Huenda hii ndio sababu ya kisayansi kwanini Kaini alimuua Habili (Abeli)

Huenda hii ndio sababu ya kisayansi kwanini Kaini alimuua Habili (Abeli)


Hakuna wa kudhihaki dini. Wewe umekaa umeleta mawazo yako kuwa Kaini alikuwa taahira wakati sio kweli. Hakuna verses kwenye Biblia zinazodhibitishwa hivyo. Unataka tuiamini hivyo. Biblia ni msitu mnene usisome Kama gazeti kujifurahisha au kukebehi dini za wengine.
 
Unajiita mkristo wakati hapo juu umetoka kusema Biblia ni stori za kutunga na zina loose ends.
Kwani kuwa mkristo ni lazima wote tuwe mbumbumbu kama makondoo tu, tupo wakristo tunaoijua vizuri biblia, kwamba imeandikwa na watu tu, kwa utashi wao, na ina mikanganyiko kibao, kama ilivyo Quruani.
 
Kwani kuwa mkristo ni lazima wote tuwe mbumbumbu kama makondoo tu, tupo wakristo tunaoijua vizuri biblia, kwamba imeandikwa na watu tu, kwa utashi wao, na ina mikanganyiko kibao, kama ilivyo Quruani.

Nakubishia , Biblia haina mikanganyiko na ipo sahihi kabisa.
 
Dogo wa llb first year bana. Unataka ni establish mens rea na actus reus.

Vyote vipo wazi

Mens rea = kamuua KWA sababu ya wivu kwamba eti sadaka yake imekubaliwa na Mungu.


Actus reus = tendo la kumuua Habili lime fanyika.


Motive ndio inayo FANYA mimi niseme Cain alikuwa insane.

Wewe unaweza kwenda kumuua kaka ako kwa sababu ametoa sadaka kubwa KWA Mwamposa kuliko uliyo itoa wewe?

Ukifanya hivyo tutakosea tukikuita insane?
Humjui huyo mtu Kaka chunga vidole vyako visiandike kwa jazba
Nenda naye kwa hekima.
 
Subirini jamani kwani hamuwezi kucommunicate na Mungu migogoro na migongano iishe

Hakuna mgogoro Biblia inajitosheleza. Mama Samiah alitoa ushauri tusome aya yote sio nusu aya. Mleta mada kasoma aya nusu halafu anataka wote tuifuate.
 
Kwa hivyo walikaa Chini wenyewe wakajitungia ya kuandika. Walivyojisikia?
Baadhi walitunga, na baadhi walirekodi historia za ukoo wao, Utasikia, "Henoko akamzaa Kenani, Kenani akamzaa Zebedayo, Zebadayo akamzaa sijui nani nakadhalika. Hizo ni historia za ukoo wao wayahudi, waliamua kuziweka kwenye kitabu.

Sehemu zingine wanazungumzia maisha yao tu..., Kama vile Yakobo akamuoa mke mdogo Rahel, Rahel akazaa Yusufu na Benyamini, Yusufu akauzwa utumwani Misri, akafungwa jela kisha akatolewa, akawa waziri mkuu. Hizo ni historia za maisha yao, Wayahudi.

Kwenye agano jipya sehemu kubwa wamerekodi mahubiri ya Yesu, yule mtoto wa fundi seremala.
 
Upo sahih kwenye mtazamo wa mungu kuumba watu wawili walianzaje kuingiliana ndugu kwa ndugu maisha hayana mwanzo yalikuwepo

Unataka uwe na mawazo sahihi Kama Mungu?. Ujue kila kitu?. Kuna mambo ni Mungu pekee anayafahamu sio mwanadamu.
 
Ukisoma kisa cha Kaini na Habili ( watoto wa Adam na HAWA ambao KWA mujibu wa mafundisho ya wakristo, waislamu na Wayahudi ina aminika ndio binadamu wa kwanza duniani jambo ambalo ni kinyume na mafundisho ya imani za jadi za kiafrika)

Utagundua kwamba Cain killed Abel over bullshit. Hakukuwa na sababu yoyote ile ya msingi ya ku mfanya Kaini amuue Habili.

Waulize wachungaji hivi ni sababu GANI hasa iliyo mfanya Kaini amuue nduguye Habili?

Utasikia ooh Kaini aliona wivu KWA Habili KWA sababu sadaka ya Habili ilikubalika mbele za Mungu. . Blah blah blah. Alijuaje kama sadaka ya Habili imekubalika mbele za Mungu?

Kama sadaka ya Habili ilikubalika mbele za Mungu na sadaka ya Kaini haijakubalika kwanini Habili ambae sadaka yake ndo imekubalika (mwenye haki) ndio afe na Kaini ambae sadaka yake haijakubalika (asie na haki) aishi..


Jibu ni moja tu kwamba adhabu ya kutoa sadaka inayo kubalika mbele za Mungu ni kuuwawa.

Now back to my topic

Kaini alikuwa TAAHIRA.

KWANINI KAINI ALIKUWA TAAHIRA?

Ni sababu za kisayansi.

KWA mujibu wa maandiko Kaini na Habili wali share the same father with their mother. Yani baba wa Kaini na Habili ndio huyo huyo alikuwa baba wa mama mzazi wa Kaini na Habili.


Yes KWA mujibu wa maandiko HAWA alikuwa mtoto wa Adam.

Adam alikuwa ndio baba wa HAWA.

Adamu alikuwa ndio mama wa HAWA.

Adamu hakusema " she is flesh of my flesh and bones of my bones" kimakosa.

Without a doubt !!! Eve was a biological daughter of Adam

Sayansi inasema baba na binti au dada na kaka endapo watazaa mtoto basi kuna uwezekano mkubwa sana wakazaa mtoto mwenye matatizo ya akili.

Ndivyo ilivyo kuwa kwa Kaini. Kaini alikuwa na matatizo ya akili. Ningekuwa wakili wa Kaini mbele za Mungu ninge raise defense ya Insanity.

Ningemwambia Mungu kwamba mteja wangu Kaini ana tatizo la akili..wakati anafanya tukio la kumuua ndugu yake his right part of his brain was left and his left part of his brain was not right.

Kama Kaini angekuwa SAWA SAWA kichwani asinge muua ndugu yake.

Ange enda na yeye kutoa sadaka kama aliyo toa Habili. Kaini alikuwa mgonjwa wa akili.period. Je sisi waafrika ni kizazi cha Adam?

The evidence says No.

Mungu hakuumba watu wawili tu duniani. Aliumba a hundred of thousand of couples.( This will be a topic for another day)
Sio kweli.... Mambo ya koroho tofauti na elimu za kidunia.
 
Baadhi walitunga, na baadhi walirekodi historia za ukoo wao, Utasikia, "Henoko akamzaa Kenani, Kenani akamzaa Zebedayo, Zebadayo akamzaa sijui nani nakadhalika. Hizo ni historia za ukoo wao wayahudi, waliamua kuziweka kwenye kitabu.

Sehemu zingine wanazungumzia maisha yao tu..., Kama vile Yakobo akamuoa mke mdogo Rahel, Rahel akazaa Yusufu na Benyamini, Yusufu akauzwa utumwani Misri, akafungwa jela kisha akatolewa, akawa waziri mkuu. Hizo ni historia za maisha yao, Wayahudi.

Kwenye agano jipya sehemu kubwa wamerekodi mahubiri ya Yesu, yule mtoto wa fundi seremala.

Sio kweli, Biblia wameipanga kulingana na Nia ya kitabu na sio umri wa kitabu.

1. Kundi la kwanza vitabu vya torati. Maagano Kati ya Israel na Mungu.
2. Kundi la pili Ni vitabu vya Historia.
3. Kundi la tatu vitabu vya Zaburi
4. Kundi la nne vitabu vya manabii wadogo
5. Kundi la tano vitabu vya manabii wakubwa.

Unaposoma kitabu Cha mwanzo kinatuelekeza Mwanzo wa Dunia ulivoanza, mpango wa Mungu kwa mwandamu, mwandamu wa kwanza,dhambi ya kwanza, mauaji ya kwanza, uasi wa mwandamu wa kwanza, hasira ya Mungu ya kwanza etc.

Kwenye suala la Kaini Biblia inajaribu kutuonesha kwamba dhambi huwa haiji kwa siku moja bali huwa inamnyemelea mtu, na asipokaa vizuri inamvaa. Ndicho kilichotokea kwa kaini.

Uzuri wa Biblia ukiielewa Wala hungaiki lakini usipoielewa utajitungia mambo yako na kilazimisha yawe kweli.
 
Ili uwe na haki ya kuikosoa Biblia lazima uyafahamu yafuatayo:

1. Mchanganuo wa Biblia nzima. Biblia imegawanywaje.
2. Mwandishi wa kitabu husika.
3. Walengwa wa kitabu husika.
4. Mpangilio wa aya za kitabu husika.
5. Ujumbe wa kitabu husika.
6. Tafsiri ya maandiko kwenye kitabu husika.
7. Application ya kitabu husika kwenye Dunia ya leo.

Lakini ukiipinga Biblia bila hiyo knowlegde ya hayo mambo Saba utakuwa unakosea.
 
Back
Top Bottom