Hotuba ya mwisho ya Muamar Gaddafi-aliyosema yametokea!

Wazungu wanawapenda sana wafrica mazuzu kama wewe Wanatamani bara lote la Africa liwe linaongozwa na maraisi mazuzu kama wewe

Na hata siku Moja zuzu kama wewe hauwezi kuwakubali maraisi kama

JIWE
GADDAFI
PUTIN
KIDUKU WA COREA
Kuna kitu naona wengi kwenye huu mjadala hamuelewi.

US ni kweli haikupatana na Gadaffi lakini tusipuuze kwamba wananchi nao hawakupenda udikteta wake. Ni kama tu Huko Saudia wananchi wanakula Bata ila haimaanishi yule Prince Salman anakubalika!! Wana makondo kando kama hayo ya kuua wakosoaji, kukandamiza haki za raia n.k Sasa Leo hii Saudia ikipinduliwa why tulaumu US na NATO?

Hata Mugabe alikua hapatani na West ila haimaanishi ndio waliompindua? Itakua ni mjinga tu atakayepinga kuwa Raia wa Zimbabwe walimchoka Mugabe. Na hii ni kote kuanzia Nkrumah, Haile Selassie, Mubarak, Karume n.k licha ya kufanya maendeleo kwa sehemu Yao but hawakuwa perfect na ndio maana walipinduliwa.

Point ya pili.... Kilichoiharibu Libya sio Gadaffi kupinduliwa ila VITA. Mbona Misri Mubaraka baadae Morsi walipinduliwa ila hatukuona VITA? Mbona Mugabe alitolewa na hatukuona damu ikimwagika? Nadhani ifike mahali tukubali kwamba VITA inaharibu uchumi whether kwa uzuri au ubaya na ndio maana hata uchumi wetu ulivurugika baada ya vita ya Uganda licha ya kwamba Idd Amin alitukosea.

Busara ingekua Gadaffi apishe au aite serikali ya muafaka wa kitaifa Wala NATO wasingepata pa kuingilia wala kusingemwagika damu. Gadaffi mwenyewe ndio aliharibu nchi yake kwa kung'ang'ania madaraka miaka 40 kiasi mpaka kurushia mabomu na risasi raia wake waliompinga kwa maandamano.

Tumeona Gabon, Mali, Burkina Faso Kuna mapinduzi ila mbona hamlaumu wazungu? Kwa sababu hakujatokea damu kumwagika! Sasa kigumu Kilikua kipi kwa Gadaffi kukubali yaishe mapema??
 
Labda Simba wa Africa ya Waarabu
 
Katika mbwa ambao walikufa na Bora walikufa ni pamoja na Mbwa Gadaffi
 
Unamuonaje na Kagame kwa kung`ang'ania madaraka. Naona dunia wakati mwingine inataka watu kujitambua zaidi na sio kuongozwa ongozwa na maono ya mtu mmoja
Kwani mara ngapi Kagame anatajwa na Hao mabeberu kuhusika na mauaji DRC? Kagame is evil and everyone knows it and so was Gadaffi. Sasa ugomvi wake na US usigeuzwe ndio chanzo cha yeye kuondolewa wakati alichokwa na raia wake badala ya kuwaita mezani akaanza kuua waandamanaji mwishowe ikazaa vita badala ya kuadress matatizo akazidi kuua tu ulitaka afanyweje? Hata Kagame akifanya huo upuuzi atatolewa tu.
Toeni propaganda hapa, kwa hiyo Kwa mifano hii kumbe hata Idd Amin alikua Rais mzuri sana maana ndio alitimua mabeberu, alijenga viwanda vingi na uchumi wa Uganda ulikua mzuri sana kipindi chake. Kwa logic Yako ni kwamba Mtu muovu akigawa pesa basi inasafisha maovu anayofanya?

Hii logic ya wapi? Gadaffi was evil and that won't change hayo ya maendeleo wapo madikteta kama Hitler walifanya zaidi yake ila wanachukiwa kwa maovu Yao sio maendeleo Yao.
 
Waarabu hawapendani na wanapenda sana kuua. Kwanini matukio mengi ya vita yanatokea kwenye nchi za waarabu au zenye waislamu wengi?
Sudani, Somalia, Libya, Mali, Syria, Pakistani.
Urafiki huwezi kukusaidia ikiwa wewe mwenyewe hauna upendo na umoja na ndugu zako
 
Si Kweli kama vitu vyengine hujui bora unyamaze tu.

Baada ya Ghadafi kumaliza Tatizo la ajira nchi kwake alichukua Migrants kibao wengi kutoka Nchi kama Niger, Chad, Nigeria etc. Jumla Libya ilihifadhi migrants kama milioni 2 na nusu wakati wa Ghadafi


Pia Libya sio weusi asilimia 97 ni waarabu na berbers, weusi unaowaona Libya wapo Njiani kwenda Ulaya.
 
Vikundi hivyo hivyo mnavyosema ni vya Kigaidi wame kuja Wagner wamevipiga, Ufaransa katolewa hizo Nchi na Vikundi vimepotea. Muda ni Mwalimu mzuri sana, Vision ya Ghadafi ndo hiyo hiyo Inatokea Niger sasa hivi.
 
Mkuu una Ignore vitu vingi kwenye Comment yako.

1. Raia wa Libya wengi tu walimsupport Ghadafi, tulionao maandamano makubwa Mno ya kumuunga Mkono Ghadafi,



2. Sababu wengi walimsupport Ghadafi ikawa nguvu ya Wananchi haiwezi kumtoa Madarakani ikabidi itumike nguvu ya Kijeshi kutoka Nje, Ghadafi hajapinduliwa na wananchi tu bali Nato alihusika kwa kiasi kikubwa zaidi.

3. Lengo la Magharibi sio Demokrasia bali ni kumuweka Kiongozi wanaotaka wao, Chukulia huo huo mfano wa Misri, walipoitisha Uchaguzi Mosri si alishinda? Mbona west wakamtoa kiongozi aliechaguliwa na wananchi?

4. Libya aliefanya vita viendelee zaidi ni hao hao Nato, wamewaweka waasi waongoze nchi baada ya kuwasaidia waunde serikali Nato wakaanza kusupport waasi wengine, in short hawana nia ya kui stabilize Libya, kama Ilivyo China, Iran, Urusi hawataki Nchi ambayo ipo against na wao iwe na Maendeleo.
 
Dohhh pole sana .. umetolea mfano wa misri ivi unajua Abdulfatah Al sis ni kibaraka wao na ndio walimtumia kumpindua Mohamed mursi Rais aliyependwa na Raia kwakuwa alkuwa threat Kwa Israel na USA ndio mahana wakamtoa Kuna madikteta kibao tu apa Africa kwakuwa ni vibaraka wa west hutosikia wanawasema vibaya
 
Kuna madikteta kibao tu apa Africa kwakuwa ni vibaraka wa west hutosikia wanawasema vibaya
Issue ni kuwasema au mnasubiri wapinduliwe ndio mseme wamehusika?

Kwani Gadaffi hawakumsema miaka yote mbona hawakuwahi muua? Ila wananchi walipoamua kukianzisha ndio lawama kwa wazungu.

Tuache inferiority complex
 
Kupiga marufuku boxing ungetoa mfano wa hapa karibu, AA Karume.
 
Mbona wafalme, familia na koo zao zinatawala muda mrefu kama vile nchi ni mali yao binafsi
Libya ilikuwa nchi ya kifalme pia, Gaddafi akampindua mfalme 1969 halafu akajifanya mfalme yeye mwenyewe!
 
Raia wa Libya wengi tu walimsupport Ghadafi, tulionao maandamano makubwa Mno ya kumuunga Mkono Ghadafi,
If this was the case wangebeba silaha wampambanie Gadaffi!! Sasa unasema alikua na wafuasi wakati numbers zilimzidia kwenye uwanja wa vita.
2. Sababu wengi walimsupport Ghadafi ikawa nguvu ya Wananchi haiwezi kumtoa Madarakani ikabidi itumike nguvu ya Kijeshi kutoka Nje, Ghadafi hajapinduliwa na wananchi tu bali Nato alihusika kwa kiasi kikubwa zaidi
Waandamanaji walianza kuuwawa na baadae Gadaffi akaanza kutumia ndege kupambana na waasi. Akawa analipua Ile miji ya kipinzani na hapo ndio NATO ikaingilia tena ilishapita miezi zaidi ya 6 Toka vita vingurume. So Gadaffi ndio aliyeanza kulipua nchi yake mwenyewe na kuua maelfu ya raia.

3. Lengo la Magharibi sio Demokrasia bali ni kumuweka Kiongozi wanaotaka wao, Chukulia huo huo mfano wa Misri, walipoitisha Uchaguzi Mosri si alishinda? Mbona west wakamtoa kiongozi aliechaguliwa na wananchi?
Lakini Morsi aliondolewa na raia baada ya kuanza kuleta siasa kali za Islamic Brotherhood. Kama hao US wanataka vibaraka wao mbona hawakumtetea Mubarak alipopinduliwa na wananchi?
Sio kweli nchi yoyote baada ya vita huwa Kuna ombwe la uongozi hata Nyerere alipomtoa Amin tuliona jinsi wahuni walitawala na vikundi vya waasi vikajaa Kila kona. Hayo ni madhara ya vita yoyote Ile hata Ukraine ikimshinda Russia tarajia makundi ya waasi kuibuka na kujitawala Sasa hiyo inahusiana vipi?

Baada ya hapo rejea mapinduzi ya Gabon, Burkina Faso, Mali, Zimbabwe n.k why huko hatujaona mabomu, magofu, au vita? Sababu watawala walikubali matokeo na kukaa pembeni ila Gaddaffi tamaa ya madaraka akaona kuliko kupisha Bora apigane vita mpaka mwisho na ndio imeiharibu LIBYA.
 
Vikundi hivyo hivyo mnavyosema ni vya Kigaidi wame kuja Wagner wamevipiga, Ufaransa katolewa hizo Nchi na Vikundi vimepotea. Muda ni Mwalimu mzuri sana, Vision ya Ghadafi ndo hiyo hiyo Inatokea Niger sasa hivi.
Hii nayo huwa hoja nyepesi sana, mara zote humu mnasema vikundi vya kigaidi vinapandikizwa na wazungu Sasa Cha kujiuliza kwani hao wazungu huwa hawana mikataba halali ya kuchimba madini katika hizo nchi??

Mfano kule Msumbiji kwenye gesi wakasema ooh wazungu ndio wameleta magaidi Ili waibe gesi. Cha ajabu wafaransa ndio walikua na kampuni zao za kuchimba gesi Sasa why ulete vita au magaidi ilihali gesi umeshapewa?

Hii hoja sijawahi ielewa, huwa mnaitumia DRC pia ilihali hao hao mabeberu Wana mikataba halali why Tena waingie gharama ya kufund waasi wakati Mali tayari wamekabidhiwa? Yaani what are they fighting for?
 
Gaddafi alikua muslim propagandist na mfadhili mkubwa wa vikundi vya kigaidi,ndiye aliyemfadhili Iddi Amin katika vita vya Tz na uganda.

Wananchi wake walimchoka kwa udikteta ndio mana walimuua kafiri yule.
Kama alikuwa mfadhili wa Vikundi vy kigaidi Mbona Amefariki na Hivyo vikundi bado vinaendelea kuwepo na Kufadhiliwa,

Je nani anyeendelea kuvifadhili vikundi hivyo au ni Mizimu ya Gaddafi inavifadhili ?
 
1. Si maeneo yote wana mikataba halali
2. Wanachukua zaidi Ya kilichoandikwa kwenye mikataba.

Mfano sasa hivi Syria Usa wanachimba mafuta, Hawajaingia mkataba wowote na serikali ya Syria na issue ipo UN ila inafunikwa funikwa.

Na hii issue ya West kufund hivi vikundi mbona sio siri tena? Nakupa mifano ya uhakika Kampuni za west zikikiri kutoa hela.

1. Lafarge Kampuni ya Cement Ufaransa ilitoa mabilioni na kuwapa Isis

2. Ericsson wameshtakiwa na investors wao wenyewe baada ya internal document kuleak walikua wanafund IS na scandal nyengine za Corruption Iraq

3. Mwandishi wa habari wa Bulgaria Dilyana alileak silaha za zaidi ya Dola za kimarekani Bilioni 2 ambazo Usa wamezinunua na kusupply kwenye Conflicts zone na kuwapa vikundi vya magaidi, Ana ushahidi wa serial no, vilipotengenezwa silaha, zilipokua supplied etc.

Ushahidi upo mwingi mno, kama lengo ni kujua naweza kuendelea na huu ushahidi.

Ingekua source of fund ni Ghadaffi alipokufa hivi vikundi navyo vingepotea, ila viliendelea strong hadi Wagner alipoingilia.
 
How comes he said he lived in modest house and tents?what about his palace?am getting confused 🤔🤔🤔🤔

NB:He was among my favorite African leaders.
 

Attachments

  • Screenshot_20230920-115048.jpg
    55.6 KB · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…