Hotuba ya Rais Samia Suluhu kwa Taifa Desemba 8, 2021 kuelekea miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika

Hotuba ya Rais Samia Suluhu kwa Taifa Desemba 8, 2021 kuelekea miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika

Kuelekea Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akilihutubia Taifa leo tarehe 08 Desemba, 2021, Ikulu Jijini Dar es Salaam..
Kuna nyingine inaeendelea au ameishia hapa hapa?
 
Mkuu fanya tathimini. Nyerere was good, akaja Mwinyi nchi hoi, akaja mkapa akajenga, alivyokuja JK ohhhh wewe unajua (ingawa awamu zote kuna vitu walifanya lakini siyo priority na sustainable), na vipindi hivyo rushwa na kujuana na kurithishishaba familia. Alipokuja Dkt Magufuli wewe unajua. So Mama naye kaelekea kwa Mwinyi na Kikwete yaani full kuzuga Mama, haeleweki anataka kuitendea nini Tanzania.
Hivi Kuna Rais wa kumfananisha na Jakaya linapokuja suala la maendeleo?
 
Mkuu fanya tathimini. Nyerere was good, akaja Mwinyi nchi hoi, akaja mkapa akajenga, alivyokuja JK ohhhh wewe unajua (ingawa awamu zote kuna vitu walifanya lakini siyo priority na sustainable), na vipindi hivyo rushwa na kujuana na kurithishishaba familia. Alipokuja Dkt Magufuli wewe unajua. So Mama naye kaelekea kwa Mwinyi na Kikwete yaani full kuzuga Mama, haeleweki anataka kuitendea nini Tanzania.
Hivi Kuna Rais wa kumfananisha na Jakaya linapokuja suala la maendeleo?
 
Hapana..kulikuwa kuna jambo nyeti na unusual RAIS alitaka kuhuhudia taifa, pengine alikuwa too emotional, sasa kuna watu wa karibu sana nae watakuwa walinusa hilo.

Kiufupi, raisi hakudhamiria kuzungumza alichozungumza.
thats what i can bet.

Jambo la kujiuliza:
RAIS alikuwa na udharula gani kuzungumzia aliyoyahutubia LEO?
huku KESHO ni siku ya kuadhimisha sherehe za uhuru, ambapo angekuwa wasaa mzuri wa kuhutubia nchi.

Kwamba hayo tuliyoambiwa leo, yalikuwa yana udharula gani kusemwa leo?
 
Hii si hotuba alitoa Bungeni maana hakuna jipya kbs nilidhani nipo darasani kwenye somo la historia.
 
🤣🤣🤣 ni muhimu ufahamu wapi ulipotoka Maana ukwendapo hupajui...... Kusema hi hotuba sio, nafikiri huko.ni kumvunjia heshima kiongozi wa nchi.
 
mtu anasimama jukwaani anahutubia nchi eti anasema uhuru wa tanzania bara 🤣🤣🤣🤣 urais wa kuokota
 
Mwasisi wa Taifa hili aliwahi kutangaza vita juu ya maadui wakuu watatu ambao ni MARADHI, UMASIKINI na UJINGA. Hawa ni maadui ambao inahitaji weredi kupambana nao tofauti na hapo watakumaliza wewe. Tanzania bado tunao maadui hawa. Hasa UJINGA, maana ndo umesababisha UMASIKINI na MARADHI kuendelea kupiga gitaa. UJINGA umeendelea kuumiza jamii na taifa letu tokea tupate uhuru mpaka sasa.

Tumetimiza miaka 60 tokea taifa letu lipate uhuru lakini tunaposherehekea yatupaswa kujiuliza tunasherehekea au kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika kwa yapi mazuri tuliyoyapatia?

Ni miaka 60 ya Uhuru ambayo adui Maradhi anaendelea kutunyanyasa ipasavyo kwa sababu ambazo walio na nafasi wanaendelea kutupatia ahadi. Madawa na huduma za Afya stahiki kwenye mahospitali yetu imekuwa ni kitendawili kigumu sana kukitegua. India, Uingereza na Marekani pameeendelea kuwa Clinic na sehemu za kukimbilia kwa walio nacho pamoja na wenye magonjwa maalumu na sio KCMC, Bugando au Muhimbili.

Leo hii maji safi na salama kwenye maeneo mengi ya vijijini yamekuwa changamoto kwelikweli. Bado watu wanapiga safari ya zaidi ya Km 15 kufuata maji, maeneo mengine binadamu wanagombania maji na wanyama. Ni miaka 60 tokea taifa letu lipate uhuru, ahadi ni zile zile, "Tutawaletea maji vijijini", hazibadiliki na hakuna anayejali.

Miaka 60 ya uhuru baadhi ya maeneo yaliyo mengi hapa nchini mawasiliano ya simu bado ni shida. Unakuta kasi ya Internet ipo chini sana kiasi kwamba ukianza kudownload picha ya KB 740 utahitaji kusubiria nusu saa. Uhitaji wa mawasiliano hasa vijijini ni mkubwa lakini huduma bado hazikidhi mahitaji haya.

Tunasherehekea miaka 50 ya uhuru, wanafunzi bado wanasomea nje (madarasa hayatoshi), wanakaaa chini na uhaba wa vyoo na nyumba za walimu vikikidhiri huku kuna katibu wa chama fulani anaendesha gari la Mil. 400. Tumeendelea kuamini katika mfumo wa Elimu yetu ambayo ni kukaririshana Italy revolution na sio How Elites can transform Tanzania. Vijana wanaandaliwa kuajiriwa na sio kujiajiri. Wapi somo la STADI ZA KAZI? TEHAMA? HAIBA NA MICHEZO? Wasomi wa taifa hili mchango wao uko wapi maana Wazungu na Wachina wanachuma mali kama wako kwao?

Ni kipindi hiki ambacho bado ajira kwa vijana imekuwa shida kubwa sana. Viongozi wa Serikali wameamua kuja na msamiati mpya wa KUJIAJIRI kama fimbo ya kuwanyamazisha wanaohoji ukosefu wa ajira. Wapo vijan wanaojaribu kujiajiri na wanakutana na urasimu mkubwa sana ambao huwarudisha nyuma. Ni nani asimame awatetee vijana? Leo Cameraman anajichanganya ananunua Drone yake ya kupigia picha na atapaswa kulipa USD 100 kwa kila mkoa atakaotaka kufanya kazi kwa mwaka. Tanzania ina mikoa mingapi? Kwa nini serikali isitafute namna ya kumsaidia kijana huyu hata alipe fee moja kwa mwaka na awe huru kufanya kazi popote?

Miaka 60 ya Uhuru wetu lakini hatuna uhakika wa Uhuru wa tuyaongeayo. Ni nani ajuaye kesho yake?

Miaka hii bado watu wanaendelea kutambiana na kuulizana ukanda, ukabila na udini wao ili wapeane fursa. Bado masuala yasiyo na Afya kwa ustawi wa jamii zetu na taifa kwa ujumla yanapewa kipaumbele.

"Rushwa ni adui wa Haki", ni kauli ya mwasisi wa taifa hili. Miaka hii bado kuna kada na watu wanaendeleza Rushwa ili wapate nafasi fulani wakati hawafai kuwa hapo. Ni miaka hii, bado tunapambana kumaliza swala ambalo baadhi ya watu wanapambana kuliimarisha. Haki, Uhuru na Stahiki za watu walio wengi zimepokonywa kisa Rushwa.

Wakati China akileta mapinduzi ya Teknolojia na kuitetemesha USA, bado taifa letu pendwa limeendelea kuamini katika kushikiria madaraka miaka 60 tokea tupate uhuru. Hatuna hata mpango wa kuwekeza kwenye angalau hub moja kubwa ya Teknolojia ya kitaifa ila tunawezekeza kwenye kuumizana na kubambikiana kesi ili tuendelee kutawala na kuongoza Nchi. Umoja na Uhuru kama ilivyo kaulimbiu yetu iko wapi?

Je, haya ndiyo yalikuwa malengo ya Uhuru wetu? Ni akina nani haswa tunawasubiri waje watuchoree ramani ya vita tunayopaswa kupigana huku tukiwa tumelalia maziwa, madini, mbuga za wanyama, mapori na ardhi yetu rutuba huku tukilia njaa, ukosefu wa ajira, ubovu wa miondombinu n.k?

Ndani ya miaka 60 tumepeleka timu kwenye michuano ya Afrika mara mbili. Tuna medali ngapi za dhahabu kwenye olimpiki vile? Kamati za ushindi na michezo ni nyingi kuliko mafanikio yetu kwenye michezo. Miaka 60 ya Uhuru bado sera ni zile zile na vilio vile vile. Hakuna kilichobadilika. Bado tunaongozwa na Rasimu za vyama na sio msimamo wa pamoja kama taifa. Leo akija Rais mpenda kilimo tutalima, kesho akija mpenda Utalii tutatalii. Kwa nini lakini Tanzania yetu.

Kila nikisoma historia ya taifa langu, na hapa tulipo naendelea kuogopa na kuhofia kuwa miaka 70 ya uhuru wetu tutakuwa vile vile kama tusipoacha Urasimu wa kifikra, kimadaraka, na tamaa za vitu. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA. HERI YA MIAKA 60 YA UHURU.

NB. Vijana wa leo ni zao la wazee wa juzi, jana na leo.
 
Oscar Kambona hajatajwa kwenye orodha ya wapigania uhuru
 
Back
Top Bottom