Kwanza sina budi kutoa pongezi zangu kwa shirika hili la simu jinsi lilivyoingia kwenye soko la mawasiliano na huduma zake za maongezi T-PESA na INTERNET YA KASI KUBWA Kwa Bei nafuu, huku wakiwa na kaulimbiu yao ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA, kwa sasa mlipoharibikiwa ni hapa:
1. Kusajili laini zenu kwa fingerprints Dar es salaam mzima, huduma inapatikana Kariakoo na Posta tu.
2. Huduma ya vocha na T-PESA, mawakala hamna, ili update ni lazima upitie AIRTEL MONEY.
3. Ile internet ya 4G mlikuwa mnatupatia, kwa sasa hata ZERO-G haifiki
Sent using
Jamii Forums mobile app