Nashukuru kwa maoni yako,ambayo nayapokea kwa mikono miwili, asante sana kukosoa na kukosalewa ni sehemu ya maisha ya mtu mstarabu INGAWA SIJUI NI WAPI NIMEONYESHA JAZBA,
HOJA YANGU HUJAIJIBU. KUHUSU MTAZAMO HUO WA BOTHA,KWAMBA HUKUANZA NAO WEWE HILO TU!
SIONI SABABU YA KUINGIZA SWALA LA DR SLAA HAPA, NONA UNAKWEPA HOJA YANGU KWA MIFANO AMBAYO HAIHUSIANI
kama wewe ni mkweli kubali tu kuwa huo sio mtazamo uluokuwa nao, na kama ulukuwa nao ulichelewa kuutoa, nadhani umenielewa brother
Kwa ushauri wa kukufaa zaidi ni huu hapa.
Ukiwa kama mwakilishi wa wananchi, jitahidi kuingia jamii forums kupata mengi yanayozidi kumiminika kila kukicha, na utajifunza mazuri, tahadhari na mbinu za jitihada za kuwatumikiwa wananchi. Muhimu soma paragarph ifuatayo.
CCM inafanya jitihada kubwa ya kufa na kupona kurejesha jimbo la ubunge Iringa mjini kwa gharama yo yote, na bahati ya wewe kuukwaa ubunge Iringa mjini ujue ni hasira za WanaCCM kumtupa nje Mwakalebela waliyemtaka. Hivyo jitihada za pekee sana unahitaji kufanya kuendelea kulishika jimbo hilo vinginevyo Uchaguzi ujao litarudi mikononi mwa CCM tena, na hii siyo siri, tunakutahadharisha tu Mheshimiwa Mchungaji Mbunge Msigwa.
Eneo unalotoka juhudi zako za utendaji jimboni huwezi kuzilinganisha na mbunge wa viti maalum wa Chadema Chiku Abwao, unatakiwa ufuate nyayo zake. Pamoja na jinsia yake, anafanya makubwa si ya kutetea nafasi ya ubunge, ila kutoa elimu ya uraia kwa wananchi hasa vijijini na ndilo tunalotaka ambalo Chadema wanatakiwa kufanya kwa sasa ili kujiweka sawa kuwa Chama kikubwa cha upinzani kilichojizatiti katika nyanja zote kwa wananchi wa rika zote na wa maeneo yao ambako CCM wanajivunia kwamba ndio chimbuko la ushindi wao.
Angalia pia mbunge kutoka chama cha magamba Mheshimiwa Filikunjombe wa Ludewa pamoja na kuwa kijana, anafanya kasi ya ajabu katika utendaji wake, busara, heshima na ushirikiano mzuri sana. Amewakusanya wabunge wote waliomtangulia kuanzia na mbunge wa kwanza kabisa jimbo hilo Bi Baraka, Mr. Simalenga, Profesa Mathias Kihauli ambaye aliwahi kuwa naibu speaker wa bunge, Kolimba, na Profesa Mwalyosi; kwa ajali ya kupata ushauri na uzoefu wao na papo hapo wako bega kwa bega katika kushirikiana kuleta maendeleo ya utumishi wao katika jimbo lao. You can learn something from him.
Muhimu tusitegemee kupata nafasi kwa misingi ya kuhurumiwa, bali utendaji. Tusitangulize jambo la kusifiwa au kuonekana mtu wa maana sana, bali taswira yako ya utendaji, utu, heshima, busara na ushirikiano ndivyo vinavyokujengea mtu mfumo mzuri wa uongozi na uwakilishi katika jamii yako na taifa.
Wanajamii forums wengi hapa ni watu wasio wafuasi wala wanachama wa vyama vya siasa, mimi nikiwa mmojawapo, ila tu watu wenye jicho kali la upembuzi, na tu wakereketwa wa itikadi na utendaji mzuri katika utumishi wenye kutukuka katika nchi yetu. Sifa njema huhitaji mtu kujitangaza, ila matendo yako ndiyo yanayokutangaza (action speaks louder than words). Viongozi wengi wenye busara hawakurupuki katika kujibu majadiliano hapo, ila ni mahiri katika kufuatilia nini kinaongelewa na kuchota mengi mazuri kwa manufaa ya utumishi wao katika jamii, na laiti wangejitambulisha tungestaajabia wakubwa wengi tusiotegemea.
Kumbuka nukuru za watu wa kimataifa zimehifadhiwa katika vyombo vingi vya habari, ni just bofya vitufe na kuanza kubrowsi, na wazoefu katika fani ya uandishi hawezi kukichukua kitu kilichoongelewa na fulani bila kuhakiki source yake ni sahihi au la, vinginevyo kiwe kitu umekitunga toka kichwani mwako hapo una haki ya kukilalamikia.
:smash: Lets stay stable with solidarity to stabilize real democracy :smash: