Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Ndugu zangu,
Huenda maisha ya lockdown yamemwathiri Tundu Lissu,ukimsikiliza utagundua walemgwa wa "urais" wake sio Watanzania bali ni mabalozi na raia nchi za ulaya na Amerika waishio Tanzania.
Nilifikiri kukaa Ubelgiji angekutana na akina Mouse Katumbi au marafiki wa Tshisekedi ambao wangemfunza jinsi ya "kufanya siasa ughaibuni'.Leo wananchi wa Ikungi wameshasahau kama walishawahi kuwa na Mbunge anaueitwa Tundu Lissu sababu hazungumzi kero yao hata moja japo kwa unafiki.
Nimalize tu kwa kumtakia maisha mema huko ughaibuni ahakikishe wanae wanasoma nayeye alinde kibarua chake.
Si vibaya kujitoa hofu, leo nilitarajia wanaccm kujazwa humu mitandaoni kupunguza sumu ya hotuba ya Lissu. Kwa mtu yoyote anayejua siasa anajua fika alichoongea leo Lissu, na kwa uwezo wake wa kushawishi, hata kama hatashinda, ataiacha serikali ya ccm ikiwa na wakati mgumu sana baada ya uchaguzi. Nina uhakika kwa ushawishi alionao Lissu, na uvumilivu mdogo alionao mwenyekiti wa ccm kwenye ushindani wa kisiasa, tutegemee kampeni zitazokagubikwa na ukiukwaji mkubwa wa haki, vipigo kwa wapinzani vitakavyopekea vilema na hata vifo. Uchaguzi wenyewe mkuu kama wapinzani watashiriki hadi siku ya kupiga kura, tutaona uchaguzi wa kishenzi kupata kutokea ndani ya nchi hii, na vifo kwa wale watakaoamua kulinda haki yao.