Mbona unaongeza mashaka zaidi kwa maelezo hayo. Inachukua muda gani kuinuka na kulaza kiti ulichokalia, uinuke ili uhamie nyuma na risasi zinamiminwa? Isitoshe, kama alijua angemiminiwa risasi angechukua tahadhari zaidi za usalama, kuliko hiyo ya kuhama kiti ati kujificha viti vya nyuma kana kwamba huko risasi haziwezi kufika. Kitendo cha kuinuka kwenye kiti kunaweka mwili wote kwenye hatari ya kupigwa risasi.
Hata vile, hoja ni yaliyomo kwenye hotuba yake kama yanatosheleza kushawishi chama chake kimpe ridhaa ya kuwa mgombea wa kiti cha Urais. Na endapo na wananchi watampa ridhaa hiyo, bila shaka waliopanga na kutekeleza shambulio, kama utawala ulipo haujawakamata, atalishughulikia kwanza. Tumwombee arejee salama kutimiza ndoti zake.