Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Hii rasimu mpaka alipofikia ni nzuri sana, aliponiboa ni serikali tatu.. Nashangaa serikali tatu, hiyo nchi ya tatu ni ipi? Mimi nataka serikali mbili
Serikali 2 ipo unaitakaje tena? tatizo imeshindwa kukidhi haja ndani ya miaka 50 iliyopita,hatuna budi kubadilika na kuangalia serikali 1 au 3.
 
Mkuu, kinachonipa hofu ni kuona wabunge wa Zanzibar bila kujali itikadi zao wanashangilia sana hotuba ya Warioba. Wana ajenda ya siri hawa

Mkuu Wazanzibar wanataka serikali tatu na ndio maana kura ya siri ni mwiba mchungu kwa wapenda serikali mbili. Believe me wakifika kwenye kipengele cha muundo wa muungano Wazenj wote bila kujali vyama vyao watawatosa wapenda serikali mbili ilimradi tu kura iwe ya siri.
 
Kwa nondo za leo zinazoendelea kushushwa na mzee wa busara Warioba, napendekeza apewe ulinzi madhubuti kuanzia sasa hadi Mungu atapomchukua, nadhani mkinisoma kwa makini mtanielewa nimemaanisha nini.
 
Serikali 2 ipo unaitakaje tena? tatizo imeshindwa kukidhi haja ndani ya miaka 50 iliyopita,hatuna budi kubadilika na kuangalia serikali 1 au 3.
Kwa hiyo kama wanawake wawili wamekushinda ndo uamue kuoa mke wa tatu? Si unarudi kuwa na mmoja tu au kutokuwa na mke kabisa?
 
[h=1]Bunge lavunjikaBUNGE Maalum la Katiba, limevunjika ghafla baada ya Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kukataa kuwasikiliza wajumbe waliokuwa wakimlalamikia kuvunja kanuni.[/h] Written by makame silima // 18/03/2014 // Habari // 1 Comment

PM-Miizengo-PInda-akibadilishana-mawazo-na-MP-wa-Urambo-Samuel-Sitta.jpg
Bunge lavunjika
Wajumbe waparaganyika, Warioba akwama kuhutubia
by Edson Kamukara
Bunge lavunjikaBUNGE Maalum la Katiba, limevunjika ghafla baada ya Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kukataa kuwasikiliza wajumbe waliokuwa wakimlalamikia kuvunja kanuni kwa kumruhusu Mwenyekiti wa Tume Maalum ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kuwasilisha rasimu ya Katiba badala ya Rais Kikwete kulihutubia Bunge.
Dalili za Bunge hilo kuingia dosari zilianza kuonekana tangu mapema mchana baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Uwaka) kutofautiana na Sitta kuhusu kutengua kanuni bila kufuata utaratibu.
Kanuni ya 7-(1) (g) na (h) inasomeka kuwa; 7- (1) Shughuli za Mkutano wa Bunge Maalum zitakuwa kama ifuatavyo: (g) hotuba ya ufunguzi ya Mgeni Rasmi (Rais Kikwete); (h), uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba (Jaji Warioba).
Hata hivyo Sitta alitengua kanuni hiyo ili kumpa nafasi Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba awasilishe rasimu ya katiba kabla ya hotuba ya ufunguzi ya Rais Jakaya Kikwete.

BONYEZA WEB

KAMATI YA MARIDHIANO SIX WARIOBA APIGWA STOP BUNGENI - YouTube
 
Mimi binafsi siupendi huo muungano!!

Akaunti ya pa! Haijaanzishwa!

Kama hawataki uvunjike basi serikali 3 zipite kwani zitavunjika tu huko mbele.!!

Nimemuona lema mjengoni halafu kaitwa kwenda kuapa hatjatokea.!!

Mungu mlinde huyu warioba!!
 
Kwa nondo za leo zinazoendelea kushushwa na mzee wa busara Warioba, napendekeza apewe ulinzi madhubuti kuanzia sasa hadi Mungu atapomchukua, nadhani mkinisoma kwa makini mtanielewa nimemaanisha nini.
Mkuu, huyu ni Mwenyekiti wa Tume ya Katiba hivyo ana walinzi. Na isitoshe ni Waziri Mkuu mstaafu hivyo lazima awe na walinzi
 
Warioba ni very straight na simple...CCM wana kazi sana kumuondoa kwa jinsi anamwaga ushahidi..JK anayo kazi kuleta porojo
 
Mimi binafsi siupendi huo muungano!!

Akaunti ya pa! Haijaanzishwa!

Kama hawataki uvunjike basi serikali 3 zipite kwani zitavunjika tu huko mbele.!!

Nimemuona lema mjengoni halafu kaitwa kwenda kuapa hatjatokea.!!

Mungu mlinde huyu warioba!!
Hakika mkuu.
 
Tuone sasa jinsi huyo JK anakavyomzima, sijui atakuja na hoja gani nzito zaidi ya hizi?

JK atakuwa na kazi ngumu sana ya kupangua hizi hoja...maana Mzee Warioba anatoa hoja kwa vielelezo...ni ngumu kwelikweli.
 
Warioba ni very straight na simple...CCM wana kazi sana kumuondoa kwa jinsi anamwaga ushahidi..JK anayo kazi kuleta porojo
Mkuu, CCM wametulia tuliiii. Wanajua kuwa wapo wengi na kelele za Warioba hazitawazuia kufanya maamuzi yao waliyokubaliana ndaninya chama.
 
Back
Top Bottom