Huenda Mwenyezi Mungu sasa katuchoka Wanaume na ameamua kuwainua Wanawake katika nyadhifa kubwa za kiuongozi Duniani ili tujifunze kwao

Ni kweli kuna upepo flani sshv unavuma sio wa kawaida ni nyakati za wanawake hizi hata kazi nyingi kwenye international organisation ie UN zikitangazwa kwa chini unaona zimeandikwa women are encouraged to apply!!?
 
Ndiyo kusema Wanaume tumekuwa Mapopoma siku hizi hadi Wanawake wanatupiku au kuna tatizo gani labda?
Tatizo ni ukosefu wa nguvu za kiume si unaona hata bungeni wanatusema..!!! Yaani nguvu za kiume zimegeuka na kuwa nguvu za kike
 
Kwa Kenya Lady Justice Martha Koome amependekezwa na JSC(Judicial Services Commission) kuwa the coming CJ..

Then jina lake linapelekwa kwa Rais nae analipeleka Bungeni for final endorsement..

Bunge likimkataa, mchakato wa kupata CJ mwingine unaanza upya kabisa..

So kwa Kenya mchakato bado haujakamilika na anything can happen sababu Bunge lao sio kama la Tanzania linalopitisha kila kitu..anything can happen.
 
Rais Samia aliongoza vizuri bunge gumu la katiba alipopewa nafasi, atashindwa vipi kuiongoza CCM muda huu.

Mfumo dume unakwenda unapungua nguvu kila kukicha. Na wanawake wameweza kuutetea mchango wao kidunia.

Kila wanapoweza kuwa na mawakili wengi, kunakuwepo na utetezi mkubwa wa maslahi yao.. Utetezi ukizidi kuongezeka na kile wanachoweza kukifanya kwa mafanikio kinazidi kuonekana.
 
''... tukilichukulia kisayansi zaidi tunagundua kuwa mpambano wa kuwania madaraka miongoni mwa wanaume umekuwa mkali sana wakati kwa jinsia ya pili kuna 'affirmative action' na huruma/aibu za wababa linapoibuka la kupambana na kina mama ... UNATEGEMEA NINI HAPO? ...CHEKECHEO LINACHAGUA JINSIA NA KWA WALE, WAMAMA, WALIOZIDISHIWA KIDOGO TU HORMONES ZA KIUME KAZI INAKUWA LAINI SANA!
😎
 
100% atapitishwa Yeye tu acha Kubisha.
 
Ila kwa sasa wameibuka kwa Kasi sana.
Ukiwa pale international road hammer zote wanaendesha wanawake wakitoe kusikojulikana,by the way hawa watu ni viumbe zaidi ya makini,wanavumilia mpaka unajishtukia
 
Kwani ni lini tulikwambia sisi wanamume tunashindana na wanawake??

Yaani kabisa tukae, vikao tunawaza sasa hivi wanawake wanatuzidi!!!

Huo siyo uanamume.
 
Ni dalili ya mwisho wa dunia wanawake kua watawala...!
 
Ukiwa pale international road hammer zote wanaendesha wanawake wakitoe kusikojulikana,by the way hawa watu ni viumbe zaidi ya makini,wanavumilia mpaka unajishtukia
Ipo wapi hiyo road kwa hapa Dar? Nataka siku moja nikashuhudie kaka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…