mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Mkuu pengine umeamua kufanya "negation" katika hii sentensi yako ili kufikisha ujumbe sahihi.CCM NI WAADILIFU SANA, WENGI WA VIONGOZI NI WACHAMUNGU SANA
Nakumbuka enzi hizo tukiwa chipukizi na damu changa ya wana CCM, huku tukiaminishwa ya kuwa sisi ni taifa la kesho, kwa hamasa kubwa tulitelekeza masomo ya shule za msingi na kwenda kupokea viongozi wa chama wa kitaifa, kushiriki onyesho la halaiki ya vitabu, na pia hata kucheza gwaride wakati wa sikukuu za kitaifa.
Tukiwa elimu ya sekondari tulijiunga na UVCCM kwa matarajio ya ahadi hiyo hiyo kuwa vijana ni taifa la kesho. Tulipojiunga na JKT kwa mujibu wa sheria tulilazimika kuwa wanachama wa CCM.
Lakini ilikuwa kipindi hili ndipo viguvugu la vyama vingi lilirejea tena hapa nchini, na ninakumbuka kipindi hicho nilipiga kura ya kutoutaka mfumo wa vyama uje hapa nchini. Licha ya ukereketwa wangu wa wakati huo, ninashukuru Mwl. Nyerere alitunusuru Watanzania kwa kutambua ukweli kwamba mfumo huu ni muhimu mno na wala haukwepeki.
Kauli ya thabiti ya Kambarage ya kuwa CCM si baba wala mama yake, na yupo tayari kurudisha kadi yake na kujiunga na chama kingine chenye kujali Watanzania ilinifungua akili. Kuanzia muda huo ukimbelembele wangu kwa shughuli za chama hiki ndipo ukafa rasmi.