Huenda mabadiliko makubwa yakafanywa ndani ya Serikali muda mfupi ujao. RAS, DCs, DAS, DEDs baadhi yenu mmekuwa mizigo kwa nchi

Huenda mabadiliko makubwa yakafanywa ndani ya Serikali muda mfupi ujao. RAS, DCs, DAS, DEDs baadhi yenu mmekuwa mizigo kwa nchi

CCM NI WAADILIFU SANA, WENGI WA VIONGOZI NI WACHAMUNGU SANA
Mkuu pengine umeamua kufanya "negation" katika hii sentensi yako ili kufikisha ujumbe sahihi.

Nakumbuka enzi hizo tukiwa chipukizi na damu changa ya wana CCM, huku tukiaminishwa ya kuwa sisi ni taifa la kesho, kwa hamasa kubwa tulitelekeza masomo ya shule za msingi na kwenda kupokea viongozi wa chama wa kitaifa, kushiriki onyesho la halaiki ya vitabu, na pia hata kucheza gwaride wakati wa sikukuu za kitaifa.

Tukiwa elimu ya sekondari tulijiunga na UVCCM kwa matarajio ya ahadi hiyo hiyo kuwa vijana ni taifa la kesho. Tulipojiunga na JKT kwa mujibu wa sheria tulilazimika kuwa wanachama wa CCM.

Lakini ilikuwa kipindi hili ndipo viguvugu la vyama vingi lilirejea tena hapa nchini, na ninakumbuka kipindi hicho nilipiga kura ya kutoutaka mfumo wa vyama uje hapa nchini. Licha ya ukereketwa wangu wa wakati huo, ninashukuru Mwl. Nyerere alitunusuru Watanzania kwa kutambua ukweli kwamba mfumo huu ni muhimu mno na wala haukwepeki.

Kauli ya thabiti ya Kambarage ya kuwa CCM si baba wala mama yake, na yupo tayari kurudisha kadi yake na kujiunga na chama kingine chenye kujali Watanzania ilinifungua akili. Kuanzia muda huo ukimbelembele wangu kwa shughuli za chama hiki ndipo ukafa rasmi.
 
Kama hii ndio dira ya chama/Rais basi kazi tunayo.
Nilidhani utasema wengi wao hawana ubunifu kazini ili kutatua shida za wananchi, hawasimamii vizuri mapato na matumizi kwenye ofisi zao na pengine labda wamekua viburi kuwatukia wananchi.
Lakini kwako wewe mizigo unayoiona ni kusifia tu mwanzo mwisho.

Hii ndo Tanzania ya hovyo
 
Mkuu pengine umeamua kufanya "negation" katika hii sentensi yako ili kufikisha ujumbe sahihi.

Nakumbuka enzi hizo tukiwa chipukizi na damu changa ya wana CCM, huku tukiaminishwa ya kuwa sisi ni taifa la kesho, kwa hamasa kubwa tulitelekeza masomo ya shule za msingi na kwenda kupokea viongozi wa chama wa kitaifa, kushiriki onyesho la halaiki ya vitabu, na pia hata kucheza gwaride wakati wa sikukuu za kitaifa.

Tukiwa elimu ya sekondari tulijiunga na UVCCM kwa matarajio ya ahadi hiyo hiyo kuwa vijana ni taifa la kesho. Tulipojiunga na JKT kwa mujibu wa sheria tulilazimika kuwa wanachama wa CCM.

Lakini ilikuwa kipindi hili ndipo viguvugu la vyama vingi lilirejea tena hapa nchini, na ninakumbuka kipindi hicho nilipiga kura ya kutoutaka mfumo wa vyama uje hapa nchini. Licha ya ukereketwa wangu wa wakati huo, ninashukuru Mwl. Nyerere alitunusuru Watanzania kwa kutambua ukweli kwamba mfumo huu ni muhimu mno na wala haukwepeki.

Kauli ya thabiti ya Kambarage ya kuwa CCM si baba wala mama yake, na yupo tayari kurudisha kadi yake na kujiunga na chama kingine chenye kujali Watanzania ilinifungua akili. Kuanzia muda huo ukimbelembele wangu kwa shughuli za chama hiki ndipo ukafa rasmi.
Tatzo ata hcho chama cha kujiunga nacho kipo? Maana vilivyobaki ndo zero kabsa
 
Wateuliwa amani iwe kwenu,

Huenda wakati Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anakwenda kufanya mabadiliko makubwa Serikalini Mimi Wacha niwalaumu kidogo na endapo Wewe utasalia rekebisha hili,

Viongozi wetu, Miongoni mwenu mmegeuka mabubu ghafla tu baada ya kifo cha Hayati Rais Magufuli , leo wala hakuna anayemtetea Rais Samia Suluhu Wala Serikali yetu,wote mmepiga kimya,Sijui ni kwa bahati mbaya au ni kwa kusudio!!??

Viongozi wetu, Wengi wenu mmekuwa mkijifanya nyie ni Wana-Serikali zaidi ya kuwa wanachama hata sare za Chama wengi wenu hamna na hamvai eti nyie ni Serikali,

Viongozi wetu, Tunakumbuka wakati wa JPM mlikuwa wasemaji wazuri sana wa miradi ya Serikali Ila leo mmegeuka mabubu kwa vigezo eti Mama hataki kusemewa vizuri kwa wananchi hili nani kawaambia na lini?

Viongozi wetu, Sisi wanachama/Wananchi tunahitaji viongozi walio Watendaji na Wasemaji, Haiwezekani Mkuu wa Mkoa au Waziri hana hata akaunti moja mtandaoni,

Viongozi wetu,Leo zaidi ya Watanzania 25m wanamiliki simu Janja,Wewe kiongozi wao huna akaunti hata ya kupost barabara inayojengwa kwenye eneo lako kisa eti Wewe ni RC au Waziri unatuchelewesha sana,

Viongozi wetu,Mtakumbuka Rais wa nchi kubwa kama Donald Trump alitumia mtandao wa tweeter tu kuongoza nchi kubwa kama Marekani why Wewe mwenye Wilaya tu,

Sote tunafahamu Rais wa JMT Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan anayo akaunti Official kule tweeter Wewe DED huna ata akaunti moja kisa eti ni boss hakika kwenye karne hii 21 Wewe haustahili tupishe,

Sasa, huenda mabadiliko makubwa yakafanywa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ndani ya Serikali muda mfupi ujao nyie Mawaziri, RAS, DCs, DAS, DEDs baadhi yenu mmekuwa mizigo kwa nchi, Mmegeuka mabubu ghafla baada ya kifo cha JPM lazima muwajibike kwenye hili,​

[Kidumu chama cha Mapinduzi ]

View attachment 2440539

Walamba asali km mzee makamba ni hatari kwa mama na taifa kwa ujumla
 
Tatzo ata hcho chama cha kujiunga nacho kipo? Maana vilivyobaki ndo zero kabsa
Mkuu, kwa uzoefu tulioupata ndani ya CCM, ninafuu kuzidi kuunga mkono upinzani kupitia chama cochote kile unachokiona kinafaa, mathalani CDM, ACT Wazalendo, NCCR Mageuzi au CUF, kuliko kuzidi kuliunga mkono kundi dogo lililokiteka chama tawala na kugeuka kuwa wabadhilifu, wahujumu uchumi, na wezi wa mali za umma.
 
Hata hao wapinzani ni kwamba hawana tu hayo madaraka ila wakipewa ndo kabisa
 
Hata hao wapinzani ni kwamba hawana tu hayo madaraka ila wakipewa ndo kabisa
Tunaweza kukubali kutokukubaliana katika hilo, lakini kiwango cha uhujumu na ubadhirifu wa mali za umma kwa manufaa ya kikundi cha wana CCM wachache imefika kiasi sasa kina kera.

Kundi la watu wachache hata hawana "background" yoyote ile katika historia ya waasisi wa taifa hili, ama wale waliopigania Uhuru, wapejipachika na kujifanya wao, familia zao pamoja na rafiki zao wa karibu, ndiyo pekee wnye haki ya kuiongoza nchi hii na kunufaika na rasilimali zake.

Suala muhimu ni kuliondoa kundi hili madarakani, kabla halijaota mizizi. Ni vyema kuiondoa CCM madarakani ili ikiwezekana chama kingine kitwae dola. Itakuwa ni rahisi sana kukiondoa madarakani kikifanya vibaya, kuliko kuendekeza uchama dola wa CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaweza kuwa hoja ya kuwamaliza masalia na kujenga mtandao tata mpya
 
Unabadilishaje ma DC,das,ded
huku
Wakuu wa idara na vitengo waachwa wanajenga mazoea yya kipuuzipuuzi.

Heads of department and unit Hawa inatakiwa iendane na kuwashusha vyeo...

Miaka na miaka wanasababisha ma DC,das,ded wanatenguliwa wao Wana kula posho kisheria. Wanaohudumiwa na kisaidia kuhudumia wakiteseka na usafiri wa bodaboda, Bajaji na Kwa miguu. Mazingira magumu...Hawa watu hawajaki kabisa yani

Tena waanze sekta ya Elimu.

Maafisa Elimu wachujwe...anayofanya vema kwenye kuhudumia watendaji wake.

Mwenye upeo na utendaji uliotukuka awe atambuliwe. Sio wahuni wahuni wanaambukizana ukimwi tu.

Angalizo.
Ukiitumia Tamisemi ikufanyie hili ni sawa na kupeleka kesi ya fisi kwa mizoga
 
Watu watapimwa kwa ufanisi Wala sio mtandao,
Je mitazamo yetu ni sawa na yao?
Unadhani kwa vijembe vile vya Uzi Mkubwa kwa waafu Uzi Mdogo utatemwa baada ya kulalamikiwa pumzi yake akiongea inazima vibatari vyetu?
 
Kuna nyuzi ukizisoma unabaki kujiiuliza hivi huyu mtu anafikiria kwa utumia kiungo gani cha mwili,
 
Walamba asali km mzee makamba ni hatari kwa mama na taifa kwa ujumla
Kwa maneno ya JK, Makamba sr, na mama siku ile wanafunga mkutano basi mabaliko serikalini maana yake ni majanga kwa wale "wakuja" na makada chawa wataingizwa kwenye cycle, kuna hatari mawaziri , Dc, Rc, DAS na wengineo ambao walibebwa na JPM wakapigwa chini bila huruma kupisha makada ili nao wakalambe asali kuelekea uchaguzi wa 2025
 
Je mitazamo yetu ni sawa na yao?
Unadhani kwa vijembe vile vya Uzi Mkubwa kwa waafu Uzi Mdogo utatemwa baada ya kulalamikiwa pumzi yake akiongea inazima vibatari vyetu?
Sijakuelewa hapa Faana
 
CCM yote ni mzigo kwa watanzania.

Hao wanaofurahia wanafurahi kwasababu wanajua sasa wanaweza kupata nafasi(zamu yao imefika) na si kwasababu nyingine yoyote.

Hapo Rizmoja anaenda kuwa Waziri kamili na Majaliwa anapumzishwa.
Wote wapiga dili tupu
 
Back
Top Bottom