Japan, Korea Kaskazini nk. Wanamaendeleo makubwa sana wakati hawatumii Kiingereza. Na kwa taarifa yako nchi ambazo zimejitenga na kiingereza ndio zilizoendelea sana tu lakini nchi zenye kuendekeza utumwa wa akili ndio nchi zilizonyuma kimaendeleo. Mpaka tutakapojitambua ndio tutapata maendeleo ya kweli.
Tunaziita na kujisifu kwa kuinua mabega " COOOOOMOOOON WEALTH "[emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom