Huduma katika hospitali za umma ni mbovu sana na zinatesa wananchi!

Hospital nyingi za serikali hasa za wilayani ni majanga leo nimempeleka wife na mtoto akachomwe chanjo kufika tunaambiwa eti hawana syringe mpaka waagize
 
Hii lazima ni Mwananyamara hapo.
 
Yupo mwana jf mmoja alileta kilio chake humu kwa kifo cha binti yake mdogo akiwa amecheleweshewa huduma hospital.

Nchi imekuwa ngumu, no where to breath, sembe 1800 kipande cha sabuni 900, hospital huduma mbovu.

Tumlilie nani.
 
Wapinzani walituchelewesha bwana , Acha muisome namba
 
Swala la afya nchi hii si mchzo
Inabidi ujipange kisawasawa
Matibabu ni ghali mno kwa baadhi
Ya matatizo ya mwili

Ova
 
Tulishauri hospital za umma zifungwe cctv camera ili kubaini uzembe wa watoa huduma
Alafu hizo video za kwenye cctv camera atakuwa anaziangalia malaika Gabriel maana watendaji wote kuanzia kwa Hangaya ni wabovuuuuu! Eti "watumishi walimuogopa Simba wa Yuda na kuwa na nidhami ya woga..." hahaha endeleeni kufurahia nidhamu "natural" ya watanzania!
 
Nidhamu natural ni ya mtu na kazi zake tuu!

Na kama kuna awaye yote aseme eti watumishi wanapaswa wawe na nidhamu bila kusimamiwa na kushushwa cheyo Kwa uzembe, hili halitatokea kwenye ofis zote!

Watu wanaukashifu mfumo wa kusimamiwa Kwa karibu, kushushwa cheyo na kutimliwa Kwa wazembe, ili tuu kuhalalisha uzembe wao ulio kwenye damu zao

Nidhamu ya uwogo ndio kila kitu, maana mtu akitii katika hali ya uwoga, na anafanya kazi, kunakuwa na tatizo lipi Kwa mwajiri?
 
kuna hospitali mfan mtwara referal hospitali inaoaswa kuwa na watumishi 200 ila wapo chini ya 50 unategemea huduna gani?
 
Ufinyu wa wahudumu, Fikiria mfano hospitari ya rufaa ya mtwara inapaswa kuwa na wahudumu 200+ lakini inao 48 tu, unategemea nini hapo?

jamaa anasema wahudumu wanakaa ofisini kupiga stori sio kweli hakuna mtu anayeweza kukaa tu huku watu wamemsubiri labda yeye kaona wanaopiga story ni watu wa OPD wakati mgonjwa yupo wodini hvyi ni vitengo viwili tofauti
 
Jamaa popoma sana Wafanyakazi wanafanya kazi 24 hours.Lakini bado wanapiga kazi kama Kawa.Yeye ajaribi kukesha hata siku moja aone moto wake.Watanzania ni watu wakulalamika sana.Alitaka akifika ahudumiwe yeye kwanza wengine 100 waachwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…