Hotuba ya Jenista Mhagama wakati wa mkutano wa WHO Africa huko Brazaville

Hii lugha imekuwa mwiba kwetu watanzania...yaani dah!!
Hivi sisi kama taifa, tuchague KIMAKONDE kiwe lugha ya taifa maana kiswahili hatujui na kingereza hatujui.
Mtu anasema "Alusha, arisema atakuja, etc" tupige kura tujifunze kimakonde.
 
Kila mtu ni mahiri katika lugha yake mwenyewe, mbona wamagharibi wànashindwa kuongea lugha zetu hatuwacheki? Je, Waingereza wasomi wote wanajua kuongea kifaransa kwa usahihi?

Lugha ya kiingereza tusiitumie kama kipimo cha ufahamu wa mtu
Mkuu lishauri bunge liondoe kiingereza kama lugha rasmi ya Tanzania.

Kama hujui, hadi muda huu Lugha rasmi za Tanzania ni mbili, kiswahili na kiingereza. Hivyo katika nchi ambayo zaidi ya miaka 9 mtu anajifunza kwa kutumia kiingereza, haitegemewi mtu kwa ngazi ya waziri mtu kutokuwa na ufahamu wa hiyo lugha.

Achilia mbali kuisoma kiufasaha.. Halafu mkuu, mikataba mingi na taarifa za kidiplomasia zinaandikwa kwa kiingereza je, waziri kutokuwa na ufahamu wa lugha. Huoni inaathiri
 
Well said mkuu
 
Wewe siyo mzima.
Kwa hiyo Kiingereza ni utumwa ila Kirusi si utumwa?
Mimi nakakataa kusema kwamba Kiingereza ndio lugha inakufanya uonekane ni msomi na una maarifa zaidi ndio maana nikatoa mifano ya lugha mbalimbali ikiwemo Kirusi, Kichina n.k ambako wanamaendeleo na maarifa zaidi. Nasema slavery mentality kwa mtu anayefikiri Kiingereza ndio lugha inayokufanya uonekane una maarifa zaidi ukitilia maanani sisi tulitawaliwa na Waingereza. Soma bango hapa chini labda utanielewa zaidi.
 
Nadhani huwa ina maana kuwa hiyo speech inayohusu jambo husika sio ujumbe wake mfano hapo uawakilisha nchi hivyo anazungumza kwa niaba ya nchi.
Anaingizia neno hilo kuonesha naye personally yupo pamoja naye
Hakunagaa kingereza cha namna hiyo hata kiswahili huwezi sema kwa niaba yangu mimi mwenyewe na wakati tayari upo mahali hapo...amefanya direct translation..yani kaongea kama mtoto wa darasa la tatu
 
Hakuna aliyesema kwamba kujua kingereza ni usomi... Huyu waziri amesoma tangu form 1 kingereza mpaka amefikisha masters degree, na bado hawezi kusoma lugha aliyoisoma miaka yote hiyo?? maana yake ni kwamba hata huko darasani alikuwa haelewi anachosoma.. Angekuwa amesoma masters yake kwa kiswahili wala tusingelalamika hapa maana tungejuwa ni lugha ngeni...hata angekuwa ameongea kifaransa tungesema amejitahidi sio lugha anayoifahamu
 
Akikujibu jamaa nistue tuna watu wa ajabu mnooo
 
Kwa nini hakutumia Kiswahili??
 
Hizi ndizo tunasema akili za kitumwa. Nenda Urusi kama utafundishwa kwa Kiingereza. Madaktari wazuri hapa TZ ni wale wamesoma Udaktari wao huko Urusi na walitumia Kirusi.
Kwa nini hakutumia Kiswahili??
 
Kwa hiyo mkuu, uwajibikaji wa viongozi sio tatizo, wizi na rushwa sio tatizo, elimu na kodi sio tatizo, ukosefu wa ajira umesababishwa na kutumia Kiingereza? Umaskini na mengine yote ni kwa sababu ya Kiingereza? Je, tukitumia Kirusi au Kichina ndio tutaendelea?
 
Tunaziita na kujisifu kwa kuinua mabega " COOOOOMOOOON WEALTH "[emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…