Tangawizi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 8,072
- 8,942
Hatua hiyo itasaidi pakubwa kuimarisha demokrasia, uwazi, utawala bora na utawala wa sheria nchini.
Kufutwa kwa Chadema kama chama cha siasa itakua ni ni fursa muhimu kwa vyama vingine vya siasa kukomaa, lakini pia itakua ni mwanzo mpya wa zama za siasa za kistaarabu Tanzania. Kubwa zaidi itakua ni fundisho kwa vyama vingine vya siasa kudumisha amani, siasa za kistaarabu, uhuru, haki na uwazi katika masuala yote yahusuyo chaguzi za amani nchini Tanzania.
una maoni gani kwenye hili.
Chadema ifutwe au izuiwe kufanya siasa Tanzania?
Mungu Ibariki Tanzania.
Mwalimu Nyerere, aliposikia kuhusu Azimio la Zanzibar ambalo liliua rasmi Azimio la Arusha, kwa kuruhusu viongozi wa umma kuanza kujilimbikizia mali...na ndio mwanzo wa kuanza kula rushwa kubwa kubwa kama za IPTL, aliwahi kusema, mawazo makubwa makubwa hayafi kirahisi rahisi. Huwa yana tabia ya kukataa kufa.
Kila la kheri katika safari yenu ya kisiasa wana nzengo. Mkifika mnakoenda mtujulishe 😂 😂 😂 😂 😂

