Hotuba ya Rais Samia Suluhu kwa Taifa Desemba 8, 2021 kuelekea miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika

Hotuba ya Rais Samia Suluhu kwa Taifa Desemba 8, 2021 kuelekea miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika

Yaani baada ya kutaja maneno "Tanganyika na sasa Tanzania Bara" hotuba nzima imegeuka na kuanza kuzungumzia masuala jumuishi ya JMT!

Nadhani uongozi wa juu haujielewi au pengine mifumo nayo imekosa uelewa!

Hivi kweli unasherehekea miaka 60 ya uhuru wa kitu ambacho hakipo!

Watanganyika ni watu wa ajabu sana! Hawapendi kuitwa Watanganyika! Hawajui wanavonufaika na muungano zaidi ya kuitwa Watanzania!

Hawataki hata kujifunza na kuwaelewa wenzao wa Zanzibar waliopambana kuwa huru licha ya kukaliwa kimabavu na

#Miaka 60Uhuru_Bila_Tanganyika
 
Suala la mfumuko wa bei/kutetereka kwa uchumi kwa ujumla wake sio la Tanzania pekee bali ni tatizo la dunia nzima, nalo limesababishwa na Janga na UVIKO 19.
Hiyo ni athari ya uviko 19.
Acha izo embu nielezee kidogo uwo uviko unahusiana na mfumuko wa bei za vitu kupanda? Uwo uviko leo ndo umeamza au ni Tangu 2019? Huu mfumuko wa bei umeanza mwezi wa5/2021

Sent from my E2363 using JamiiForums mobile app
 
Rais Samia jana usiku Desemba 08, 2021, hotuba yake ilikuwa ni nyepesi sana haina nyama za kutosha, haikupevuka, haikukidhi na kutupatia vision mpya. Hakuweza kuweka wazi baadhi ya misukosuko Taifa iliyopitia na yeye anakuja na Tiba gani.

Mimi binafsi nilijutia muda wa kuangalia Chelsea ikicheza nikitarajia kupata kitu kipya bali niliambulia patupu

Sijui wataalam wa hoja zaidi mmetosheka?
 
Si ungezima redio? Mbona uliendelea kusikiliza? Akili za mende bwana
 
Mh Rais Samia jana hotuba yake ilikuwa ni nyepesi sana haina nyama za kutosha haikupevuka haikukidhi na kutupatia vision mpya hakuweza kuweka wazi baadhi ya misukosuko Taifa iliyopitia na yeye anakuja na Tiba gani ??mimi binafsi nilijutia muda wa kuangalia CHELSEA WAKICHEZA nikitarajia kupata kitu kipya bali niliambulia patupu sijui wataalam wa hoja zaidi mmetosheka ??
Mfano wa Hotuba....tulipata uhuru mwaka.....nyerere alikuwa rais wa kwanza, Tumejenga shule 10, tumelima mpunga mwaka huu, ......Asante ndugu watanzania kwa kunisikiliza
 
Nimefuatilia hutuba ya Mh. Rais aliyoitoa leo na kufadhaishwa saana na aina hutuba aliyoitoa . Hakika hii imekuwa ni historia ya nchi yetu na sio hutuba. Nashauri atafutiwe washauri na waandaaji weredi wa hotuba za Marais....
Ukiona kiongozi anaongelea mambo yaliyopita ujuwe tu hakuna kitu, kiongozi anatakiwa aje na vision 10 years ncho iende wapi huko kujisifia tuna shule 1000 sujui Hosp 100 ni mambo hayana tija.

Sema tumetimiza miaka 60 lakini dira yetu ni hivi, juzi tulikuwa nchi ya viwanda nyimbo zikawa viwanda ila naona sasa tuko amapiano hatujui tunaimba nini mpaka sasa kuna chorus tu kazi iendelee lakini nyimbo hawajaingiza sauti.

Nchi bila vision shida sana, nadhani kuna mengi kujifunza nilitaka kusikia vision Tanzania 2030 halafu anaweka malengo halafu sote tuimbe same song unakuja kuleta story tulikuwa na hichi sasa tuna hichi bila kusema lengo ilikuwa hichi lakini tumepata hichi. No target no measurement
 
Hotuba ya rais wa JMT imebase sana kwenye mafanikio tu. Lakini ukweli ni kuwa sio kwamba kumekuwa na mafanikio pekee bali pia kumekuwa na kurudishana nyuma. Na ndio maana taifa letu bado lina umasikini mkubwa.

Mfano ni ufisadi uliotamalaki kwa miaka mingi umesababisha tuwe masikini. Na ufisadi huu umekuwa ukifanywa na wanaCcm. Na sababu ya ufisadi kama Epa,Kagoda, Escrow na leo hii hata Hospital hazina madawa, madarasa hakuna na barabara hazipitiki vijijni.
 
Rais anahutubia Nchi hata maamuzi magumu na yenye maslahi kwa wananchi hamna , Bei za bidhaa zinazidi kupanda , bei ya mbolea huku kwetu tukajua ni utani ingeweza kukaa sawa kabla ya msimu lkn wapi.

Cheo cha Uraìs hakijaendana na hotuba , haina uzito . Mwelekeo wa Nchi dhidi ya mabadiliko yatakayotokana na Propaganda ya Korona na Chanjo yake hamna .

Huenda huo ulikuwa utangulizi hotuba yenyewe inakuja. ILA WALIOKO NYUMA YA HAYA MF. J HAWAMTAKII MEMA MAMA AU NDIYO MAPENZI YAO KUTIMIA ?
 
Hivi hakukuwa na mwanamke hata mmoja kumbe[emoji848]
 
Makosa ni MENGI SANA KULIKO MAFANIKIO Ndio maana hawasemi.

JamiiForums-1827926957.jpg
 
Eti anasema serikali imeleta unafuu wa maisha kwa watanzania, hivi sijui hapo alikua anamaanisha nini
 
Back
Top Bottom