Mkuu una Ignore vitu vingi kwenye Comment yako.
1. Raia wa Libya wengi tu walimsupport Ghadafi, tulionao maandamano makubwa Mno ya kumuunga Mkono Ghadafi,
View attachment 2755340
View attachment 2755341
2. Sababu wengi walimsupport Ghadafi ikawa nguvu ya Wananchi haiwezi kumtoa Madarakani ikabidi itumike nguvu ya Kijeshi kutoka Nje, Ghadafi hajapinduliwa na wananchi tu bali Nato alihusika kwa kiasi kikubwa zaidi.
3. Lengo la Magharibi sio Demokrasia bali ni kumuweka Kiongozi wanaotaka wao, Chukulia huo huo mfano wa Misri, walipoitisha Uchaguzi Mosri si alishinda? Mbona west wakamtoa kiongozi aliechaguliwa na wananchi?
4. Libya aliefanya vita viendelee zaidi ni hao hao Nato, wamewaweka waasi waongoze nchi baada ya kuwasaidia waunde serikali Nato wakaanza kusupport waasi wengine, in short hawana nia ya kui stabilize Libya, kama Ilivyo China, Iran, Urusi hawataki Nchi ambayo ipo against na wao iwe na Maendeleo.