Paulsylvester
JF-Expert Member
- Oct 15, 2021
- 1,464
- 3,379
- Thread starter
- #81
Daah!Mambo ni mazito, jana nilikwenda Sekou Toure-Mwanza, nilikuwa sijaenda pale takribani mwaka hivi, nilifika pale nikakuta wamehamia kwenye jengo jipya la ghorofa.
Cha kusikitisha ni kwamba nilipita kwenye chumba cha dharula kwa ajili ya kupata huduma za kiofisi, ghafla kaletwa mgonjwa wa dharula akiwa amebebwa juu, juu akiwa amepoteza fahamu, nikasikia nesi akiuliza walo mleta;
Nesi:Huyo wa kike au kiume
Walombeba mgonjwa:Wa kiume.
Nesi:Hii wodi ya kiume imejaa, mpelekeni kule wodi ya kike, litakalo kuwa na liwe hatuna vyumba vya kutosha hapa chumba cha dharula.
Mimi nilijua kwakuwa jengo ni jipya labda huduma zitakuwa zimetengamaa, sasa ndiyo uone tupo wapi....
Kwa kuwa serikali na viongozi wake huwa wanapitia humu, hii watainusa na kufanyia kazi kwa haraka!
Ki ukweli, hali ni mbaya sana kwa mgonjwa kupata huduma hasa kwenye hospital zetu hizi za halaiki
Nadhani pia, kuwa tunapaka paka rangi kwenye uhalisia, ni makosa makubwa, wale chawa wa kila pahala hata kwa mambo yanayowagusa hata ukoo wao, wanafanya kazi ya shetani kupaka rangi kwa mambo yasiyopakwa rangi