Uchaguzi 2020 Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Juni 08, 2020

Sikatai mazuri anayoyafanya leo ndio maana siachi kusema inapobidi.ila kitendo cha kutaka kumuondoa list duniani kupotea kwa Ben na wengine hilo doa kwangu halifutiki mpaka naingia kaburini.Hakuna blunder kubwa iliyofanyika kwenye utawala wake kama kupotea kwa ben na assassination plot ya lisu na ndio maana wengi hapa na mitandao I na dunia nzima wanamsema Lissu kwa wema na kumuombea heri kwasababu ya kumhurumia jaribio la mauwaji dhidi yake hiyo imewaumiza watu mnoooooo Kama hujui.
 

Itakapothibitishwa kuwa wahusika siyo Serikali, rejea kuiomba radhi jumuia ya JF. Nasema hili kwa uhakika kabisa kwani mazingira ya matukio hayo mnayodai Serikali inahusika, kwa jinsi yalivyotokea ni dhahiri kuna mkono wa mtu wa ndani. Tuombe uzima Lissu arejee na dereva wake, kama huo ubavu anao, ili mbivu na mbichi zijulikane.
 
Ulichoandika hapa umemkufuru Mungu// lisu alitelekeza Jimbo kweli?

Mngefanikiwa kumuuwa Kama yalivyokuwa matakwa yenu hilo Jimbo mngesemaje? Kifupi mnapambana na mungu hampambani na Lissu.

Nitajie mtanzania aliepigwa risasi 16 za smg na akapona kwataarifa yako wanajeshi wengi ambao kimsingi ndio wanajua maana ya risasi ndio wanaouelewa muujiza wa Tundu Lissu.
 
Wat watu wameuliza maswali ya mantiki juu ya swala la lisu kwa unyenyekevu hawapati majibu unadhani watamnyooshea kidole Nani?
 

Sijui kwa wengine ila kwangu watu kupotea, kushambuliwa na wengine kuuwawa katika nchi yenye serikali na vyombo vya ulinzi na usalama inasikitisha kama sio kukatisha tamaa.

Huu utetezi wa sijui hakuna ushahidi, mara serikali haihusiki ni hoja dhaifu mno, bora mara milioni ingehusika kuliko kila siku kupuga kelele kwamba hawajui wahusika.
 
Kwa hiyo unamuunga mkono Lissu kwa sababu tu ya shambulizi la kumuuwa, siyo? Ikithibitishwa kuwa ni shambulizi la uhalifu au vingenevyo, utaomba radhi?

Maswali machache, kwa kuwa umeamua kuamini hivyo:
• Umewahi kumwona mtu yeyote aliyepigwa risasi? Inasemekana risasi zaidi ya moja ziliingia mwilini mwake, na bado yuko hai, hadi leo.
• Unaelezaje yeye kupigwa risasi kulia (upande wa dereva) wakati anayedaiwa kupiga risasi alifanya hivyo upande wa kushoto?
• Je, kwa nini dereva wake hakupatwa na hata risasi moja?

TAFAKURI kwa kina kuhusu tukio hilo kwa kutumia maswali hayo.

Vyovyote vile, INAPENDEZA unapokiri kuwa Serikali iliyoko madarakani inafanya vizuri kwa masuala ya kiuchumi
 
Mhusika wa shambulio anajulikana pasipo shaka, na muda mwafaka atakamatwa na kufikishwa kujibu mashitaka. PERIOD
 
Mhusika wa shambulio anajulikana pasipo shaka, na muda mwafaka atakamatwa na kufikishwa kujibu mashitaka. PERIOD

Walioenda shule wanasema haki iliyocheleweshwa ni haki iliyopotea. Nashukuru kwa kutuweka wazi kuhusu wahusika wa shambulio mkuu, naomba tu niulize, hiyo kauli kwamba wahusika wanajulikana ni ya kutoka kwa nani? Ni chanzo cha kuaminika? Kina utofauti na wanaosema serikali inahusika?
 

Wakati uliyemnukuu na kumuuliza hayo maswali anajiandaa kukujibu, majibu yake mepesi sana.

Nikikwambia aligeukia nyuma akitaka kujificha viti vya nyuma ila ndio jamaa walikua wameshaanza kumimina risasi ndio maana akaathirika upande wa kulia utapinga?
 
Nakukumbusha haya maswali.

.1. Nani mwenye mamlaka ya kubadili zamu za walinzi kati
Swali langu ni moja tu,hata kama Lissu atashinda urais,nani atathubutu kumtangaza?
Labda nikuambie lissu amekuja kuwatega na kuwakamatisha wenye mamlaka mbele ya mahakama za kimataifa hili analijua sana dunia nzima inasubiri magu ajichanganye hujiulizi kwanini hata majirani zetu wametudindia ishu ya covid anatafutwa happy mtu wa kufungwa na mahaka ya the hague Yani wanasubiriwa wajichanganye tu historian ya taifa ibadilike.
 
Labda nikukumbushe tu kwamba toka awali Lissu, aliyejeruhiwa, mara kadhaa kabla hajashambuliwa kwa risasi, na hata baada ya kupata fahamu, amekuwa akidai anawajua wabaya wake. Kwa kuwa yuko hai, naamini atakuwa shahidi namba moja. Tuvute subira tu.
 
Du, maelezo hayo hayakisi uhalisia wa ntu aliyekaa kwenye kiti, ndani ya gari, amefunga mkanda, kwa muda huo risasi zinamiminwa, aweze kugeuza upande wake wa kulia uwe kushoto na hata risasi moja isimpate mgongoni! Na kwa nini kiunoni kulia tu isiwe sehemu zingine za mwili?
 
Labda nikukumbushe tu kwamba toka awali Lissu, aliyejeruhiwa, mara kadhaa kabla hajashambuliwa kwa risasi, na hata baada ya kupata fahamu, amekuwa akidai anawajua wabaya wake. Kwa kuwa yuko hai, naamini atakuwa shahidi namba moja. Tuvute subira tu.

Rejea post yangu ya awali kuhusu hili jambo.
Washambuliaji wake kutokua kwenye vyombo vya dola mahali panapohusika hadi sasa ni doa na aibu kwa taifa.

Haijalishi ni cdm, ccm, askari, viongozi wa vyama, dini , kikundi au mtu yeyote yule, wanatakiwa wawe wanatumikia haki yao kwa mujibu wa sheria zetu.

Narejea tena, mara milioni vyombo vyenye dhamana ya ulinzi wangekiri kuhusika kuliko kukiri kutokujua na kutokuchukua hatua stahiki kwa hili sakata.
 

Kwamba mtu aliyechaguliwa na wananchi kuwaongoza, mwenye mamlaka ya juu ya vyombo vyote vya ulinzi, halijui hilo unalodhania, basi hakika hastahili kuwa Rais na viongozi wa vyombo hivyo pia hawafai. Du! Ati Lissu amekuja kuwatega!!!!
 

Hizo ni taaluma za watu mkuu. Unaongeleaje mgongo wakati tunajadili kulia na kushoto?
Umeshaambiwa walishakua na mashaka ya kuona wanafuatiliwa, unaweza kueleza ni muda gani waliwaona hao watu, walichukua hatua gani kabla ya kuanza kumiminiwa risasi na hicho kitendo kilichukua dakika ngapi?

Ukiwa kwenye kiti cha abiria ukakilaza na kukilalua ukielekea nyuma ya gari mgongo ukiwa juu tumbo chini, upande wako wa kulia utakua upande upi wa gari?
 

Mbona unaongeza mashaka zaidi kwa maelezo hayo. Inachukua muda gani kuinuka na kulaza kiti ulichokalia, uinuke ili uhamie nyuma na risasi zinamiminwa? Isitoshe, kama alijua angemiminiwa risasi angechukua tahadhari zaidi za usalama, kuliko hiyo ya kuhama kiti ati kujificha viti vya nyuma kana kwamba huko risasi haziwezi kufika. Kitendo cha kuinuka kwenye kiti kunaweka mwili wote kwenye hatari ya kupigwa risasi.

Hata vile, hoja ni yaliyomo kwenye hotuba yake kama yanatosheleza kushawishi chama chake kimpe ridhaa ya kuwa mgombea wa kiti cha Urais. Na endapo na wananchi watampa ridhaa hiyo, bila shaka waliopanga na kutekeleza shambulio, kama utawala ulipo haujawakamata, atalishughulikia kwanza. Tumwombee arejee salama kutimiza ndoti zake.
 
H Huyu Lisu ndio Yule aliyekuwa anatoa kashfa Kwa Mwl Nyerere huku mate yakimtoka, ndio huyu huyu Leo hii anaye mtoa Mwl as A reference ya kiongozi Bora???
Ndio Lisu huyu huyu ambaye kila siku alikuwa akipinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lakini huyo huyo anakubali uwepo wa Tanganyika, ?? Kwa kuwa huu muungano wa Tanganyika ulitengenezwa na Mkoloni, lakini tuliotengeneza sisi ni batili??

Na hizi sera zake za kiuchumi ukichanganya na utetezi wa Miga si ndio atatuuza kabisa na tushindwe kutoka ktk hiyo mikataba.
 


Nasisitiza, fani na taaluma za watu ziheshimiwe.
Tukirudi kwenye hoja, tuliyenae madarakani na huyu tunaejadili hotuba yake wanafanana kwa kiasi kikubwa sana, wote hawatoshi kuwa viongozi kwa hiyo nafasi tofauti ni moja tu, mmoja ameshikilia kiti mwingine anatamani ajaribu kukaa pale.

Oh! Hiyo ni kwa mujibu wa mtizamo wangu binafsi. Ikiwa tumekosa kabisa kabisaaaa, bora aliyepo amalizie muhula wake. Ila kwa hizi fununu za kubadili katiba kuhusu kinga kwa baadhi ya wakuu....inafikirisha zaidi.
 

Wanatosha, hawatoshi ni uamuzi wa wananchi. Iwapo unaye unaamini anatosha, mshawishi ajiongoze kugombea, hata kama ni wewe, ingia ulingoni, mradi unatimiza masharti yaliyoko kwenye Katiba ya JMT (1977).

Kuhusu kubadili Katiba sina la kujadili hapa labda ukilianzisha kwenye "forum" mpya naweza kuchangia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…