Huenda hii ndio sababu ya kisayansi kwanini Kaini alimuua Habili (Abeli)


Hakuna wa kudhihaki dini. Wewe umekaa umeleta mawazo yako kuwa Kaini alikuwa taahira wakati sio kweli. Hakuna verses kwenye Biblia zinazodhibitishwa hivyo. Unataka tuiamini hivyo. Biblia ni msitu mnene usisome Kama gazeti kujifurahisha au kukebehi dini za wengine.
 
Unajiita mkristo wakati hapo juu umetoka kusema Biblia ni stori za kutunga na zina loose ends.
Kwani kuwa mkristo ni lazima wote tuwe mbumbumbu kama makondoo tu, tupo wakristo tunaoijua vizuri biblia, kwamba imeandikwa na watu tu, kwa utashi wao, na ina mikanganyiko kibao, kama ilivyo Quruani.
 
Kwani kuwa mkristo ni lazima wote tuwe mbumbumbu kama makondoo tu, tupo wakristo tunaoijua vizuri biblia, kwamba imeandikwa na watu tu, kwa utashi wao, na ina mikanganyiko kibao, kama ilivyo Quruani.

Nakubishia , Biblia haina mikanganyiko na ipo sahihi kabisa.
 
Humjui huyo mtu Kaka chunga vidole vyako visiandike kwa jazba
Nenda naye kwa hekima.
 
Subirini jamani kwani hamuwezi kucommunicate na Mungu migogoro na migongano iishe

Hakuna mgogoro Biblia inajitosheleza. Mama Samiah alitoa ushauri tusome aya yote sio nusu aya. Mleta mada kasoma aya nusu halafu anataka wote tuifuate.
 
Kwa hivyo walikaa Chini wenyewe wakajitungia ya kuandika. Walivyojisikia?
Baadhi walitunga, na baadhi walirekodi historia za ukoo wao, Utasikia, "Henoko akamzaa Kenani, Kenani akamzaa Zebedayo, Zebadayo akamzaa sijui nani nakadhalika. Hizo ni historia za ukoo wao wayahudi, waliamua kuziweka kwenye kitabu.

Sehemu zingine wanazungumzia maisha yao tu..., Kama vile Yakobo akamuoa mke mdogo Rahel, Rahel akazaa Yusufu na Benyamini, Yusufu akauzwa utumwani Misri, akafungwa jela kisha akatolewa, akawa waziri mkuu. Hizo ni historia za maisha yao, Wayahudi.

Kwenye agano jipya sehemu kubwa wamerekodi mahubiri ya Yesu, yule mtoto wa fundi seremala.
 
Upo sahih kwenye mtazamo wa mungu kuumba watu wawili walianzaje kuingiliana ndugu kwa ndugu maisha hayana mwanzo yalikuwepo

Unataka uwe na mawazo sahihi Kama Mungu?. Ujue kila kitu?. Kuna mambo ni Mungu pekee anayafahamu sio mwanadamu.
 
Sio kweli.... Mambo ya koroho tofauti na elimu za kidunia.
 

Sio kweli, Biblia wameipanga kulingana na Nia ya kitabu na sio umri wa kitabu.

1. Kundi la kwanza vitabu vya torati. Maagano Kati ya Israel na Mungu.
2. Kundi la pili Ni vitabu vya Historia.
3. Kundi la tatu vitabu vya Zaburi
4. Kundi la nne vitabu vya manabii wadogo
5. Kundi la tano vitabu vya manabii wakubwa.

Unaposoma kitabu Cha mwanzo kinatuelekeza Mwanzo wa Dunia ulivoanza, mpango wa Mungu kwa mwandamu, mwandamu wa kwanza,dhambi ya kwanza, mauaji ya kwanza, uasi wa mwandamu wa kwanza, hasira ya Mungu ya kwanza etc.

Kwenye suala la Kaini Biblia inajaribu kutuonesha kwamba dhambi huwa haiji kwa siku moja bali huwa inamnyemelea mtu, na asipokaa vizuri inamvaa. Ndicho kilichotokea kwa kaini.

Uzuri wa Biblia ukiielewa Wala hungaiki lakini usipoielewa utajitungia mambo yako na kilazimisha yawe kweli.
 
Ili uwe na haki ya kuikosoa Biblia lazima uyafahamu yafuatayo:

1. Mchanganuo wa Biblia nzima. Biblia imegawanywaje.
2. Mwandishi wa kitabu husika.
3. Walengwa wa kitabu husika.
4. Mpangilio wa aya za kitabu husika.
5. Ujumbe wa kitabu husika.
6. Tafsiri ya maandiko kwenye kitabu husika.
7. Application ya kitabu husika kwenye Dunia ya leo.

Lakini ukiipinga Biblia bila hiyo knowlegde ya hayo mambo Saba utakuwa unakosea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…