Hotuba ya Pieter Willem Botha aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini ya Makaburu

Hotuba ya Pieter Willem Botha aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini ya Makaburu

Duh...hii balaa. Lakini je anaweza kuwa sahihi hapa chini? Hasa ukiangalia mikutano ya kikwete na watu wanavyojipanga huku? Pia hili swala zima la ufisadi hasa ukiangalia watu kama Chenge? Na pia hizi takrima wakati wa uchaguzi?

"Secondly, most Blacks are vulnerable to money inducements. I have set aside a special fund to exploit this venue. The old trick of divide and rule is still very valid today. Our experts should work day and night to set the Black man against his fellowman. His inferior sense of morals can be exploited beautifully. And here is a creature that lacks foresight. There is a need for us to combat him in long term projections that he cannot suspect. The average Black does not plan his life beyond a year: that stance, for example,should be exploited."

Sehemu kubwa ya hiyo hotuba ni UKWELI, hiyo mikakati yake kwenye palagraph nne za mwisho ndy balaa lilianzia hapo!...hawa jamaa ni k**anyoko sana!
 
Botha anastahili ukiranja kwenye himaya ya mashetani.
 
Mwanzoni hotuba ina mtiririko makini unaoweza kuaminika lakini mwishoni ni kama mletaji ameongeza manjonjo. Pamoja na yote, ukiondoa wachache waliojipambanua au wanaojipambanua kuwa watu wa kipekee wasioyumbishwa na tamaa ya utajiri uchwara na burdani za kibwege, mtu unaweza kabisa kukubali kwamba mtu mweusi ana matatizo ya asili ya kupoteza mwelekeo wa mustakabali wake.

Sijui ni nchi ipi inayoongozwa na watu weusi tunaweza kuipigia mfano na kujivunia uongozi wake? Inatosha kutaja Botswana ambayo nayo chama tawala ni kilekile tangu uhuru?
 
Wakati mmoja nilijadili hii makala na raia mmoja wa kutoka Afrika kusini (mzungu raia wa SA lakini asili yake ni Uingereza, sio Udachi), na alinieleza kuwa makala haya ni ya bandia, na ilitungwa na wazungu wa kiasili ya kiafrikana ili kwelekeza lawama yote ya mfumo ubaguzi wa rangi kwa huyu Mbeberu Botha ili wajisingizie sio wote waliounga mkono ubaguzi; ni watu ti wachache waliokuwa kwenye mamlaka, kama vile Botha, Vorwoed na pengine Jan Smuts
 
I am speechless,

Kama hii speech ni ya kweli (na uwezekano ni mkubwa kuwa ni kweli) basi inábidi tujiangalie upya. Kuna mambo mengi ni ya kweli kwa jinsi waafrika tulivyo walafi wa ngono, pesa na starehe nyingine za kijinga jinga.

Haaaa, ngoja na uitwe ubaguzi wa rangi kwani kama jamaa alikuwa na hiyo mikakati basi ni mtu hatari kuliko shetani!
 
Kuna mambo ambayo Botha ameyaongea humo kuhusu waafrika ukiaangalia in one way or another kuna baadhi ya mambo ni kweli pamoja na kuwa jamaa alikuwa na evil mind dhidi ya waafrika ambayo sijapata kuona na by that time ubaguzi ulikuwa kwenye climax stage lakini pamoja na yote unapoaanza kusoma habari hii mwanzoni kuna fikra fulani unazipata lakini unapozidi kuendelea kuisoma kuna vitu vingine kama vile mwandishi ameongeza chumvi
 
walijisahau kuwa wataondoka madarakani siku moja, naona hili halikuwa kwenye akili zao. Kama wanavyojigamba wengine kuwa hapajawa na mtu mwingine wa kuweza kutawala zaidi ya mafisadi.

Hawajui nguvu ya umma, wanaweza kutumia pesa ila kwa muda,wanaweza kudanganya ila kwa muda. Waelewe hivyo na si vinginevyo
 
Hakuna mtu mjinga anayeweza kutoa speech hii. wala tusiumize vichwa. hata kama mtu anaweza kuwa na ubaguzi wa ajabuajabu kama huuu kwenye hii document, hakika yake atafanya kisirisiri tu, hatafanya waziwazi kiasi hicho, hata vitani, utunzaji wa siri ni kitu muhimu, na kama unayo strategy fulani, kutunza siri ni kitu muhimu, kama alikuwa na strategy mbaya kiasi hicho, si rahisi kuiweka waziwazi, angeiweka kisirisiri.

Siiamini hii speech, naona ni product ua politics na uzushi tu.
 
Hii Familia ya Magazeti ya NewHabari sasa waandishi wake wanaongelea Matatizo wanayoyaona sasa hivi nchini, nadhani walikuwa wamelala, wanahoji Uongozi Sio Imara wa CCM; 2015 Jibu ni CHADEMA

http://www.newhabari.com/2011/05/11/tanzania-bado-kuna-wenye-fikra kama-pieter-botha/#respond

Na Conges Mramba, Musoma

KATIKA uhai wake, Kaburu Pieter Botha, aliwahi kusema:

“Mungu ninaye mwamini ni mkuu kiasi kinachotosha kuwa Mungu wa watu wengine!”

Alitetea nguvu za Jeshi imara la Afrika Kusini, lililokuwa na nguvu kuliko majeshi yote Afrika kuilinda Katiba iliyokuwa ikitetea maslahi ya Wazungu ambao wakati huo walikuwa asilimia takriban sita tu, ya idadi ya watu wote Afrika Kusini.

Kaburu Botha, aliamini kuwa mtu mweusi, asilani hawezi kutawala nchi, ikawa na maendeleo, ikawa na amani, ila kuchinjana, dhuluma inayotokana na ufisadi uliotamalaki, pengine na ubaguzi!
Ni kauli mithili ya Dk. Watson, dhidi ya Mwafrika; kwamba hawezi kujitawala na kujiletea maendeleo; kwa hiyo eti Mwafrika hakustahili kuwa huru milele?

Wapo Waafrika wengi, na wamesoma, lakini wanaamini kuwa Mwafrika hawezi kujitawala, ndiyo maana tangu uhuru Afrika ni bara la umasikini, vita na njaa.

Alitabiri hata vita Afrika nyakati za amani.


Naam, wakati anafariki Jumanne, Oktoba 31, mwaka 2006, unabii wake ulikwisha timia; Afrika ikiwa inagugumia ukoloni wa aina yake, kiasi cha watu wengine kudhani, “Mungu wa Pieter Willem Botha, aliyemsukuma kutumia jeshi lenye nguvu kuendesha ubaguzi wa rangi Afrika, ni wa kweli, na bado yupo!”

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, alikuwa bado kifungoni enzi za utawala huo wa Botha, Rais wa kwanza Mtendaji, Afrika Kusini.

Mandela, aliyeswekwa kizuizini tangu mwaka 1964, alikuja kupigiwa kura Aprili 1994, takriban miaka mitano baada ya Botha kuondoka madarakani, akaja kuwa Rais Mzalendo wa taifa hilo lenye bendera ya rangi ya upinde wa mvua.

Hili ni somo la kwanza kwa viongozi wa bara hili kwamba; Mungu wa Botha awe amekufa, au bado yu hai, wapinzani wa serikali iliyoko madarakani hufika muda wakaaminiwa na umma kushika madaraka ya nchi, kama haki haitendeki.

Mandela alikuja kuachiliwa huru na De Clerk, Feburuari 1990.

Kwa Mandela, uhuru binafsi toka gerezani haukuwa jambo la msingi kuliko uhuru wa Waafrika waliokuwa wakibaguliwa katika nyanja zote, na hivyo kuendelea kuwa duni kulinganisha na Wazungu, Wahindi, Waarabu na watu wengine.

Licha ya Makaburu kutangaza kuwa Afrika Kusini ilikuwa nchi huru toka mikononi mwa Waingereza mwaka 1961.
Mandela alikataa alipopewa nafasi ya upendeleo kwa kupatiwa uhuru, akakataa kutoka gerezani. Aliona ni heri abaki jela kuliko kupewa uhuru bandia wenye masharti kwamba asijishughulishe na harakati za ukombozi zilizoitwa na Makaburu, ‘violence.’ Yaani, kwa Makaburu harakati za Mwafrika kujikomboa ilikuwa ni machafuko, na ilikuwa kinyume cha ‘Mungu’ wa akina Botha!

Mandela alikataa uhuru aliopewa na Marehemu Botha.

Nasi leo Waafrika tunapoadhimisha miaka 50 ya uhuru tuliopewa na mkoloni, wakati bado kuna vita vinavyoendelea katika baadhi ya nchi za Afrika kama Libya na mahali pengine ambavyo tunaweza kuviita ‘vita vya maslahi ya Wazungu.’

Uhuru tulipata hauwaruhusu walio wengi kujiamulia mambo yao wenyewe, bali ni ule uliokuwa ukiruhusu Wazungu wachache kuneemeka zaidi wakati wengi wakitengwa na kuonwa kama majambazi katika nchi yao wenyewe!

Mandela, hakuwa tayari kupewa kazi au cheo chochote ‘bandia’ na Wazungu, wabaguzi wa rangi wa Afrika Kusini, wakati maslahi ya weusi walio wengi yakikanyagwa chini kwa ridhaa ya ‘miungu’ ya akina Botha.

Hakuwa tayari kupewa rushwa ya ‘nafasi nzuri’ kulinganisha na watu wake. Maisha yake hayakuwa kitu cha thamani kuliko ya watu wake.

Utajiri kutoka kwa mabeberu haukuwa chochote kwake, zaidi ya unyama, usaliti, ushenzi na kutokuwa na msimamo kwa watu wake.

Mandela aliyefunguliwa kesi na utawala wa Makaburu Oktoba 9, 1963, alikubali kukosa raha za kitambo hadi watu wake wote watakapokuwa huru kujiamulia mambo yao wenyewe, bila kujali kama ingefika siku jeshi bora la Makaburu lingedhoofika, wanaharakati, weusi wakasimika bendera ya uhuru.

Kwa viongozi wazalendo wa ‘matumbo yao wenyewe,’ watoto wao na jamaa zao, roho ya Mandela katika utawala imara wa akina Botha, ulikuwa ujinga!

Botha, aliyefariki miaka minne iliyopita, alizaliwa kijijini katika Jimbo la Orange Free State, Januari 12, mwaka 1916.

Katika umri wa miaka 20 alikwisha hamasisha wenzake katika harakati za chama cha National.
Miaka 12 baadaye, yaani mwaka 1948 aliingia bungeni; na akapewa uwaziri.

Mwaka 1976 alikuwa Waziri wa Ulinzi kwa miaka miwili, mwaka 1978 alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu, na baadaye Rais Mtendaji wa Afrika Kusini, Septemba 1984 hadi 1989 alipomwachia De Clerk.

Wakati wa utawala wa Botha, angalau katiba ilianza kutambua uwakilishi wa rangi mbalimbali, wakiwamo weusi, hususan bungeni ambako hata hao weusi waliwakilishwa kikabila.

Kwa kiasi kidogo Botha alikataa jamii za watu weupe wa Afrika Kusini kujiona wateule kuliko weusi.
Hili ni somo kwa viongozi wa sasa wa Afrika, waliojigeuza watawala, kuacha kujenga matabaka katika nchi.

Siku hizi matabaka yanaonekana dhahiri kwa rangi kwa cheo, kwa walio nacho-mabwana na watwana!

Matabaka ya walionacho na wasio nacho. Watawala na watawaliwa.Walanchi, wananchi na wenye nchi!

Siku zote watawala hujiona daraja la kwanza, matajiri daraja la pili, na walalahoi ambao ndio wengi katika nchi husalia watu wa chini wasio na mtetezi.

Kama alivyofanya Botha, na wenzake waliomtangulia, baadhi ya watawala wa Afrika huthubutu kutumia jeshi kuua raia wanapoamka kupinga uonevu na unyang’au sawa sawa na unyama wa Afrika Kusini enzi za mauaji ya SOWETO, na hata mauaji ya wazalendo kama Chris Hani, na wenzao lukuki.

Mwaka 1984, Botha aliondoka kutafuta uungwaji mkono kwa mataifa ya Magharibi, lakini akakataliwa kwa sababu ya siasa za kibaguzi.

Leo Afrika inao viongozi kama Botha, kasoro rangi, lakini wabaguzi, watesaji wa raia wao; wanaowapendelea wageni na matumbo yao, ndugu na jamaa zao, lakini wanapofika huko Ulaya na Marekani hutandikiwa zuria jekundu na kuidhinishiwa misaada!
Iko wapi roho ya mataifa iliyoiwekea vikwazo Afrika Kusini enzi za akina Botha leo?
Kwa nini wanaowabagua raia wao katika nchi yao wenyewe, wasibaguliwe na Jumuia za Kimataifa na kunyimwa misaada leo?

Leo viongozi huwekewa ‘Bingo’ ya mamilioni ya dola za Bwana Mo Ibrahim, pindi wamalizapo mihula yao kwa kutekeleza utawala bora, wakati ni wajibu wao!
Kila Rais wa nchi huapa kufanya yaliyo mema kwa raia wao wakati wa utawala wao, sasa ‘rushwa’ kutoka kwa Mo Ibrahim za nini?

Nani alisema anayetimiza wajibu apewe zawadi?
Rushwa hutolewa kwa viongozi ili wawatendee raia wao mema?
Si kwamba kuwatendea mema raia ni wajibu; na ni haki kiongozi kutekeleza wajibu, haki na utawala bora kwa watu wake?

Kwa nini kuweka bingo kwa watawala wanaokula rushwa ambao ni wabaguzi sawa na akina Botha, wakati Botha alipokea vikwazo kwa mataifa?

Niliwahi kupokea ujumbe mfupi wa maandishi kutoka kwa mmoja wa wasomaji wa gazeti hili uliosomeka; “katika nchi zetu, raia wamegeuka mateka wa mfumo ‘twawala’ hadi mategemeo na jukumu la uhuru vimeachwa mikononi mwa vyombo vya habari, na si kwa viongozi mithili ya Nelson Mandela!”

Kwa mawazo ya wasomaji wangu kama huyu, japo Mandela yu hai na amemzika Kaburu Botha, lakini atakapokufa, Mandela ataondoka na roho yake.
Hakuna tena akina Mandela, Julius Nyerere, Kwame Nkrumah, Gamal Abdel Nasser, Patrice Lumumba, na Samora Machel.

Viongozi waliobaki ni ‘Makaburu’ waliojivika koti la ‘vyama twawala’ vinavyowaweka vigogo wake daraja la kwanza, wageni na matajiri daraja linalofuata, huku wakiwabagua na kuwanyanyapaa raia waliobaki!

Kama nasema uongo, mbona vigogo watoto wao wanasoma shule za kimataifa – nje ya nchi, wakati watoto wa masikini wanasoma shule za kata zisizo na walimu na miundombinu?
Ni kama madai yale yale ya watoto 250 waliouawa Soweto (South West Township) Afrika ya Kusini mwaka 1976.

Katika uongozi wa awamu ya nne, Rais Jakaya Kikwete, ameahidi kuondoa matabaka haya na kuleta ‘Maisha bora kwa kila Mtanzania.’

Swali linaloulizwa ni Je, Watanzania wote watakula ‘matunda’ ya CCM, ifikapo 2015 au tutaambulia majani na mizizi ya sumu?

Watanzania leo wanaomba kupata viongozi shupavu kama Waziri Mkuu wa zamani wa Singapore, Lee Kuan Yew, alivyowalinda watu wake kutoka katika Dunia ya tatu hadi ya kwanza .
Watanzania wanamtaka Rais Jakaya Kikwete, amuige Lee Kuan Yew, ili mambo yaende!
Kinyume cha haya tutakuwa tukitimiza unabii wa Botha, kwamba Waafrika tukipewa madaraka, hatuwezi kujitawala, badala yake tutaishia kuuana, kujilimbikizia mali, au kung’angania madaraka!

Pengine unabii wa Marehemu Botha ulikwisha timia. Ama – unatimia.
Tumeona watawala wa Afrika kama akina Mobotu, Idi Amini, Sani Abacha na wengine wakiwaua raia wanaopinga utawala wao ili wabakie madarakani milele.

Tawala zao ziliandamana na ufisadi licha ya unyama, na ubaguzi wa matabaka, huku ndugu zao wakitajirika kwa muda mfupi sana kwa fedha walizopata kwa njia za magendo na rushwa, na kuzificha huko huko kwa hao wanaoimba wimbo wa utawala bora Afrika!

Kulingana na kauli za wasomaji, viongozi wetu wanapaswa kumpinga Kaburu Botha, kwa vitendo, kwa kuendesha utawala bora kwa vitendo, ‘to walk the talk’ na wala si kwa vishawishi kutoka kwa matajiri, kama Mo Ibrahim kwa ahadi ya kitita cha dola za Marekani, wanapostaafu.

Watanzania wana maoni kuwa Tanzania inao Watanzania bado; ila wamekuwa wakibaguliwa na mfumo wa waliobahatika kuingia madarakani kwa njia za rushwa, ambao hutumikia zaidi njaa zao kuliko raia wanaowaongoza.

Watanzania sasa wameanza kuhoji uzalendo wa viongozi: Kwamba kwa nini wauze mashirika ya umma kitapeli?

Kwa nini mikataba hewa? Kwa nini kuuziana nyumba za umma kindugu, kwa madai kuwa ni ‘sera’ ya chama chenu?

Watanzania wa leo wanamtaka Rais Kikwete kufanya mapinduzi makubwa ya kuondoa ubaguzi mamboleo ili kuwaondolea mbali viongozi magaidi waliojipenyeza katika utawala wa nchi.
Kama, Mandela alivyojitoa mhanga kuikomboa Afrika Kusini, Tanzania inawahitaji akina Mandela watakaozika fikra za akina Botha.

Vinginevyo utabiri wa Kaburu huyu utakuwa kweli kwamba, viongozi wa Bara la Afrika hawana cha kuwafanyia watu wao, ila kuwabagua, kuwaua na kula rushwa!
Ilifika wakati utawala wa makaburu uliokuwa na jeshi imara, ukapisha mabadiliko kwa walio wengi kujitawala wenyewe.

Makaburu mamboleo waliojipenyeza katika tawala za Afrika, iwe kimwili au kiakili, wanapaswa kupisha utawala wa watu na watu kwa ajili ya watu!

Anapozikwa Botha, wazalendo wa bara hili wanapaswa kupinga unabii wake ili viongozi wawe watumishi badala ya wachuuzi wa watu wao, ambao hawana tofauti na magaidi!
Je, Botha kafa na roho yake, ama roho bado ipo, au bado kuna Makaburu wengine?
Je, iko wapi roho ya akina Mandela, Nyerere na Lee Kuan Yew?
 
Makuaburu weisi? Duh wapo wengi. Sasa Kenya, Zambia, Malawi, Botswana, RSA, DRC, Rwanda, Sudani Kusini, Ivorycoast tayari. Zimbabwe, Misri, Tunisia, karibu zinapata afya. Zimbabwe, Tanzania, Uganda bado wezi wa kura. Ila inaonekana kati ya sasa na 2015 kuna mambo mazito.:israel:
 
Moja ya kauli ya kaburu Botha wa Afrika Kusini karibu mwishoni mwa utawala wa kibaguzi kusambaratika, alisema nukuru inayofuata:

"By now every one of us has seen it practically that the Blacks cannot rule themselves. Give them guns and they will kill each other. They are good in nothing else but making noise, dancing, marrying many wives and indulging in sex. Let us all accept that the Black man is the symbol of poverty, mental inferiority, laziness and emotional incompetence
And here is a creature that lacks foresight. There is a need for us to combat him in long term projections that he cannot suspect. The average Black does not plan his life beyond a year."


Kauli hii ukiiangalia kwa makini je, kuna ukweli fulani au tumwelewe alikuwa na dharau kwa Waafrika? Ni matatizo gani yanayosababisha nchi nyingi za kiafrika kutopiga hatua za kasi kimaendeleo licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa mali asili? Ni ukweli kwamba watu weusi wakishapata nafasi huishia kufurahia maisha ya anasa, kuoa wake wengi na kujihusisha na ufuska? Ni kweli tu wavivu? Hatuna upeo wa kuona mbali?

Wakati nilipoku shuleni, na vyuoni na kazini nchini mwangu kabla sijatia mguu nchi zilizoendelea niliridhika na hali tuliyo nayo na kufikiria walioendelea wamebahatika, na nikifika huko nitajifunza wamebahatikaje huenda wana ardhi ya kuaminika kuliko ardhi yetu ya kusadikika. Cha ajabu baada ya kutia mguu tu nikaona afadhali ya ardhi nilikozoea kula organic food, na kuchuma mapera fresh tangu nilipoanza kupata akili ya utambuzi. Nikajiuliza ni nini kilichoturudisha nyuma? Biashara ya utumwa? Ubunifu wa ushindani kimaendeleo? Kuridhika na hali tuliyo nayo? Kutanguliwa kimaendeleo kumetupumbaza? Na mengine mengi sipendi kujaza nafasi mode asije nimute. Katika kupembua kuna mengi tu aliyosema Kaburu Botha ni ya kuaminika ingawa si vizuri kuanika hapa mifano hai.

Viongozi wengi wa nchi za Kiafrika hawaongozi nchi zao kwa mtazamo wa kiuchumi ila kuonekana wanajishuhulisha, Rais atasafiri kwenda nchi za nje kutafuta misaada, gharama za safari yake zinazidi msaada atakaopata huko. Kumbuka rais anaposafiri ni gharama kubwa ikiwa ni pamoja maandalizi ya safari yake kabla hajaenda katika nchi husika, wajumbe wanaoandamana naye na watumishi inakuwa kati ya 30 -40 na bado kuna baadhi wanaotangulia kwa usafiri mwingine. Posho ya rais, wajumbe, na gharama za kuishi hotelini na usafiri utaona bora asingeenda kuomba msaada, pesa anazosafiria zingesaidia kuinua huduma za kijamii bila gharama za riba ya mikopo iliyozoeleka kama misaada.

Tumeshuhudia viongozi wengi wakishaanza kuwa na mapato mazuri wake zao wanahalalishwa kutunza makazi na wenyewe kubaki wakijiliwaza na vimwana. Nadra siku hizi kuona viongozi wakisafiri na wake zao, je huko waendako nani anawajinafsisha? Hakuna siri viongozi wengi, watumishi mbalimbali wa umma wengi imebaki historia yao tu na machungu kwa familia zao baada ya kumwendea Baba wa Milele wakati tukiwahitaji bado, nini sababu kuendekeza ufuska kutokana na pesa kuwaruhusu na hivyo kushtukia baadhi kuathiriwa na HIV.

Waafrika wengi hatuna hulka ya kujadili maendeleo ila kunung'unika na kulalamika bila kikomo tangu macheo hadi machweo. Hapa Jf mada zinazoletwa zinye kujadili mambo ya maendeleo na kujadili ubunifu hazina mshiko, ila za kunung'unika na kulalamikia hali ya maisha zina wafuasi wengi zaidi. Maana yake mambo ya vijiweni yanamshiko zaidi kuliko ya kufungua kurasa za kujielimisha juu ya maisha.

Baada ya kutembea nimeshuhudia waafrika tunapenda kula sana kuliko tunavyozalisha, hasa sehemu za utumishi serikalini. Tofauti ni vijijini ambako ulaji wao unawiana na utendaji wakati vitendea kazi vyao ni duni sana. Watumishi wa umma wanageuza ofisi ni vijiwe na kusubiria mishahara mwisho wa mwezi.

Wanalalamikia kuwa mishahara haitoshi wakati utendaji ni duni, sasa pesa ya kuwalipa zaidi itatoka wapo wasipokuwa wawajibikaji? Wizara ya utumishi haina vigezo vya kupima utendaji wa watumishi wa umma, na hivyo kulipa mishahara watu wasiowajibika.

Nilishangaa kuona maprofesa, ma-dr. baada ya madarasa katika nchi moja tajri na yenye nguvu kubwa kiuchumi duniani wanaenda kufanya kazi ya usafi kwenye makampuni ili kujiongeza kipato. Wafanyakazi wengi wanafanya kazi zaidi ya moja ili kuhimili hali ngumu ya maisha. Wanashangaa kama Afrika tuna uhuru wa kutumia ardhi na wakati huo huo tukilalamika umaskini. Nchi tajiri mtu huwezi hata kutafuta ziada ya kulima tuta la mchicha. Kibarua kikiota mbawa aoutomatic umeshakuwa homeless kwa walio na kipato cha chini.

Kauli ya kaburu Botha ina ukweli katika mambo mengi, na tunatakiwa kubadilika. Makampuni ya kigeni yanapowataka wafanyakazi kuwajibika kazini kama ilivyo nchi zilizoendelea zinavyofanya kiuchumi, utaona wafanyakazi wanalalamika kwamba wanatumikiswa kama watumwa, tukumbuke wenzetu wanafikiria kiuchumi vinginevyo mitaji yao itakuja filisika kama ilivyotokea mashirika ya umma. Kila siku mfanyakazi kuna record yake ya uzalishaji, na ikitokea muda mrefu amezalisha chini ya kiwango basi must be fired ili kupisha mwingine atakayefaa kwa kampuni. Katika suala la uchumi takrima kando, vijiwe kando, maslahi ya kukuza uchumi mbele.
 
Kwanza to start with, hakuwahi kusema hivo, hii ni hoax. na kama hakusema hivo, despite his strong racist feelings, ni sababu hakuna ukweli wowote.

Tofauti ya maendeleo kati ya nchi za kiafrica na nchi za kizungu au za asia (sisemi waafrika na wazungu au watu wa asia) ni namna serkali na vikundi vingine vyenye maamuzi (decision making actors) wana apply theories to practice, namna wanaunda policies na namna wanamiliki ressources.

Huku afrika serkali zinakosa accountability na raia hawapewi nafasi ya kuwaomba wahusika wawajibike au wajiuzulu. maybe sababu tunaogopa, maybe sababu hatujali, kila mtu ajiulize.

Ila hakuna kabisa tofauti ya akili iliyo kua based on the color of the skin that is what THEY want you to believe ili uendelee kuogopa, uendelee kutojali.
 
kwanza to start with, hakuwahi kusema hivo, hii ni hoax. na kama hakusema hivo, despite his strong racist feelings, ni sababu hakuna ukweli wowote. tofauti ya maendeleo kati ya nchi za kiafrica na nchi za kizungu au za asia (sisemi waafrika na wazungu au watu wa asia) ni namna serkali na vikundi vingine vyenye maamuzi (decision making actors) wana apply theories to practice, namna wanaunda policies na namna wanamiliki ressources.
Huku afrika serkali zinakosa accountability na raia hawapewi nafasi ya kuwaomba wahusika wawajibike au wajiuzulu. maybe sababu tunaogopa, maybe sababu hatujali, kila mtu ajiulize.
Ila hakuna kabisa tofauti ya akili iliyo kua based on the color of the skin. that is what THEY want you to believe ili uendelee kuogopa, uendelee kutojali.

Ni kweli hakuna tofauti ya akili based on rangi ila bado kuna ka ukweli kuhusu maisha yetu. Tumekuwa huru miaka 50 sasa, kwanini bado tupo nyuma hivi? Kwani mzungu ndio anatulazimisha kufanya short term planning? Or to work less and expect more? Or kuendekeza nyumba ndogo na ngono? Kuna thread nimeipitia leo with a title of something like "ukiamua kuwa na nyumba ndogo ..."

Mtu anatoa ushauri jinsi ya kumudu nyumba ndogo na anashangiliwa. What does it say about us as jamii? What goes in our brains? Vitu gani tunahusudu?

Akili tunazo ila tunatofautiana priorities.
Wenzetu priorities zao zipo vingine. Hii ndio tofauti.
 
Ni kweli hakuna tofauti ya akili based on rangi ila bado kuna ka ukweli kuhusu maisha yetu. Tumekuwa huru miaka 50 sasa, kwanini bado tupo nyuma hivi? Kwani mzungu ndio anatulazimisha kufanya short term planning? Or to work less and expect more? Or kuendekeza nyumba ndogo na ngono? Kuna thread nimeipitia leo with a title of something like "ukiamua kuwa na nyumba ndogo ..." Mtu anatoa ushauri jinsi ya kumudu nyumba ndogo na anashangiliwa. What does it say about us as jamii? What goes in our brains? Vitu gani tunahusudu?
Akili tunazo ila tunatofautiana priorities.
Wenzetu priorities zao zipo vingine. Hii ndio tofauti.
Kumbe na wewe ilikukera hiyo thread? anyway...
Kumbuka siku za kwanza za independance tofauti kati ya ulaya na africa haikua kubwa sana. in the city capitals tulikua tumeendelea na tulikua na paplanz nzuri sana za kujiendeleza. shida ilikuja president Thurman wa US aliposema kuna "developed" na "underdeveloped" countries. kuanzia hapo, wenyewe wakaweka ni kitu gani developemnt (kuishi kama wazungu) na kwa nchi kuingia katika hali ya development lazima isaidiwe na brettonwood institution (International Monetary Founds na INternational Bank for Reconstruction and Development, aka IMF na World Bannk).

Hizi institution mbili ziliundwa kwa nia ya kujenga nchi za ulaya baada ya vita na policies zao zilikua friendly, ila walivo zileta huku wakawa wanaoperate kama bank, with high interest rates. Kwa nchi kupewa au kunyimwa loan unapewa masharti magumu kama kupunguza taxes za kuingiza bidhaa toka ulaya na kuongeza taxes kwenye bidhaa produced domesticaly. Kuna nchi ziliamua kujitoa katika hiyo system na kujaribu bahati yao peke yao na waliweza kabisa kuendelea (china, india, singapoore etc).

Sisi tumebaki na madeni, corrupted governemnt na more promise of loans if we weaken our institutions.

Kwa kweli sio kosa la mzungu au la mwafrika, ni kosa la decision makers na serikali, pamoja na "donor" agencies, zikiwemo NGO kadhaa.
 
Nchi yenye watu weusi wengi duniani ni Brazil. Nchi yenye watu weupe wengi duniani ni Russia.

Moldova, a european country has the per capita GDP of 1800$, Botswana an African country has per capita GDP of 5500$.

Need I say more?
 
Back
Top Bottom