===
Sitaki kuzungumzia mambo mengi yaliyofanywa na Serikali za Chama Cha Mapinduzi za awamu zote kwa miaka 60 toka tukiitwa TANU na sasa CCM,
Kwamsiojua,Umri wa kuishi kwa Mtanzania umeongezeka kutokana na uboreshaji na upatikanaji wa lishe na kuondoa udumavu pamoja na huduma bora za afya nchini,
Wakati tunapata Uhuru wastani wa Umri wa kuishi kwa Mtanzania ulikuwa ni miaka 37 na sasa Serikali za CCM na Mungu wameufikisha miaka 67.
Wewe unayelalamika leo huoni faida za CCM huenda bila CCM na Mungu Usingekuwa hai,Hivyo Moyo wako ukusute unapoinyanyasa CCM kwa kejeli na dharau,
Mtakubaliana na Mimi,Zawadi kubwa kuliko zote kwa mwanadamu hapa duniani ni Uhai|Kuishi,
Wale wanaosema hawaoni ni nini CCM imefanya kwa miaka 60 basi hili la Umri wao wenyewe na ndugu zao kuongezeka kutoka kuishi wastani wa miaka 37 hadi miaka 60 liwaoneshe umuhimu na kazi nzuri ya Chama Cha Mapinduzi na Mungu,
Mungu Ibariki Africa
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Rais Samia Sululu,
#Happy birthday Tanganyika