ras jeff kapita
JF-Expert Member
- Jan 4, 2015
- 22,152
- 33,899
Ni kweli kuna upepo flani sshv unavuma sio wa kawaida ni nyakati za wanawake hizi hata kazi nyingi kwenye international organisation ie UN zikitangazwa kwa chini unaona zimeandikwa women are encouraged to apply!!?Huko Marekani kwa mara ya Kwanza katika Historia yao Makamu wa Rais wa sasa ni Mwanamke Kamala Harris.
Nchini Tanzania kwa sasa na haikuwahi kutokea Rais wa nchi ni Mwanamke Mama Samia Hassan.
Huko nchini Kenya pia katika Historia yao kwa mara ya Kwanza leo imempata Jaji Mkuu Mwanamke Martha Koome.
Katika Maisha ya sasa ( tena huku Vyuma vikiwa Vimekaza ) ila cha Kushangaza Wanawake wanazidi tu kuwa na Uchumi mkubwa na Sisi Wanaume tunadidimia tu.
Huenda kuna mahala Wanaume tumefeli na huenda hata Baba Muumba ( Mwenyezi Mungu ) nae katuchoka vile vile hivyo anatukomesha sasa Kiaina.
Nawapongeza Wanawake wote duniani.