Hakika imani yangu kuwa ukweli hujitenga na uongo inazidi kuimarika. Nondo anazoshusha mzee Warioba bungeni muda huu ni nomaaaaa!
Kama kweli wabunge wa CCM wanajua anachokiongea huyu Jaji, basi ni wazi magamba wanajuta kumjua huyu mzee ambaye naona leo kaamua kutapika yote ya moyoni mwake na mzee anaonekana anaongea kwa hisia toka moyoni mwake kwa dhati kabisa.
Kuna wakti Prof Shivji alimdiscredit ila nimegundua kumbe kuna vitu Prof ameachwa mbali na huyu Jaji anayeongea kwa takwimu na uhalisia wa kinachoendelea ktk maisha ya watanzania wa kawaida. Maprofesa wengi wa CCM ndani ya bunge wamekuwa wadogo na inaonekana somo linawaingia haswaaa!