Uchaguzi 2020 Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Juni 08, 2020


Si vibaya kujitoa hofu, leo nilitarajia wanaccm kujazwa humu mitandaoni kupunguza sumu ya hotuba ya Lissu. Kwa mtu yoyote anayejua siasa anajua fika alichoongea leo Lissu, na kwa uwezo wake wa kushawishi, hata kama hatashinda, ataiacha serikali ya ccm ikiwa na wakati mgumu sana baada ya uchaguzi. Nina uhakika kwa ushawishi alionao Lissu, na uvumilivu mdogo alionao mwenyekiti wa ccm kwenye ushindani wa kisiasa, tutegemee kampeni zitazokagubikwa na ukiukwaji mkubwa wa haki, vipigo kwa wapinzani vitakavyopekea vilema na hata vifo. Uchaguzi wenyewe mkuu kama wapinzani watashiriki hadi siku ya kupiga kura, tutaona uchaguzi wa kishenzi kupata kutokea ndani ya nchi hii, na vifo kwa wale watakaoamua kulinda haki yao.
 
Uyu, uyu, uyu...hivi tunakwama wapi, hata kuandika tunashindwa.
 
Endelea kusubiri ikufwate haki mkuu .Hata huyo unayemsadiki akifanikiwa utaona mziki wake. Politics siku zote ni bad and dirty game.Tuendelee kupambana na maisha yetu.Hakuna jipya.

Hii post ni post inayojua fika ikitendeka haki kutatokea matokeo yasiyomfurahisha. Hivyo namna pekee ni kuhalalisha uhayawani kama sehemu ya kuficha hofu ya kushindana kihalali.
 
Iv jiwe ataongea nini aeleweke, naona Rais tundu lissu hotuba yake imepiga kotekote
 
Ningeshauri chadema iachane na urais ikomae na wabunge maana hali sio hali,fedha za kampeni za urais zitumike kujenga haya chuo chamfano cha ufundi ama ofisi bora za chama!! Sijawahi kuona chadema imejenga kitu cha maana chakuwawezesha wananchi wetu. Maandamano,matusi,kukashifu viongozi,ndiyo nembo ya chadema sasa hivyo vimedhibitiwa chama kimekuwa arosto.
Chadema ibadilike kiwe chamakipya nasera mpya zakimaendeleo badala ya janjajanja nahapo ndipo kitapata viongozi wasomi na mahiri sio vijana wajanjajanja kama kinasugu,profujei sijui lijualikali nk.
 
Mimi Mwaka huu nakomaa na lissu.Japo magu yako mambo kafanya vizuri, yako mambo yanamponza jpm.Kiburi kwa waliomchagua
 
Lissu anajitutumua ili asipotee mazima.
Ila kiukweli kafeli pakubwa sana.
Tanzania kama taifa inasonga mbele.
 
Mmmmh.. yaani nyinyi wanasaccos nafikiri kwenye vichwa vyenu hamna akili kabisa kuna makamasi tu. Yaani Tundu awe Rais wa Tanzania kama ameshindwa Lowassa!! Ngoja apate pesa za wajinga!
 
Hilo andiko la Lissu ni shule tosha; watu humu ndani watazame mpangilio wa hoja zake na jinsi alivyoziwasilisha, mifano aliyoitoa kusapoti hoja zake, matumizi sahihi ya alama kama koma na nukta, matumizi ya herufi ( wengi huwa mnachanganya "r" na "L").

Angalau mjifunze namna ya kuanzisha hoja, kuitetea, na kuwa tayari kurekebishwa pale itapothibitika hoja unayoisimamia haina uungwaji mkono wa kutosha, tuwe tayari kukubali kukosolewa, kwani hakuna anayejua kila kitu.
 
Lissu anajitutumua ili asipotee mazima.
Ila kiukweli kafeli pakubwa sana.
Tanzania kama taifa inasonga mbele.

Sauti iko chini, tunachukua mrejesho wa jinsi mlivyopanic. Iwapo ccm watafanya kosa la kumuachia Lissu kushiriki kampeni, nina hakika hata ccm ikishinda, kutatokea mabadiliko makubwa sana kwenye katiba yetu. Ngoja uone wakati wa kampeni mtaona hilo nyomi lake. Anayekubalika anakubalika tu.
 
Yaani mmefurahii[emoji23][emoji23], hamuoni Tena kuwa tume ya uchaguzi siyo huru, mnaona tayari mmeshinda uchaguzi!
 
Urais hauapatikani kwa kutajwa mitandaoni kamanda! Unapatikana kwa mikakati.

Wakati nyie mnashangilia jina la Lisu mitandaoni, ccm wako field kupanga mikakati ya ushindi.
Mtaelewa lini nyie bavicha?

Wachawi ,mashetani wakubwa ,wamwagaji wa damu za watu CCM Wakofield au wako wanawanga?
 
Nikiwa mmoja miongoni mwa raia wa taifa hili napaswa kufungua mdomo hasa ktk mambo mazito na muhimu kama uchaguz mkuu wa mwaka huu.
Leo Juni 8, kupitia vyombo vikubwa vya habar kama DW na mitandao ya kijamii tumepata habari kwamba wakili maarufu na mbunge wa zamani Tundu Antipasi Lissu amekusudia kuomba ridhaa kupitia chama chake kugombea nafasi ya uraisi wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania.
Jambo hili limezua mjadala mkali ktk jamii, baadhi ya watu wakimbeza kuwa hatoweza kuishinda CCM ktk uchaguz mkuu, wengine hata wakimtukana hasa ktk mtandao wa Facebook lakini kiasi kaungwa mkono ktk mtandao wa tweeter, kila mmoja ana mtazamo wake lakini tusipingane kwa matusi bali kwa hoja zenye mashiko na maslahi mapana kwa taifa hili.
Binafsi namtazama advocate Lissu kama ifuatavyo;
1: Msomi aliyebobea hasa ktk sheria.
2: Mwanasiasa mahiri mwenye uwezo wa
kujenga hoja na kuitetea.
3: Ni miongoni mwa wanasiasa maarufu
duniani baada ya kunusurika kifo cha ris
asi mjini Dodoma na kutumia jukwaa la
kimataifa kuihabarisha dunia juu ya jarib
io la kutaka kumuua.
Hayo mambo makuu matatu (3) naamini wakili Lissu ndio nguzo zake za kutegemewa ambazo anahisi anaweza kugombea uraisi mwezi October 2020. Huku kipengere namba tatu (3) akitegemea kupata kura nyingi zilizojaa huruma kutoka kwa wananchi.
USHAURI KWA LISSU.
Namshauri asigombee mwaka huu kwa sababu kuu zifuatazo;
1: Raisi Magufuli kisiasa amekuwa more
popular it means hayupo mwanasiasa
wa kumshinda ktk uchaguzi mkuu 202
0, majority ya wananchi wanaridhishw
a na utendaji wa raisi Magufuli.
2: Upinzani mwaka huu watakosa sera z
a kujinadi mbele ya wananchi na waka
eleweka maana Magufuli ameingia kt
k nyoyo za watanzania.
3: CHADEMA sasa hiv imekuwa kama ny
umba iliyogeuka gofu baada ya kukim
iwa na wakazi wake.
Binafsi namhurumia wakili Lissu namshauri kubaki kuwa mpiga kura tu kwa wengine labda akagombee ubunge lakini sio uraisi wa Jamhuri, asubiri mpk 2025 Magufuli akimaliza muda wake lakini sio mwaka huu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji12] hawatakuelewa mkuu, mahaba yameanza Tena kama ya mwaka ulee[emoji23]
 
Kama ningekuwa mimi ndio Mbowe nisinge ruhusu Tundu Lissu aongee kwa sababu amekiabisha chama pia kuonyesha moja kwa moja kua CHADEMA hawana Sera

Hotuba mzima ya Tundu Lissu point ambayo imeonekana kidogo ni ya muhimu ni yakutangaza nia tu ndio hoja ambayo vyombo vya habari vyote vimeripoti

Huwezi kugombea Urais ukaja na Sera za kusema kwamba utawafuta watanzania machozi na utasimama na wajane are you serious

Kwa hotuba ya leo haikuwa hotuba ya kisiasa bali ya kiroho na ilitakiwa itolewe kanisani mambo ya kufarijiana na Urais wapi na wapi yaani unatuahidi watanzania kushuhulika na wajane jamani jamani Tundu Lissu dah

Yani unataka ukishindwa Urais uje utufariji badala ya kutuletea maendeleo
 
Wenye akili tu watakuelewa ila misukule nadhani hawatakuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…