FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Ndugu Bongolander,
Hata Mlowezi Ian Smith, wa Rhodesia (Zimbabwe), alipata kunena kwamba mtu mweusi kamwe asingelitawala nchi hiyo katika kipindi cha miaka 100. Of course, mwenzetu 'Uncle Bob' i.e. Robert Gabriel Mugabe, ametawala (na anaendelea kutawala) nchi hiyo hata kabla ya robo ya kipindi ambacho Bwana Ian Smith alikitabiri.
Lakini matokeo ya utawala wa 'Mjomba Bob' hauna tofauti na tunachokiona leo nchini mwetu. Ninamaanisha kusema: mkoloni alichukua rasilimali zetu nchini kwake (Uingereza). Lakini kujitawala kwetu kulimaanisha mwisho wa unyonyaji huo kwa maana kwamba kile ambacho mkoloni alikuwa akikichukua nchini mwetu na kukipeleka nchini mwake, kingelibaki (baada ya kujitawala) kwa manufaa (maendeleo) ya wananchi.
Lakini miaka 50 baadaye, licha ya kujitawala, tunaona kinyume chake. What went wrong? Ninadhani kauli ya Bwana Botha ina imply ukweli kwamba 'Mvunja nchi ni mwanchi'; na, kama unavyosema: Mr Botha's statement is, frankly speaking, more of a challenge to our race than anything else.
Unajua, Ndugu Bongolander, inashangaza jamii ya kimataifa, hakika, kuona watawala wa mataifa yaliyo maskini wakiwa matajiri wa kupindukia kuliko viongozi wa mataifa yaliyoendelea?
Kuwa na madaraka au Rais au Waziri Mkuu hakumaanishi "kutawala" hivi katika ukweli haswa, unaamini kuwa kuna mtu mweusi anatawala? mimi sijaiona.